
29/7/2025
Abu Wadaha News: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan Yaandaa Mkutano Kuhusu Ulazima wa Kuwasaidia Watu wa Gaza Katika Soko Kuu la Port Sudan
*Mkutano Kuhusu Ulazima wa Kuwasaidia Watu wa Gaza Katika Soko Kuu la Port Sudan*
Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan, iliandaa mkutano wa kisiasa katika jiji la Port Sudan, Jumatatu hii, 03 Safar 1447 Hijria, inayolingana na 2025/07/28 Miladia, mkutano wa kisiasa wenye kichwa: (Ulazima wa Kuwasaidia Watu wa Gaza).
Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan, Ustadhi Muhammad Jami Abu Ayman, alihutubia umati wa waliohudhuria katika uwanja wa Hoteli ya Haramain huko Port Sudan, ambapo alianza hotuba yake kwa kuwakumbusha Waislamu kuhusu udugu wa Kiislamu, na ulazima wa kuwasaidia Waislamu popote walipo, na pia aliwakumbusha kuhusu safari ya usiku ya Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم, na kwamba yeye pia ni mateka katika mikono ya Mayahudi ndugu wa nyani na nguruwe, na akaeleza msimamo wa watawala, na akawaelezea kama wasaidizi wa Mayahudi katika kutekeleza uhalifu huu dhidi ya Waislamu wa Gaza.
Kisha akawalingania waliohudhuria, na akawahimiza kuishinikiza jeshi, na kuondoa vizuizi vinavyowazuia, ili watekeleze wajibu wao wa kuwasaidia ndugu zao huko Gaza, na katika nchi zote za Waislamu zilizokumbwa na majanga, akitoa ushahidi kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {NA WAKIKUOMBENI MSAADA KATIKA DINI, BASI NI JUU YENU KUWASAIDIA, ISIPOKUWA JUU YA WATU AMBAO KATI YENU NA WAO IPO AHADI ۗ NA MWENYEZI MUNGU ANAYAAJUA VYEMA MYATENDAYO} [Al-Anfal : 72]. Na alieleza kuwa kitendo hiki kimeamuliwa na Uislamu kwa Khalifa wa Waislamu, anayewaongoza kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na anapigana kutoka nyuma yake.. Mmoja wa waliohudhuria alikatisha kwa mshangao akidai Khalifa kama Abu Bakr As-Siddiq.. anayeendesha jeshi, na anajua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wake .. na alimkumbatia mzungumzaji huku akilia na akitukuza mbele ya waliohudhuria na kumwambia Abu Ayman tunakupenda kwa sababu unasema ukweli .. na anasema tunapenda na tunataka dini hadi wote waliohudhuria waliguswa.
Abu Ayman alihimiza mzungumzaji kuwahudhurisha kufanya kazi ya kuondoa viti hivi vya enzi na kusimamisha Khilafah, na kwamba kuna ahadi kutoka kwa Mola Mtukufu ya kuwasaidia wale wanaomsaidia. Amesema: {ALLAH AMEWA AHIDI WALIO AMINI MIONGONI MWENU NA WAMETENDA MEMA ATAWAFANYA MAHALI PAO KATIKA ARDHI, KAMA ALIVYO FANYA MAHALI PAO WALIO KUWA KABLA YAO ..} [An-Nur : 55] Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Abu Wadaha News
