Taarifa za Habari 2025/07/14
Mada Kuu:
- · Onyo la Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka kwa ukali wa njaa huko Gaza
- · Ahmed Al-Shara'a anahudhuria mikutano na maafisa kutoka taasisi ya Kiyahudi huko Azerbaijan
- · Abbas: Kuondoka kwa uvamizi ni sharti la amani ya Gaza na Hamas haitatawala Ukanda
Maelezo:
Onyo la Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka kwa ukali wa njaa huko Gaza
Mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza yameacha takriban watu 195,000 kati ya waliouawa na waliojeruhiwa, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, na zaidi ya watu 10,000 hawajulikani walipo, pamoja na mamia ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao na njaa ambayo imepoteza maisha ya wengi, wakiwemo watoto kadhaa. Tangu Oktoba 7, 2023 hadi leo, Wayahudi wamekuwa wakifanya mauaji mabaya zaidi na vitendo vya mauaji ya kimbari mbele ya macho na masikio ya watawala wasaliti wa Waislamu. Ama nchi zenye majeshi makubwa kwenye mipaka ya Palestina na karibu nayo, bado zinaendelea na ukimya kamili. Ukimya huu wa aibu ndio unaowapa ujasiri Wayahudi na kuwasukuma kuendelea na uovu wao. Jukumu la watawala hawa ni la mtazamaji anayehesabu mashahidi, wakati majeshi yao ambayo yamemwagiwa mamilioni ya pesa ni chombo laini katika huduma ya kafiri mkoloni! Lau majeshi haya yangefanya harakati, yangewaangamiza Wayahudi kwa saa moja, na yangelikomboa ardhi iliyobarikiwa, na kuirejesha kwenye mikono ya umma wa Kiislamu.
----------
Ahmed Al-Shara'a anahudhuria mikutano na maafisa kutoka taasisi ya Kiyahudi huko Azerbaijan
Tovuti ya Kiyahudi "i24NEWS" ilifichua kuwa Rais wa Syria Ahmed Al-Shara'a atahudhuria mkutano mmoja angalau, Jumapili na maafisa kutoka taasisi ya Kiyahudi huko Azerbaijan, licha ya vyanzo huko Damascus kukanusha. Chanzo kililiambia tovuti hiyo kwamba mkutano huo unaotarajiwa unakuja kama sehemu ya mfululizo wa mikutano miwili au mitatu kati ya pande hizo mbili, ikihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad Al-Shaibani, pamoja na Ahmed Al-Dalati, mratibu wa serikali ya Syria katika mikutano ya kiusalama na taasisi ya Kiyahudi. Ujumbe wa ngazi ya juu wa Kiyahudi unajumuisha mjumbe maalum wa Waziri Mkuu Netanyahu, pamoja na watu wa usalama na kijeshi. Tovuti hiyo ilisema kuwa mikutano hiyo inalenga kujadili maelezo ya ziada kuhusu makubaliano ya kiusalama yaliyopangwa kutiwa saini kati ya taasisi ya Kiyahudi na Syria, tishio la Iran nchini Syria na Lebanoni, silaha za Hezbollah ya Iran, silaha za makundi ya Kipalestina, kambi za Kipalestina huko Lebanoni, na mustakabali wa wakimbizi wa Kipalestina kutoka Gaza katika eneo hilo.
Aibu kwa hali hii ambayo mtu anayedai kuwa anafanya jihadi amefikia, badala ya kutangaza jihadi tangu wakati wa kwanza alipofika madarakani dhidi ya taasisi ya Kiyahudi ambayo inakalia ardhi yake na ardhi ya Palestina iliyobarikiwa, anatafuta kuanzisha uhusiano wa kawaida na taasisi hii vamizi. Lau angetangaza jihadi dhidi ya taasisi ya Kiyahudi baada ya kumuondoa Bashar madarakani mara moja na kabla ya mwangaza wa ushindi kupoa, angepata uungwaji mkono wa Waislamu wote na wangefurika katika makundi kwa ajili ya jihadi pamoja naye.
-----------
Abbas: Kuondoka kwa uvamizi ni sharti la amani ya Gaza na Hamas haitatawala Ukanda
Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, alisema kuwa "suluhisho pekee linalowezekana huko Gaza ni kuondoka kamili kwa uvamizi na kuiwezesha dola ya Palestina kuchukua majukumu yake katika Ukanda, kwa msaada wa Kiarabu na kimataifa madhubuti." Kulingana na shirika rasmi la habari la Palestina (Wafa), Abbas aliongeza, wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, katika makazi yake huko Amman, kwamba Hamas haitatawala Ukanda. Wakati wa mkutano huo, alijadili na Blair kile kilichoelezewa kama "maendeleo ya hivi karibuni katika ardhi ya Palestina, na maendeleo ya kisiasa na kibinadamu yanayoendelea", huku akisisitiza "ulazima wa kufikia usitishaji mapigano wa haraka, kuachiliwa kwa mateka wote (Waisraeli) na wafungwa wa Kipalestina, na kuhakikisha kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu ya haraka katika Ukanda wa Gaza bila vizuizi."
Msaliti kama Abbas hana nia ya kukomboa ardhi, bali anatosheka na jimbo dhaifu kwenye kipande kidogo cha ardhi. Ukweli kwamba sehemu kubwa ya Palestina inakaliwa haimuhusu kwa chochote. Yeye na watu kama yeye hawana nia ya kukomboa Palestina, lakini wana nia ya kuhalalisha uvamizi na kulazimisha kukubalika kwake kwa umma. Je, huu si ndio lengo la kuanzishwa kwa Shirika la Ukombozi la Palestina? Shirika hilo ni chombo kilichoanzishwa chini ya usimamizi wa wakoloni wa Magharibi ili kuondoa suala la Palestina kutoka kuwa suala la umma na kulifanya suala la ndani la Palestina, na kuhalalisha uvamizi wa Palestina.

