Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utambuzi wa Masharti wa Australia kwa Palestina
ni Zawadi kwa Shirika la Kiyahudi kwa Mauaji ya Kimbari, na Sio Ushindi kwa Aliyeonewa
Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ametangaza rasmi utayari wa Australia kutambua taifa la Palestina. Amewasiliana kibinafsi na Mahmoud Abbas na Benjamin Netanyahu mapema, kana kwamba anataka kuwatuliza wahalifu wanaohusika na miongo kadhaa ya uhalifu kabla ya kufanya uamuzi.
Hivi majuzi Albanese alisema kwamba utambuzi wa taifa la Palestina unategemea Palestina kuitambua mamlaka ya uvamizi, na kukubali mipaka ya kudumu, na kupokonya silaha taifa la Palestina la siku zijazo, na kuondoa Hamas na juhudi zote za upinzani inazowakilisha kabisa.
Pendekezo la serikali ya Australia si zaidi ya zawadi kwa shirika la Kiyahudi kwa mauaji ya kimbari, ni kutoa taifa bandia lisilo na maana, lililonyimwa uwezo wa kujitetea, lililolazimishwa kukabidhi ardhi yake iliyokaliwa, na kuwekewa usimamizi wa madola ya Magharibi katika kuamua nani analitawala, na kulazimishwa kuanzisha uhusiano wa kawaida na shirika la uhalifu katili.
Haya si masharti ya haki, bali ni malengo yale yale ambayo shirika la Kiyahudi na Marekani yanayoyafuatilia baada ya takriban miaka miwili ya mauaji ya kimbari. Australia inajaribu tu kusaidia kusukuma kusalimu amri kidiplomasia baada ya mamlaka ya uvamizi kushindwa kuifikia kijeshi, ikitumaini kwamba udanganyifu wa taifa la Palestina utafaulu kuwa karoti baada ya kutumia fimbo ya mauaji ya kimbari.
Cha kushangaza ni kwamba Australia imetangaza nia yake ya kulitambua taifa la Palestina, lakini inashindwa kuwatambua Wapalestina wenyewe. Sera ya serikali iliyopo ya kuwanyima ubinadamu na kulaumu mwathiriwa imefanya mateso ya Wapalestina kutokuonekana, na uhalifu wa mamlaka ya uvamizi bila kuwajibishwa. Australia haikutafuta kuitambua Palestina hadi Wapalestina wengi walipouawa au kufurushwa, wakati hakuna kilichobaki cha kutambuliwa.
Ulimwengu una hofu ya kweli, kwamba mamlaka ya uvamizi sasa imesimama kwenye kizingiti cha kutekeleza "Suluhisho la Mwisho" huko Palestina. Ama Australia, inafanya juhudi kubwa kujifanya haina hatia ya kuhusika kwake katika uhalifu, lakini kwa kufanya hivyo, inathibitisha tu hukumu yake. Muungano wa Kizayuni-Magharibi umefichuliwa kwa ulimwengu, na hakuna hotuba au ishara za mfano zitakazoweza kuficha ukweli wake mbaya.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir huko Australia