Organization Logo

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707

spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Uhusiano na Mataifa ya Kigeni Umewekwa kwa Dola Peke Yake, kwa sababu Ina Haki ya Kutunza Mambo ya Umma
Press Release

Uhusiano na Mataifa ya Kigeni Umewekwa kwa Dola Peke Yake, kwa sababu Ina Haki ya Kutunza Mambo ya Umma

August 05, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhusiano na Mataifa ya Kigeni Umewekwa kwa Dola Peke Yake, kwa sababu Ina Haki ya Kutunza Mambo ya Umma

Vyombo vya habari vingine vimeripoti habari kwamba ujumbe kutoka muungano wa vyama na harakati za mashariki mwa Sudan, ukiongozwa na Sheiba Dharar, na kuandamana na ujumbe kutoka kwa wazee, walikutana na Rais wa Eritrea Asias Afwerki Jumamosi, Agosti 2, 2025 katika ofisi yake "Badi Hallou" ambapo ujumbe ulijadili naye hali ya sasa nchini Sudan kwa ujumla, kwa kuzingatia changamoto zinazoikabili mkoa wa mashariki mwa Sudan. Ujumbe huo pia ulisisitiza umuhimu wa uratibu na nchi jirani ili kusaidia utulivu wa nchi na kukabiliana na migogoro ya kisiasa na kiusalama.

Je, udhaifu na unyonge wa serikali ya Sudan umefikia kiwango hiki, au inatafuta kuwafanya watu wakubali picha hizi zilizopotoshwa, kwa haja ndani yake; picha hizi ambazo zinajumuisha mafunzo ya wanamgambo waaminifu kwa ukabila, au kikabila huko Eritrea?!

Machafuko haya ambayo yanadumishwa na serikali ya Sudan, kisiasa na kijeshi, na ambayo yanajumuisha kukuza hotuba za kibaguzi katika duru za kisiasa, yote hayo yanahudumia mpango wa Amerika wa kuigawa Sudan katika majimbo kadhaa madogo; Darfur, kisha mashariki mwa Sudan!!

Serikali ya Sudan inapaswa kuacha, na kusimamisha mchezo huu wa moto, ambao utaangamiza umoja wa kile kilichosalia cha nchi na kuiacha kuwa kumbukumbu, na hiyo ni uhaini mkuu. Simamisheni vitendo hivi vya kisiasa ambavyo vinakusudia umoja wa nchi, simamisheni mfululizo wa utengenezaji wa wanamgambo wa ndani au wanaohusishwa na mafunzo na nchi za kigeni.

Ama suala la raia wa Dola ya Kiislamu; wanachokipata na wanachopoteza, na uhusiano wao na nchi za kigeni, ni suala la kisheria, na Uislamu Mkuu una ufafanuzi wazi ndani yake; kwa kuwa hairuhusiwi kwa raia kufanya kazi ya mtawala, si ndani wala nje isipokuwa kwa uteuzi halali, kama vile Khalifa wa Waislamu, kwa sababu yeye ndiye anayehusika na kutunza masuala ya ndani na nje, kwa kauli yake ﷺ: «...basi Imamu aliye juu ya watu ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake», au kwa yule aliyeteuliwa na Khalifa, kutoka kwa wasaidizi, magavana na wengineo.

Dola ya Khilafa iliyoongoka itakapoundwa hivi karibuni, kwa idhini ya Mungu, basi hakuna mtu atakayeruhusiwa kukutana na wakuu wa nchi za kigeni, au kuwa na uhusiano na nchi ya kigeni. Ilikuja katika rasimu ya katiba ya dola ya Khilafa iliyowasilishwa na Hizb ut-Tahrir kwa umma, kifungu (182): (Hairuhusiwi kwa mtu yeyote, au chama, au kundi, au kikundi kuwa na uhusiano wowote na nchi yoyote ya kigeni kabisa, na uhusiano na nchi hizo umewekwa kwa dola peke yake, kwa sababu ina haki ya kutunza mambo ya umma kwa vitendo, na ni juu ya umma na makundi kuiwajibisha dola kwa uhusiano huu wa nje).

Enyi watu wa Sudan, je, tunayowaitia ni bora au hali hii mbaya mliyonayo?!

Je, haijafika wakati kwenu kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir; kiongozi ambaye hawaambii uongo, kuanzisha Khilafa iliyoongoka ya pili kwa mfumo wa Utume? Ni yenyewe tu ndiyo inayohifadhi taasisi ya dola, na kuifanya iwe na heshima, ili isiruhusu nchi nyingine yoyote kuingilia mambo yake, au kufungua njia za mawasiliano na raia wake, kwa kuwa yote hayo ni uhalifu mkuu na hatari kwa taasisi yake.

﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye litakalo kuuhisheni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba kwake Yeye mtakusanywa

Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir

Katika Jimbo la Sudan

Official Statement

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

السودان - مكتب - ناطق

Media Contact

السودان - مكتب - ناطق

Phone: 0912240143- 0912377707

Email: spokman_sd@dbzmail.com

السودان - مكتب - ناطق

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707 | spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Reference: PR-01987227-1260-7ad6-ba00-3c28aaaf05f5