Habari Muhimu 2025/10/13
October 13, 2025

Habari Muhimu 2025/10/13

Habari Muhimu 2025/10/13

Mada kuu:

  • ·       Nchi 6 za Kiarabu zimeongeza ushirikiano wa kijeshi kwa siri na taasisi ya Kiyahudi wakati wa vita vyake dhidi ya Gaza
  • ·       Mkutano wa Sharm el-Sheikh: Misri kuwa mwenyeji wa viongozi wa dunia kumaliza vita vya Gaza
  • ·       Afghanistan inazishutumu kundi fulani huko Pakistan kwa kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili

Maelezo:

Nchi 6 za Kiarabu zimeongeza ushirikiano wa kijeshi kwa siri na taasisi ya Kiyahudi wakati wa vita vyake dhidi ya Gaza

Gazeti la Washington Post lilibaini kuwa nchi sita za Kiarabu ambazo ni (Jordan, Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Falme za Kiarabu, na Qatar) zimepanua ushirikiano wao wa kijeshi na uvamizi huo katika miaka mitatu iliyopita, likinukuu vyanzo vyenye ufahamu. Gazeti hilo lilisema kwamba licha ya kulaani vikali taasisi ya Kiyahudi hadharani kutoka nchi za Kiarabu wakati wa vita vya Gaza, nyingi zao zimehifadhi kwa siri ushirikiano wa karibu wa kijeshi, ujasusi nayo. Kulingana na hati za Kimarekani zilizovuja ambazo gazeti na Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari za Upelelezi zilipata, angalau nchi sita za Kiarabu zilishiriki katika mfumo wa siri wa kikanda wa ulinzi unaojulikana kama "ujenzi wa usalama wa kikanda." Kuwait na Oman zimeorodheshwa kama washirika watarajiwa wa baadaye. Gazeti hilo lilisema kuwa utaratibu huo, ulioanzishwa kwa uratibu na Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM), ulifanya kazi kama mtandao wa siri wa kubadilishana habari, mafunzo ya pamoja na uratibu wa kiutendaji kwa lengo la kukabiliana na ushawishi wa kikanda wa Iran na kuimarisha uhusiano wa kijeshi na taasisi ya Kiyahudi.

Kufichuliwa kwa jambo hili ni matokeo tu. Waislamu, haswa wale wenye ufahamu, na hata watu wa kawaida katika nchi hizo, walikuwa wanajua kabisa kuwa mifumo yao inashirikiana na taasisi ya Kiyahudi ambayo inafanya vita vya ukomeshaji wa uzao ambavyo ni mbaya zaidi katika enzi hii dhidi ya Gaza. Kilichofanywa ni kwamba wamegeuza ushirikiano wao wa wazi kabla ya ukomeshaji wa uzao kuwa ushirikiano wa siri wakati wake. Wamehamisha uratibu na uhusiano wao kutoka hadharani kwenda kwa siri, si kwa chochote ila kuhofia usukani wao kuanguka na watu wao kuwaasi. Hata hivyo, ushirikiano huu haujasimama kwa dakika moja. Badala yake, wamefikia hatua ya kuipatia taasisi ya Kiyahudi wahalifu kila njia ya uzima ambayo inahakikisha kwamba inabakia na inaendelea na uhalifu wake. Kwa hivyo, haishangazi kwamba gazeti la Kimarekani linafichua jambo hili sasa. Ukweli kwamba watawala wa Waislamu ni watumwa wanyenyekevu kwa Marekani ni wazi kama jua la utosi. Hawathubutu kuasi, bali hutekeleza kile inachoamuru. Je, Marekani ingeweza kutekeleza mpango wa usaliti wa Trump bila wao? Marekani inalazimisha utawala wake juu ya nchi zetu kupitia wao.

-----------

Mkutano wa Sharm el-Sheikh: Misri kuwa mwenyeji wa viongozi wa dunia kumaliza vita vya Gaza

Misri itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa huko Sharm el-Sheikh, Jumatatu, kwa ushiriki wa zaidi ya viongozi 20 wa ulimwengu, kwa lengo la kukamilisha makubaliano ya kina ya kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza. Mkutano huo unakuja kwa mwaliko wa Misri na Amerika, ambayo inatafuta kuzindua awamu inayofuata ya mpango wake wa amani, ambayo ni pamoja na kufikia makubaliano ya mwisho ya kusitisha mapigano, na kuweka mipango ya baada ya vita katika ukanda huo, haswa kuhusiana na utawala, usalama, na ujenzi mpya. Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuwasili Misri mchana wa Jumatatu baada ya ziara ya taasisi ya Kiyahudi, ambapo atatoa hotuba mbele ya Knesset na kukutana na familia za wafungwa wa Kiyahudi ambao Hamas itawaachilia, kabla ya kushiriki katika sherehe rasmi ya kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano, akiandamana na Rais wa Misri Sisi na idadi ya viongozi wa nchi zinazodhamini makubaliano hayo.

