
2025-09-08
Abu Wadaha News: Ripoti ya Habari Kuhusu Kongamano la Masuala ya Umma la Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan
Kongamano la masuala ya Umma la kila mwezi lenye kichwa: (Mpango wa Marekani wa Kuikata Darfur na Jinsi ya Kuufelisha) lilifanyika leo Jumamosi, 14 Rabi' al-Awwal 1447 Hijria, sawa na 06/09/2025 Miladia, katika ofisi ya Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan katika mji wa Port Sudan.
Katika karatasi ya kwanza iliyokuwa na kichwa: (Mzozo huko Darfur na mipango ya kafiri mkoloni ya kuitenganisha), Ustadh Naser Reda - mkuu wa kamati ya mawasiliano mkuu ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan, alianza mazungumzo yake na historia kuhusu Darfur, kama ufalme wa zamani, uliokuwa ukiitwa Ufalme wa Darfur, na kuangazia masultani wake, Sultani Ali Dinar, kama vile alivyoeleza jinsi Waingereza waliokuwa wakikoloni Sudan walivyopanda mbegu za fitna na mzozo huko Darfur, kwa kuanzisha mfumo wa utawala wa kiasili, na kuwapa baadhi ya makabila ardhi iliyoitwa Hawakir. Kisha alizungumza jinsi mzozo ulianza huko Darfur, na jinsi harakati za uasi zilivyotengenezwa, na pia aligusia mpango wa Marekani wa kuipasua Sudan, ambao ilianza nao Kusini mwa Sudan, na jinsi inavyotaka sasa kuitenganisha Darfur.
Kisha Ustadh Naser akauliza swali, je, kujitenga ndio suluhisho la matatizo ya Darfur kama wengine wanavyodai?! Akajibu kwamba kujitenga kunatengeneza taasisi mbili dhaifu, na pia kuna migogoro zaidi kama ilivyotokea wakati Kusini mwa Sudan ilipojitenga. Kisha alihitimisha hotuba yake na pointi kumi za kufelisha mpango wa kuitenganisha Darfur, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kuvunja mzingiro wa mji wa El Fasher, kufuta mfumo wa utawala wa kiasili, mfumo wa Hawakir, kuunganisha harakati za silaha katika jeshi, kueneza ufahamu kwa misingi ya Uislamu na pointi nyinginezo.
Katika karatasi ya pili iliyokuwa na kichwa: (Enyi watu wa Sudan, je, tuna uwezo wa kufelisha mpango wa kuitenganisha Darfur?) Ustadh Muhammad Jami' Abu Ayman alieleza mwanzoni mwa hotuba yake kwamba watu wengi wanashughulika kwa kutojali, ingawa suala hilo ni hatari, na linahitaji umakini katika kazi, akieleza kwamba muumini hakati tamaa, na kwamba tuna uwezo wa kufelisha mpango huu ikiwa tutaweka uongofu wa Mwenyezi Mungu mbele ya macho yetu, akitoa ushahidi wa idadi ya aya tukufu kutoka katika Qur'ani Tukufu, na pia alitoa mifano ya kazi ya Mitume, kazi ya Salaf Salihi, na hata msimamo wa Abdul Hamid II, Khalifa wa Uthmaniyya, na kukataa kwake mamilioni ya lira za dhahabu ili Wayahudi wasikae Palestina, kisha akawahutubia ndugu wanahabari kwamba wasitoe kukata tamaa miongoni mwa watu, bali jukumu lao ni kueneza matumaini, na wajitahidi kufichua mpango huo na kuufelisha. Kisha alihitimisha kwamba suluhisho la msingi ni kuanzisha Khilafah Rashidah kwa manhaj ya Utume ambayo itasimamisha mipango ya makafiri wakoloni.
Katika kipindi cha mwingiliano, jukwaa lilijibu maswali ya waliohudhuria, kisha afisa wa jukwaa, Ustadh Ibrahim Musharraf - mwanachama wa ofisi ya habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan, alihitimisha kongamano hilo, akiwashukuru waliohudhuria, na wafuatiliaji wa matangazo ya moja kwa moja kwa ufuatiliaji na ushiriki wao mzuri.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
المصدر: Abu Wadaha News

