
5/8/2025
Abu Wadaha News: Uhusiano na nchi za kigeni ni wa serikali pekee, kwa sababu ni yenyewe pekee ina haki ya kusimamia masuala ya umma kivitendo
Taarifa kwa vyombo vya habari
Uhusiano na nchi za kigeni ni wa serikali pekee, kwa sababu ni yenyewe pekee ina haki ya kusimamia masuala ya umma kivitendo
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti habari kwamba ujumbe kutoka muungano wa vyama na harakati za mashariki mwa Sudan, ukiongozwa na Shiba Darar, na kuambatana na ujumbe kutoka kwa wazee, ulikutana na Rais wa Eritrea, Asias Afwerki, siku ya Jumamosi 2/8/2025 katika ofisi yake "Baada ya Hallo", ambapo ujumbe huo ulijadili naye hali ya sasa nchini Sudan kwa ujumla, huku wakizingatia changamoto zinazoikabili mkoa wa mashariki mwa Sudan. Ujumbe huo pia ulisisitiza umuhimu wa uratibu na nchi jirani kuunga mkono utulivu wa nchi na kukabiliana na mizozo ya kisiasa na kiusalama.
Je, udhaifu na unyonge wa serikali ya Sudan umefikia kiwango hiki, au inatafuta kuwafuga watu ili wakubali picha hizi zilizopotoshwa, kwa haja iliyo ndani yake; picha hizi ambazo zinajumuisha mafunzo ya wanamgambo wenye uaminifu wa kikanda, au kikabila huko Eritrea?!
Hakika machafuko haya ambayo yanadhaminiwa na serikali ya Sudan, kisiasa na kijeshi, na ikiwa ni pamoja na kuinua matamshi ya kibaguzi katika duru za kisiasa, yote hayo yanahudumia mpango wa Marekani wa kuigawanya Sudan katika majimbo kadhaa madogo; Darfur, kisha Sudan Mashariki!!
Serikali ya Sudan inapaswa kujiepusha, na kusitisha mchezo huu wa kucheza na moto, ambao utakuja kuharibu umoja wa kile kilichosalia cha nchi na kuiacha kama kumbukumbu iliyopita, na huo ni uhaini mkubwa. Simamisheni vitendo hivi vya kisiasa vinavyolenga umoja wa nchi, simamisheni mfululizo wa utengenezaji wa wanamgambo wa ndani au wanaohusishwa na mafunzo na nchi za kigeni.
Ama suala la raia wa dola ya Kiislamu; wao wana nini, na wanadaiwa nini, na uhusiano wao na nchi za kigeni, ni suala la kisheria, na Uislamu Mkuu una maelezo wazi ndani yake; kwani haijuzu kwa raia kufanya kazi ya mtawala, si ndani wala nje isipokuwa kwa uteuzi halali, kama vile Khalifa wa Waislamu, kwa sababu yeye ndiye anayehusika na kutunza masuala ndani na nje, kwa kauli yake ﷺ: «...Basi imamu aliye juu ya watu ni mchungaji naye ataulizwa kuhusu kundi lake», au kwa yule ambaye Khalifa amemteua, miongoni mwa wasaidizi na magavana na wengineo.
Basi dola ya Khilafa Rashidah itakaposimama karibuni kwa idhini ya Mungu, wakati huo hairuhusiwi mtu yeyote kukutana na wakuu wa nchi za kigeni, au kuwa na uhusiano na nchi ya kigeni. Imekuja katika rasimu ya katiba ya dola ya Khilafa ambayo chama cha Ukombozi kimewasilisha kwa umma, ibara ya (182): (Haijuzu kwa mtu yeyote, au chama, au kundi, au kikundi kuwa na uhusiano wowote na nchi yoyote kati ya nchi za kigeni kabisa, na uhusiano na nchi ni wa serikali pekee, kwa sababu ni yenyewe pekee ina haki ya kusimamia masuala ya umma kivitendo, na umma na makundi lazima kuiwajibisha serikali kwa uhusiano huu wa nje).
Enyi watu wa Sudan, je, tunachowaitia kwacho ni bora au hali hii mbaya mnayoishi?!
Je, haijawadia kwenu kufanya kazi na chama cha Ukombozi; kiongozi ambaye hawadanganyi, kuanzisha Khilafa Rashidah ya pili juu ya mfumo wa unabii? Ni yenyewe pekee inahifadhi muundo wa dola, na kuifanya iwe na heshima, kwa hivyo hairuhusu nchi nyingine yoyote kuingilia mambo yake, au kufungua njia za mawasiliano na raia wake, kwani yote hayo ni uhalifu mkubwa na hatari kwa muundo wake.
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye jambo lile ambalo linakuhuisheni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika mtakusanywa kwake﴾.
Jumatatu 10 Safar 1447 Hijria
04/08/2025 Miladia
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa chama cha Ukombozi
katika jimbo la Sudan
Chanzo: Abu Wadaha News