Ni mchezo wa kuigiza wazi, ulioongozwa na Marekani na kuamuru Misri kuupanga! Huu si mkutano, bali ni sherehe ya kupiga magoti miguuni mwa Trump, mnyongaji mkuu na msaidizi wa kwanza wa taasisi ya Kiyahudi. Hawatkutana kushauriana, bali watasimama katika safu moja kama watumwa kumsifu bwana wao na kumpa ishara za shukrani kwa kusimamisha vita, vita ambavyo aliviunga mkono mwenyewe! Wanataka kwa mkusanyiko huu wa aibu kuhalalisha mpango wa usaliti na kuupitisha kwa umma. Na bwana wao awapapase mabegani na kuwapongeza kwa kufanikiwa kwao katika kusimamia mauaji ya halaiki ya enzi! Mkutano huu unaodaiwa si chochote ila ni mbio za watumwa kuthibitisha nani mwaminifu na mnyenyekevu zaidi kwa Marekani.

------------

Afghanistan inazishutumu kundi fulani huko Pakistan kwa kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili

Waziri wa Mambo ya Nje Kaimu katika serikali ya Afghanistan Amir Khan Muttaqi ameyashutumu makundi nchini Pakistan kwa kujaribu kudhoofisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Muttaqi alisema wakati wa ziara rasmi nchini India, ambayo ni ya kwanza ya aina yake tangu 2021, kwamba serikali yake haina matatizo yoyote na watu wa Pakistani au na wanasiasa nchini Pakistan. Alisisitiza kuwa baadhi ya makundi maalum nchini Pakistan yanajaribu kudhoofisha uthabiti, akieleza kuwa hakuna harakati ya Taliban ya Pakistan ndani ya ardhi ya Afghanistan, na kwamba vipengele ambavyo Islamabad inaona kama tishio kwake ni watu waliokimbia makazi yao ambao walitoka ndani ya Pakistan yenyewe. Alisema kuwa Afghanistan inalinda mipaka yake, anga yake na haki zake za uhuru, na kwamba itajibu ukiukaji wowote itakaofanyiwa. Kwa upande wake, msemaji wa serikali ya Taliban alisema kuwa taarifa za kuaminika zinathibitisha kwamba kiongozi wa shirika la Dola katika jimbo la Khorasan, Shihab al-Muhajir, na wasaidizi wake wa karibu Abdul Hakim Tawhidi, Sultan Aziz Azzam, na Salah al-Din Rajab (wanaohusishwa na uongozi mkuu wa shirika la Dola) kwa sasa wanajificha ndani ya ardhi ya Pakistan.

Ajabu iliyoje! Ndugu wanapigania nini? Na damu yao inamwagwa kwa faida ya nani na roho zao zinatolewa? Na wanashindania mipaka gani ya kishetani? Hii ni mipaka ya aibu iliyochorwa na Sykes na Picot, mipaka ambayo dini yetu au taifa letu haitambui. Kuhusu watawala wa Pakistani, jambo lao limefichuliwa, hawana chochote ila vibaraka mikononi mwa Amerika. Lakini msiba mkubwa ni Afghanistan, ambayo inajigamba kuwa ni emirate ya Kiislamu! Tunawauliza: Je, vita hivi vinaamriwa na Uislamu au na Washington? Ikiwa mlikuwa emirate ya Kiislamu kama mnavyodai, mngepaswa kukanyaga mipaka hii ya ukafiri kwa miguu yenu, na kuandaa majeshi ili kung'oa mizizi ya watawala wasaliti vibaraka, na kuunganisha taifa na kuunganisha nchi za Waislamu chini ya bendera moja. Fahamuni kwamba kumwaga damu ya Mwislamu ili kulinda mstari uliowekwa na mkoloni kafiri ni mojawapo ya madhambi makubwa zaidi mbele ya Mungu, na uhalifu usiosameheka! Mchezo wa Marekani uko wazi: kuchochea mzozo kati ya Pakistan na Afghanistan ili kuizamisha Pakistan katika dimbwi la jirani yake, na lengo halisi la haya yote ni kwamba India ijitolee kwa kazi yake ya msingi, ambayo ni kukabiliana na China. Hiyo ndiyo yote iliyopo, vita mnayoiona kati ya Pakistan na Afghanistan si chochote ila ni tukio katika mchezo huu wa Marekani.

