Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kukamatwa kwa Vijana wa Hizb ut-Tahrir katika Mji Mkuu wa Beirut!
Katika kurudi kwenye mbinu ya kukamatwa kiholela, na vitendo vya vyombo vya usalama bila hati yoyote ya kisheria, watu - waliojulikana baadaye kuwa kutoka kwa chombo cha usalama kinachohusiana na mamlaka - wakiwa kwenye pikipiki waliwakamata vijana wawili kutoka Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Lebanon walipokuwa wakisambaza taarifa ikilaani kuendelea kwa uchokozi wa Wayahudi dhidi ya Lebanon na watu wake, jana tarehe 17/10/2025 baada ya sala ya Ijumaa kutoka mbele ya Msikiti wa Imam Ali katika eneo la Tariq al-Jadida katika mji mkuu wa Beirut!
Je, Lebanon itahifadhi, kwa ahadi yake mpya chini ya uongozi wa kamanda wa zamani wa jeshi na hakimu wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki - ambao waliahidi utawala wa sheria - mbinu za mifumo iliyopita?! Halafu ni nini kimewatisha kutoka Hizb ut-Tahrir? Je, ni kulaani kwake uchokozi wa Wayahudi?! Au kuzungumza kwake juu ya mwelekeo wa mamlaka katika njia ya kurejesha uhusiano wa kawaida na kujisalimisha ambayo inaendeshwa na Amerika?! Au wito wake wa kukabiliana na kampeni za Wayahudi na Amerika huko Lebanon na kanda?! Au ni jaribio la kunyamazisha midomo licha ya mabadiliko yanayodaiwa katika mbinu ya mamlaka na viongozi wake wa usalama ambao wanadai kufanya kazi ya kupata utawala wa sheria?!
Hakika, watu wote wanajua kuwa Hizb ut-Tahrir haitanyamazishwa na mbinu hizi, na uzoefu wao nayo unashuhudia hilo huko Lebanon na kwingineko, na chama kitaendelea kukabiliana na uchokozi wa Wayahudi dhidi ya Lebanon na watu wake, na kukabiliana na udhihirisho wowote wa kurejesha uhusiano wa kawaida au kujisalimisha kwa mradi wa Amerika.
Na tunaitaka mamlaka kusitisha uonevu huu juu ya kusema ukweli na maoni ya kisiasa, na tunaitaka mara moja na haraka kuwaachilia ndugu Hassan Abdel Hadi na Salah Dawood bila kuchelewa au kukawia, kwani Hizb ut-Tahrir inajulikana ni nani, na njia yake katika kazi na mapambano ya kisiasa kwa neno na hoja inajulikana, na hakuna uhalali wowote kwa mamlaka kuwakamata isipokuwa kuendelea kwa mbinu ya mfumo huo wa usalama licha ya mabadiliko ya baadhi ya nyuso, bila kubadilisha vitendo na tabia!
Na Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Lebanon, ambayo inawakilisha kundi la Waislamu, haitakubali kuwa kitoweo rahisi na mahali pa unyanyasaji wa vyombo vya usalama, ambavyo vinapuuza wale wanaotishia usalama wa Lebanon na watu wake kwa mantiki ya nguvu za kimwili, kisha wanakuja kuwadhulumu wale wanaoinua sauti zao kwa neno, hoja na kazi ya kisiasa.
﴿Hakika wale walio watesa Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi hao watapata adhabu ya Jahannamu, na watapata adhabu ya kuungua.﴾
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Lebanon