Msururu wa "Ukhalifa na Uimamu katika Fikra ya Kiislamu" - Kwa Mwandishi na Mwanafikra Thaer Salama - Abu Malik - Sehemu ya 48
Ukhalifa ni kusimama kitu mahali pa kitu, na hukumu ni ya Mwenyezi Mungu, na amewajaalia viumbe kwa ujumla kwa kauli yake ﷺ: «Hakika dunia ni tamu na ya kijani kibichi, na Mwenyezi Mungu anakufanyeni makhalifa ndani yake, ili aone mnavyotenda» Imepokewa na Muslim kutoka kwa Abu Saeed Al-Khudri, kuthibitisha kauli yake Mwenyezi Mungu ﴿Kisha tukakufanyeni makhalifa katika ardhi baada yao ili tuone mnavyotenda﴾ [Yunus: 14], yaani mtekeleze hukumu za Mwenyezi Mungu, na manhaj ya Mwenyezi Mungu baina yenu na juu ya nafsi zenu katika kila jambo, na ukhalifa kwa khasa katika hukumu, kutoka kwa mtawala anahukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, kwani manhaj hii ndio inayotofautisha baina ya anayefanywa khalifa katika ardhi awe ni mharibifu ndani yake, mtoaji damu, au awe ni khalifa anaye kingwa na manhaj hiyo kutokana na kosa hilo, na ili itawale manhaj lazima itawale kupitia dola, siyo tu kwamba wafuate watu katika jamii ambayo inatawaliwa na manhaj isiyo hiyo!