More from null

Habari za Abu Wadaha: Msimamo na hotuba ya kukwamisha njama ya kutenganisha Darfur na Port Sudan

أبو وضاحة شعار

14-11-2025

Habari za Abu Wadaha: Msimamo na hotuba ya kukwamisha njama ya kutenganisha Darfur na Port Sudan

Katika muktadha wa kampeni inayoendeshwa na Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan kukwamisha njama ya Marekani ya kutenganisha Darfur, vijana wa Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan waliandaa msimamo baada ya sala ya Ijumaa, 23 Jumada al-Ula 1447 Hijria, sawia na 2025/11/14 Miladia, mbele ya Msikiti wa Bashikh, katika mji wa Port Sudan, kitongoji cha Deim Medina.


Mwalimu Muhammad Jami' Abu Ayman - msaidizi wa msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan alitoa hotuba kwa umati wa waliohudhuria, akitoa wito wa kufanya kazi ili kukwamisha mpango unaoendelea wa kutenganisha Darfur, akisema: Kwamisheni mpango wa Marekani wa kutenganisha Darfur kama walivyotenganisha Kusini, ili kulinda umoja wa umma, na Uislamu umeharamisha kuutenganisha umma huu na kuuvunja, na umeifanya umoja wa umma na dola kuwa suala la hatima, ambalo hatua moja inachukuliwa dhidi yake, uhai au mauti, na pale suala hili lilipoanguka kutoka hadhi yake, makafiri waliweza, wakiongozwa na Marekani, na kwa msaada wa baadhi ya watoto wa Waislamu, kuuvunja nchi yetu, na kutenganisha Sudan Kusini ..Na baadhi yetu walinyamaza kimya juu ya dhambi hii kubwa, na walijishughulisha na upungufu na udhaifu, hivyo uhalifu huo ulipita! Na leo Marekani inarudi tena, kutekeleza mpango huo huo, na kwa mazingira hayo hayo, kuikata Darfur kutoka mwilini mwa Sudan, kwa kile walichokiita mpango wa mipaka ya damu. Wakitegemea wanamgambo wanaokalia Darfur nzima na wameanzisha dola yao bandia kwa kutangaza serikali sambamba katika mji wa Nyala; Je, mtairuhusu Marekani kufanya hivyo katika nchi yenu?!


Kisha alielekeza ujumbe kwa wanazuoni, na kwa watu wa Sudan, na kwa maafisa waaminifu katika vikosi vya jeshi kuchukua hatua ya kukomboa Darfur nzima na kuzuia kujitenga na kwamba fursa bado ipo ya kuzima mpango wa adui, na kukwamisha uovu huu, na kwamba tiba ya msingi ni kuanzisha Khilafah Rashidah kwa njia ya unabii, kwani ni hiyo pekee itakayo uhifadhi umma, na itatetea umoja wake, na itasimamisha sheria ya Mola wake.


Kisha alihitimisha hotuba yake akisema: Sisi ndugu zenu katika Hizb ut-Tahrir tumechagua kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tumsaidie Mungu, na tumuamini, na tutimize bishara ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ basi njooni pamoja nasi kwani Mwenyezi Mungu ni msaidizi wetu bila shaka. Amesema Mwenyezi Mungu: {Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, naye atakunusuruni na atafanya imara nyayo zenu}.


Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan

Chanzo: Habari za Abu Wadaha

Rada: Babnusa Inaelekea Kufuata Mkondo wa Al-Fashir

الرادار شعار

13-11-2025

Rada: Babnusa Inaelekea Kufuata Mkondo wa Al-Fashir

Imeandikwa na Mhandisi/Hasbu Allah Al-Nur

Vikosi vya msaada wa haraka vilishambulia mji wa Babnusa siku ya Jumapili iliyopita, na kurudia shambulio lao asubuhi ya Jumanne.

Al-Fashir ilianguka kwa njia ya kusikitisha, na ilikuwa janga lililotikisa taifa la Sudan na kuumiza mioyo ya watu wake, ambapo damu safi ilimwagika, watoto walifiwa na baba, wanawake wakawa wajane, na mama zao waliomboleza.


Pamoja na majanga hayo yote, mazungumzo yanayoendelea Washington hayakuathirika hata kidogo, bali kinyume chake, mshauri wa Rais wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati, Musaad Bulus, aliliambia kituo cha Al Jazeera Mubasher tarehe 27/10/2025 kwamba kuanguka kwa Al-Fashir kunaimarisha mgawanyiko wa Sudan na kusaidia maendeleo ya mazungumzo!


Katika wakati huo muhimu, Wasudan wengi walitambua kwamba kinachotokea ni sura mpya tu ya mpango wa zamani ambao wazalendo wamekuwa wakionya dhidi yake, mpango wa kuitenga Darfur, ambao unataka kulazimishwa kwa njia ya vita, njaa na uharibifu.


