Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mashambulizi (Tisa Ndefu) Hayataangamizwa Isipokuwa kwa Utekelezaji wa Hukumu za Kisharia Chini ya Dola ya Ukhalifa
Mwandishi wa habari wa tovuti ya Kush News, Habiba Al-Amin, alishambuliwa vikali na watu wanaohusishwa na kundi la "Tisa Ndefu," katika eneo la Transit katika jiji la Port Sudan, alipokuwa akirejea kutoka kwa ripoti ya vyombo vya habari, akiwa ameandamana na idadi ya wenzake. Hili ni tukio moja tu kati ya matukio mengi ya wizi, uporaji na mauaji, ndani ya miji ambayo inadhaniwa kuwa salama, kama vile Omdurman na Khartoum, na sasa katika mji mkuu wa utawala wa Port Sudan, kwani hizi ni miji chini ya udhibiti wa serikali, na vyombo vyake vya usalama.
Lakini wahalifu wanashambulia kwa ujasiri wote, kana kwamba wanaamini kwamba mkono wa serikali hautawafikia, na hata ukiwafikia, wana uhakika, kwa sababu ya udhaifu wa adhabu ya kuzuia, licha ya ukubwa wa uhalifu uliofanywa.
Hakuna anayepinga kwamba kuenea kwa uhalifu hakuwezi kuzuiwa isipokuwa kwa kutekeleza hukumu za Kisharia, kwani kanuni ya Kisharia ni kwamba (Hukumu ni za kuzuia na za kulipa); ni za kuzuia kutenda uhalifu, na msamaha kwa yule ambaye hukumu imetekelezwa kwake, inalipa adhabu ya Akhera.
Kutoka kwa Abdullah bin Omar alisema: «Mtume ﷺ alikata mkono kwa ngao yenye thamani ya dirhamu tatu» Imetolewa na Ibn Majah, na matamshi ni yake, na imetolewa na Bukhari na Muslim. Katika riwaya: «Kwamba Mtume ﷺ alikata mkono wa mtu aliyeiba ngao kutoka safu ya wanawake yenye thamani ya dirhamu tatu» Sahih Abu Dawood, Al-Nasa'i, na wengineo.
Ama wale wanaowatisha watu salama, na kufanya mauaji, unyang'anyi, wizi na uporaji, kwa nguvu ya silaha kama ilivyo kwa (Tisa Ndefu), aya tukufu zimewazuia na kuwakatisha tamaa, Mwenyezi Mungu alisema: ﴿Hakika malipo ya wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya juhudi za ufisadi katika ardhi ni kuuliwa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa kupishana au kuhamishwa kutoka katika ardhi. Hiyo ni fedheha kwao katika dunia, na katika Akhera watapata adhabu kubwa﴾, Lau serikali ingefanya na kutekeleza hukumu moja tu ya mipaka ya Mwenyezi Mungu, wahalifu wote wangestaafu, lakini inaonekana kuwa ni heshima ambayo haistahili, kwa hivyo tunaiona ikizunguka yenyewe ikidhani kwamba kuteua waziri wa mambo ya ndani, au kupeleka polisi katikati ya nchi, au kuandaa kampeni za kuzuia, kutaleta mabadiliko, lakini hali inazidi kuwa mbaya.
Hukumu za Kisharia hazitekelezwi isipokuwa chini ya kivuli cha dola ya Kiislamu; Ukhalifa ulioongoka kwenye njia ya unabii, ni yenyewe tu ndiyo inayowazuia wahalifu, na kuwakatisha tamaa. Ama mifumo ya kidemokrasia, huzaa wahalifu, na hata hutengeneza uhalifu, na inalinda ufisadi, kwa sababu ya udhaifu wa adhabu zao, wanafikiri kwamba wana huruma zaidi kwa watu kuliko Muumba wao, na hakuna dhambi baada ya ukafiri.
Je, watu wa nguvu na ulinzi katika nchi yetu wataitikia wito wa Rehemani, na kutoa ushindi kwa Hizb ut-Tahrir, ili kufanya bay'ah ya kisheria kwa Khalifa Rashid, anayeanzisha haki, na kueneza usalama, na kuwazuia wahalifu; wakubwa wao kabla ya wadogo wao, kama ushahidi wa kauli yake ﷺ: «Hakika Imamu ni ngao, anapiganwa nyuma yake na kulindwa naye»?!
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye jambo liliyo hai kwenu﴾
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Jimbo la Sudan