Organization Logo

الدنمارك مكتب

الدنمارك

Tel:

info@hizb-ut-tahrir.dk

http://www.hizb-ut-tahrir.dk/

Uchunguzi wa Awali wa Kidemokrasia na Upotoshaji wa Picha ya Waislamu
Press Release

Uchunguzi wa Awali wa Kidemokrasia na Upotoshaji wa Picha ya Waislamu

October 25, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uchunguzi wa Awali wa Kidemokrasia na Upotoshaji wa Picha ya Waislamu

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 22 Oktoba 2025, vyombo kadhaa vya habari viliripoti kwamba Kamati ya Uhamiaji na Uraia katika Bunge la Denmark ilikataa kumpa uraia mwanamume Muislamu kwa sababu ya maadili yake ya Kiislamu, na licha ya yeye kutimiza masharti yote magumu ya uraia wa Denmark, wengi wa wajumbe wa kamati waliamua kwamba "kutetea maadili ambayo yanapingana kabisa na maadili yetu, kunapingana na uraia wa Denmark". Ama Wanademokrasia wa Kijamii, ambao kama kawaida yao hutumia mazingira ya chuki dhidi ya Uislamu kujaribu kupunguza makali ya kushindwa kwao kuepukika na karibu kwa uchaguzi, walitumia ukurasa wao rasmi wa Facebook kumlenga mwanamume huyu Muislamu wakidai kwamba "anachukia maadili ya Denmark na nchi yetu".

Uamuzi huu ni mfano mwingine wazi kwamba Waislamu katika nchi hii wanatakiwa kuwa na masharti maalum - sio tu kufuata sheria kama watu wengine - lakini pia kujisalimisha kwa demokrasia ya kiliberali ya kilimwengu iliyoshindwa na kuachana na maadili yao ya Kiislamu. Hata hivyo, jambo hilo halizuiliwi tu kwa masharti haya maalum; serikali inazidi kuendeleza wito wake wa kiubaguzi kwa mnyama aliyefichika ambaye wanasiasa wa bunge wametumia miongo kadhaa kumkuza miongoni mwa makundi ya jamii, ambapo hofu na chuki inayotokana na ujinga imekuwa sababu muhimu katika tabia ya uchaguzi. Hivyo, wanampiga picha Muislamu anayejitolea na anayetambua maadili kama tishio kwa jamii, na maadili yake ni hatari, ya kuchukiza na ya uharibifu.

Wanasiasa wanabainisha hasa kwamba Muislamu husika anatetea Sharia ya Kiislamu, ambayo ni neno pana kwa hukumu za Uislamu na kanuni za maisha, jambo ambalo kila Muislamu analiunga mkono. Hili si kosa, bali ni adhabu inayotokana tu na kujitolea kwa Muislamu kwa Qur'ani na Sunna za Nabii Muhammad ﷺ.

Nini kinafuata? Ni katika maeneo gani mengine ambayo mahakama za kidunia za upelelezi, kwa uamuzi huu kama mfano, zinatarajiwa kuwahoji na kuwaadhibu Waislamu ambao hawajafanya kitendo chochote cha uhalifu?

Demokrasia ya kiliberali inapitia mgogoro mbaya wa maadili. Bunge kwa ujumla, na serikali inayoongozwa na Wanademokrasia wa Kijamii hasa, zimepoteza uaminifu wao kwa muda mrefu. Wamepoteza kila kitu, na wameshindwa kubadilisha mambo kwa sera zilizoshindwa na ahadi tupu. Watu wanatambua kwamba mfumo kimsingi unatumikia maslahi ya wasomi wa kiuchumi ndani ya nchi, huku mkondo wa Denmark katika masuala ya kimataifa mara nyingi unaamuliwa na mwelekeo ambao Marekani inataka.

Wanademokrasia wa Kijamii na Kamati ya Uhamiaji na Uraia ya Bunge hawana uhalali wowote wa kuchochea matatizo au kuwaadhibu Waislamu kwa utetezi wao wa asili wa Sharia ya Kiislamu. Hawako katika nafasi ya kuwahubiria Waislamu kuhusu maadili baada ya miaka miwili ya mauaji ya kimbari huko Palestina yaliyofanywa kwa kutumia vipengele vya silaha za Denmark dhidi ya watu raia Waislamu. Maadili ya Kiislamu ni ya juu zaidi kuliko maadili haya ya mauaji ya kimbari yanayopinga ubinadamu, na kinyume na maadili ya kilimwengu na kiliberali, maadili ya Kiislamu yanategemea ushahidi wa nguvu na msingi imara ambao unashinda changamoto zote. Kinachohatarisha ulimwengu na jamii nchini Denmark si Waislamu wanaoshikilia maadili ya Uislamu, bali ni wanasiasa wa kitaalamu wasio na ubinadamu na wachochezi wa chuki ambao wameruhusiwa kuongoza nchi kwa maadili yao yaliyoharibika.

Elias Lamrabet

Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut-Tahrir nchini Denmark

Official Statement

الدنمارك مكتب

الدنمارك

الدنمارك مكتب

Media Contact

الدنمارك مكتب

Phone:

Email: info@hizb-ut-tahrir.dk

الدنمارك مكتب

Tel: | info@hizb-ut-tahrir.dk

http://www.hizb-ut-tahrir.dk/

Reference: PR-019a1129-1380-77f9-84f0-a7dfd253a8e2