Mzunguko wa kukataa kile kinachoitwa usitishaji wa mapigano wa miezi mitatu umeongezeka, na sauti za kupinga zimeongezeka, hasa baada ya habari kuvuja kuhusu uwezekano wa kuongezwa kwa miezi mingine tisa, ambayo kimsingi inamaanisha kuisomalia Sudan na kufanya mgawanyiko kuwa ukweli usioweza kuepukika kama ilivyo nchini Libya.


Na pale watengeneza vita waliposhindwa kunyamazisha sauti hizi kwa ushawishi, waliamua kuzinyamazisha kwa vitisho. Hivyo, dira ya mashambulizi ilielekezwa Babnusa, kuwa eneo la kurudia tukio la Al-Fashir; mzingiro mkali uliodumu kwa miaka miwili, na kuangusha ndege ya mizigo ili kuhalalisha kusimamishwa kwa usambazaji wa anga, na kulipua miji ya Sudan kwa wakati mmoja; Omdurman, Atbara, Damazin, Al-Abyad, Um Barmbita, Abu Jubaiha na Al-Abbasiya, kama ilivyotokea wakati wa shambulio la Al-Fashir.


Shambulio la Babnusa lilianza siku ya Jumapili, na liliongezeka tena asubuhi ya Jumanne, huku vikosi vya msaada wa haraka vikitumia mbinu na njia zilezile ambazo zilitumia huko Al-Fashir. Hadi wakati wa kuandika mistari hii, hakuna hatua yoyote halisi ya jeshi iliyorekodiwa kuwasaidia watu wa Babnusa, katika marudio ya kusikitisha ambayo karibu yanafanana na eneo la Al-Fashir kabla ya kuanguka kwake.


Ikiwa Babnusa itaanguka - Mungu apishie mbali - na sauti zinazopinga usitishaji wa mapigano hazitapungua, janga hilo litajirudia katika jiji lingine... Na kadhalika, hadi watu wa Sudan walazimishwe kukubali usitishaji wa mapigano wakiwa wanyonge.


Huo ndio mpango wa Amerika kwa Sudan kama unavyoonekana wazi; Kwa hivyo jihadharini, enyi watu wa Sudan, na fikirieni kile mnachofanya, kabla ya sura mpya yenye kichwa cha habari Mgawanyiko na Upotevu kuandikwa kwenye ramani ya nchi yenu.


Watu wa Babnusa wamehamishwa kabisa, ambao wanahesabu watu 177,000, kama ilivyoripotiwa katika kituo cha Al-Hadath tarehe 10/11/2025, na wanazurura bila mwelekeo.


Kupiga kelele, kulia, kupiga mashavu na kurarua mifuko ni tabia za wanawake, lakini hali hiyo inahitaji uanaume na ujasiri wa kukataa uovu, na kuchukua hatua dhidi ya mnyanyasaji, na kuinua neno la haki linalotaka kuachiliwa kwa minyororo ya majeshi ili kuchukua hatua ya kuokoa Babnusa, bali kurejesha Darfur yote.


Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Hakika watu wanapomuona dhalimu na hawamzuilii mkono wake, Mwenyezi Mungu yuko karibu kuwafunika kwa adhabu kutoka kwake.» Na akasema ﷺ: «Hakika watu wanapoona uovu na hawaubadilishi, Mwenyezi Mungu yuko karibu kuwafunika kwa adhabu.»


Na ni aina mbaya zaidi ya dhuluma, na miongoni mwa maovu makubwa, kuwakatisha tamaa watu wetu huko Babnusa kama watu wa Al-Fashir walivyokatishwa tamaa hapo awali.


Marekani ambayo inataka leo kuigawanya Sudan, ni ile ile iliyoigawanya kusini hapo awali, na inataka kuigawanya Iraq, Yemen, Syria na Libya, na kama watu wa Sham wanavyosema "na kamba iko kwenye mtungi", mpaka machafuko yataenea katika taifa lote la Kiislamu, na Mungu anatuita kwenye umoja.


Amesema Mwenyezi Mungu: ﴿NA HAKIKA HII DINI YENU NI DINI MOJA, NA MIMI NI MOLA WENU, BASI MCHENI﴾, na akasema ﷺ: «Akiapishwa Khalifa wawili, basi muueni yule mwingine miongoni mwao.» Na akasema: «Hakika yatakuwa majanga na majanga, na anayetaka kuutenganisha mambo ya umma huu na wao wote, mpigeni kwa upanga yeye yeyote anayekuwa.» Na pia alisema: «Anayekujieni na amri yenu nyote mkiwa juu ya mtu mmoja anayetaka kuigawanya fimbo yenu au kuitenganisha jamaa yenu, basi muueni.»


Je, nimefikisha? Ee Mwenyezi Mungu shuhudia, je, nimefikisha? Ee Mwenyezi Mungu shuhudia, je, nimefikisha? Ee Mwenyezi Mungu shuhudia.

Chanzo: Rada