Organization Logo

أفغانستان المكتب

ولاية أفغانستان

Tel:

hizbuttahrir.af@gmail.com

Mapigano ya Hivi Karibuni Kati ya Afghanistan na Pakistan Yanahudumia Sera za Kikanda za Marekani na India
Press Release

Mapigano ya Hivi Karibuni Kati ya Afghanistan na Pakistan Yanahudumia Sera za Kikanda za Marekani na India

October 13, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mapigano ya Hivi Karibuni Kati ya Afghanistan na Pakistan

Yanahudumia Sera za Kikanda za Marekani na India

(Imetafsiriwa)

Usiku wa Jumamosi, majeshi ya Afghanistan na Pakistan yalizozana katika mapigano ya mpakani, huku kila upande ukishambulia maeneo ya mwenzake kwenye mstari wa Durand; kama matokeo, pande zote mbili za Waislamu zilipata hasara za kibinadamu. Siku mbili kabla ya hapo, jeshi la Pakistani lilishambulia maeneo fulani katika miji ya Kabul na Paktika, na kusababisha hasara za kibinadamu.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir Wilayah Afghanistan ililaani vita hivi vinavyoendelea kati ya nchi hizi mbili za Kiislamu, na kuona kuwa ni huduma kwa sera za kikanda za Marekani na India, na ni madhara kwa Waislamu. Mzozo huu unaonyesha tena jinsi mipaka bandia na sera zisizo za Kiislamu zimewachochea Waislamu dhidi ya wao kwa wao, huku maadui wa kweli wa Umma wakiangalia hali hiyo kutoka mahali salama kabisa.

Inasikitisha sana kwamba jeshi la Pakistani - ambalo linajiona kuwa jeshi lenye nguvu zaidi katika nchi za Kiislamu - linatumia nguvu na silaha zake si dhidi ya maadui wa Uislamu, bali dhidi ya ndugu zake Waislamu! Jeshi hili hilo, ambalo bila aibu liliikabidhi Kashmir kwa India, na likanyamaza kimya mbele ya sera za serikali ya Modi ya Kihindi ya kitaifa ya kupinga Uislamu na hatua zake za ukandamizaji, sasa linashambulia miji na vijiji katika Afghanistan na maeneo ya kikabila kwa ujasiri mkubwa, kiasi kwamba kama ujasiri na azma hii ingeonyeshwa dhidi ya India na dola ya Kiyahudi, Kashmir isingekuwa imefedheheshwa, na Gaza isingevumilia miaka miwili ya mauaji ya halaiki, na isingelazimishwa leo suluhu ya amani ya aibu kwa watu wa Gaza chini ya shinikizo na usaliti wa watawala wa Kiislamu, wakiwemo watawala wa Pakistan.

Tunajua kwamba mtindo huu wa uadui kwa Waislamu na kunyamaza mbele ya ukafiri ni kazi ya mduara maalum wa mamluki ndani ya jeshi la Pakistani, na kwamba ujasiri huu unatokana na ukaribu wa muda mfupi kati ya uongozi wa Pakistan na bwana wao, Donald Trump. Ukaribu huu umelipa jeshi la Pakistani udanganyifu na ujasiri wa kufanya mashambulizi nchini Afghanistan, na Amerika imeliwekea jukumu la kuwafanya Waislamu katika maeneo ya kikabila na kwenye mstari wa Durand wawe na shughuli na wanamgambo wa Afghanistan.

Kama ilivyotokea hivi karibuni, na kama adhabu ya muda kwa India, Amerika inajifanya tena kuwa Pakistan ni mshirika muhimu; ambapo uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistani unajishughulisha na kusafiri, kupiga picha na kuwavutia maafisa wa Marekani. Hata hivyo, upepo unapobadilika, Pakistan inasukumwa tena kwenye kona ya kusahaulika. Kama alivyokiri Khawaja Muhammad Asif, waziri wa ulinzi wa Pakistani, wakati mmoja: "Tumekuwa tukifanya kazi hii chafu kwa ajili ya Amerika kwa takriban miongo mitatu... na Magharibi, ikiwa ni pamoja na Uingereza. Ilikuwa ni kosa na tuliteseka kwa sababu yake."

Kukiri huku kunaonyesha kwamba miongo kadhaa ya sera ya Pakistan imehudumia maslahi ya Marekani na imeweka gharama kubwa kwa Waislamu wa eneo hilo. Matukio ya hivi karibuni pia yanaonyesha kwamba Pakistan haijajifunza kutokana na historia, na kwamba inarudia kujipendekeza kwa Marekani ili kurudi kwenye jukumu lake katika eneo hilo. Ukweli ni kwamba Amerika haimkumbuki Pakistan isipokuwa inapofika kwenye mkwamo katika sera zake kuhusu Afghanistan au India au China. Ndipo, Pakistan ghafla inakuwa "mshirika wa kimkakati" na jukumu lake la muda linaanzishwa! Lakini mara tu kazi inapokamilika na sera ya Marekani katika eneo hilo inarudi kwenye mkondo wake wa kawaida, Pakistan inatengwa tena; ahadi zote hizo na tabasamu za kidiplomasia - kama ilivyo wazi katika utawala wa Biden - ni vinyago vya muda tu.

Ujumbe wetu kwa wanamgambo wa Afghanistan na kwa waaminifu katika jeshi la Pakistani ni: badala ya kuwachinja Waislamu na kupigana, angalia picha kubwa. Hivi sasa, matumaini ya Waislamu duniani kote - hasa Kusini mwa Asia - yanategemea uwezo wa kijeshi wa wanamgambo wa Afghanistan na maafisa waaminifu katika jeshi la Pakistani ambao wanaweka Uislamu na ahadi ya Pepo juu ya cheo na nafasi za kidunia. Vikosi hivi vina uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa: kwa kuondoa mipaka bandia ya kikoloni na kuanzisha Khilafah Rashidah, wanaweza kuunganisha uwezo wa Umma katika eneo lote na kuibuka kama nguzo huru ya kisiasa na kijeshi katika ulimwengu. Kwa kweli, Khilafah itazuia mipango ya kikoloni ya Amerika, India na China katika eneo hilo, na kuhamasisha jeshi kukomboa nchi za Kiislamu zinazokaliwa kama vile Kashmir, Turkestan Mashariki na Palestina.

﴿Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaanza kufeli, na ikaondoka nguvu yenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Wilayah Afghanistan

Official Statement

أفغانستان المكتب

ولاية أفغانستان

أفغانستان المكتب

Media Contact

أفغانستان المكتب

Phone:

Email: hizbuttahrir.af@gmail.com

أفغانستان المكتب

Tel: | hizbuttahrir.af@gmail.com

Reference: PR-0199dc97-30c0-7079-a7df-f0ce7fed8ff2