Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Agosti 5, 2024 ni Siku ya Uasi wa Watu dhidi ya Dikteta Hasina na Utawala wa Kidikteta
Na "Tangazo la Julai" ni Hati ya Usaliti Iliyotolewa na Vyama vya Kisiasa Vya Kimarekani Ili Kukwamisha Uasi wa Watu
Mwaka mmoja umepita tangu Hasina aanguke katika uasi wa umma mnamo Agosti 5, 2024, ambapo mfumo dhalimu wa kidikteta aliokuwa akiwakilisha ulianguka. Lakini watu, katika kilele cha kukata tamaa, waligundua kuwa vibaraka wa Amerika na vyama vya kisiasa vyenye tamaa ya madaraka walikuwa wamechukua hatamu za kuamua hatima yao, wakaweka vikwazo mbele ya utekelezaji wa matumaini na matarajio yao, na bado wanajaribu kwa bidii kuteka nyara uasi huu. Na kile kinachoitwa "Tangazo la Julai" kilikuwa hatua ya aibu katika njia hii mbaya.
Watu wamekataa utumwa kwa Amerika na sarakasi ya kisiasa ya kupotosha kwa chuki yote. "Tangazo" hili haliakisi kamwe matarajio ya watu, lakini halitambui hata matukio hatari kama vile njama ya Uhindi huko Bilkhana, au mauaji dhidi ya Waislamu wanaopenda Uislamu katika uwanja wa Shapla. Wanazungumzia miaka ya 1971, 1975, na 1990 kama marejeleo, ambayo sura ya tabaka tawala ilibadilika, lakini hatima yao haikubadilika, kwa sababu mfumo mkuu wa kisiasa haukubadilika. Kwa kweli, tangazo hili limetungwa ili kudumisha uendelevu wa mfumo wa sasa wa kibepari wa kilimwengu, na kujisalimisha kwa utawala wa Amerika na washirika wake wa kikanda kama vile India.
Pia, watu walishuhudia kwamba viongozi wasaliti wa kile kinachoitwa harakati ya kupinga ubaguzi, ambao walidai kuongoza harakati ya wanafunzi, walikuwa wakisherehekea huko Cox's Bazar na Peter Haas siku ya kutolewa kwa tangazo la Julai ﴿Allaah awalaani! Vipi wanageuzwa (kutoka kwenye haki)﴾. Tunawakumbusha wasomi na wanasiasa ambao wameambukizwa na homa ya demokrasia, kwamba demokrasia yenyewe ni aina ya udikteta, kwa sababu inawapa watu mamlaka kamili ya enzi kuu. Hata Abraham Lincoln, ambaye anachukuliwa kuwa rais mkuu zaidi wa kidemokrasia ulimwenguni, alisimamisha sheria za kiraia katika maeneo fulani mwaka wa 1861, na akageuka kuwa dikteta kwa kukiuka katiba. Mnamo 1862, alisimamisha "upendeleo wa kutokamatwa kiholela" na kuwakamata wanademokrasia 13,000 wanaopinga chini ya sheria ya kijeshi, kwa sababu tu walipinga vita. Na wakati Jaji Mkuu alitangaza kuwa hatua hizi hazikuwa za kikatiba, Lincoln alitoa agizo la kumkamata, ingawa alikuwa na umri wa miaka 84!
Tukio hili linafunua kwamba chochote "kinachorekebishwa" uwiano wa nguvu ndani ya mfumo wa sasa, wasomi watawala wanabaki katika kitovu cha madaraka, na mabwana zao wa kikoloni - Waamerika - watawaunga mkono mradi tu wanabaki wamekaa juu ya vifua vya watu. Na ikiwa watu watawaondoa wasomi hao kupitia uasi wa umma, Amerika itarudi kuteka nyara harakati za watu tena chini ya ahadi za uongo za demokrasia. Ukweli huu umeshuhudiwa na watu wa nchi hii mara kwa mara kwa miongo kadhaa. Amesema Mwenyezi Mungu: ﴿Wanataka kwenda kuhukumiwa kwa Taghuti, na hali wameamrishwa wamkatae. Na Shetani anataka kuwapoteza upotevu mbali﴾.
Watu wamejaribu utawala wa demokrasia, kwa hivyo moja ya madai yao maarufu baada ya uasi wa umma ilikuwa kuondoa katiba ya kilimwengu na kuwasilisha katiba mbadala ya Kiislamu. Lakini serikali ya mpito, pamoja na vyama vya kisiasa vinavyounga mkono Amerika, ilichukua msimamo wa wazi dhidi ya Uislamu na Waislamu, na ilielezea madai ya kuanzisha Ukhalifa mtukufu kama itikadi kali, na iliwasilisha kwa Amerika ahadi zake za kupambana na Uislamu. Badala ya kuimarisha jeshi ili kukabiliana na adui Mhindi, walisababisha janga la Bilkhana. Ukweli ni kwamba India ni mmoja wa washirika wakuu wa Amerika katika eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki, kwa hivyo vyama vinavyounga mkono Amerika vinakubali sera ya kujisalimisha kwake.
Watu wa nchi hii wameachana na demokrasia na vyama hivi vya usaliti, na sasa wanaungana katika mapambano yao ya kuanzisha mfumo wa Kiislamu, yaani Ukhalifa. Ni Ukhalifa pekee ndio utakaoweka katiba ya Kiislamu, na kuhakikisha haki za haki kwa watu, na kuikomboa nchi kutoka kwa utawala wa makafiri wakoloni - Amerika - na kuichukulia India kama nchi adui, na kuondoa ushawishi wake wote kutoka nchi hii. ﴿Basi, ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu, basi watakao ufuata uwongofu wangu hawato potea wala hawato taabika﴾.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Bangladesh