
29/6/2025
Rada: Mwalimu Ghada Abdulgabbar (Ummu Awab) anaandika.. Dola ya kiraia imeshindwa kusimamisha uadilifu nyumbani kwake, vipi itafanikiwa kwetu?!
Waziri Mkuu wa Sudan, Kamel Idriss alitangaza katika mkutano na waandishi wa habari, kuundwa kwa serikali mpya inayoitwa "Serikali ya Matumaini", iliyo na wizara 22, na katika hotuba iliyoitwa (ya kihistoria), alifunua sifa za serikali ya matumaini aliyoiita serikali ya kiraia, na akasema kwamba inategemea maono wazi na kanuni thabiti za kuokoa Sudan, na kuiweka katika njia ya maendeleo na ustawi, na kufikia usalama na ustawi, na maisha mazuri kwa kila Msudani. Alibainisha kuwa maono hayo yanajumuisha kuipandisha Sudan hadi hadhi ya nchi zilizoendelea. Na maadili ni ukweli, uaminifu, uadilifu, uwazi, uvumilivu, na mbinu ni ya kisayansi, kivitendo, kitaalamu, ya pamoja, na mipango wazi na viwango sahihi vya mafanikio. Na serikali itakuwa ya teknolojia bila mfungamano wa chama, inawakilisha sauti ya walio wengi wasio na sauti, na inaunganisha kujizuia katika maonyesho ya mamlaka na ustawi wa watu, na inajumuisha fadhila za juu.
Waziri Mkuu alizungumza juu ya matokeo yanayotarajiwa ya serikali yake ya kiraia, akitaja ukweli, uaminifu, uadilifu na mengineyo, na kuunga mkono hilo kwa aya za Kurani, na mchanganyiko huu wa makusudi wa dhana tofauti ili kupata maoni ya umma yanayounga mkono. Ama ukweli ambao lazima usikilizwe na sikio makini unahitaji maelezo na uchunguzi wa kina mbali na hisia na matarajio, kwa hivyo siasa lazima zijengwe juu ya ukweli mbali na upotoshaji.
Mtu anayeangalia nchi za Waislamu, pamoja na Sudan, anagundua kwamba nchi zilizopo ndani yake ni matokeo ya makubaliano kati ya nchi za ukoloni wa zamani kugawana ushawishi mwaka 1916 BK, na ni nchi ndogo za kiutendaji, zilizoundwa kufanya kazi maalum, na hazikuwepo isipokuwa kwa makubaliano haya, na nchi hizi zimeendelea kuwa chini ya ubepari wa Magharibi ambao uliunda, na kwa muda wote wa uwepo wake, zimeendelea kushindana ili kuongoza orodha ya walioshindwa kila mwaka na zimethibitisha kwa ustahiki kushindwa vibaya katika ngazi zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii, bila kujali serikali, mawaziri na watawala wanabadilika, basi kasoro iko wapi? Na kwa nini nchi hizi zina utajiri mwingi wa rasilimali zao safi nyingi na watu wake wanaishi katika umaskini uliokithiri?!
Miongoni mwa mambo makuu ambayo Waislamu wamejaribiwa nayo katika zama zetu hizi ni fikra, na dhana zinazohusiana na utawala na uchumi, na labda ndio lengo la Magharibi katika mashambulizi yake dhidi ya Uislamu na katika kulenga utawala wake na udhibiti wa kisiasa, kiitikadi na kiuchumi.
Mizizi ya wazo la dola ya kiraia inarudi kwenye enzi za zamani, ambapo watu wa Magharibi huihusisha na kanuni za haki na utawala wa sheria katika ustaarabu wa Ugiriki, kupitia mfumo wa utawala wa kidemokrasia huko Athene ambao ulilenga ushiriki wa watu katika kufanya maamuzi, kisha dhana hizi zikawa na maendeleo zaidi na Warumi ambao waliweka misingi ya kisheria iliyoendelea ya kupanga mambo ya jamii, ambayo ilichangia katika kuunda na kuboresha kile kinachoitwa wazo la utawala wa sheria.
Na kwa maendeleo ya mawazo ya kisiasa katika Zama za Kati za Magharibi makafiri, dola ya kiraia iliathiriwa na mgogoro kati ya Kanisa na Dola huko Uropa na mgogoro huu ulisababisha kuimarisha kanuni ya kutenganisha dini na siasa, haswa baada ya Renaissance na Mapinduzi ya Ufaransa ambapo wito uliongezeka wa kuanzisha nchi zinazotegemea kuheshimu uhuru wa mtu binafsi na usawa mbele ya sheria bila kuingilia dini katika mambo ya kisiasa. Na katika enzi ya kisasa, nchi za Magharibi zililikumbatia na kiongozi wake Marekani.
Hapa linaibuka swali la kimantiki kama Waislamu na tuna urithi tofauti wa kistaarabu na historia ambayo haifanani na historia hii, yenye mizizi katika historia, kwani Mtume ﷺ; mwanzilishi wa dola ya Kiislamu huko Madina na baada yake Makhalifa Waongofu kisha Dola ya Umayya na Dola ya Abbas kisha Dola ya Ottoman, yote hayo ni mifano ya ustaarabu wa Kiislamu na asili yake na kwa utawala wa dola ya Kiislamu kwamba jicho haliwezi kukosea.
Na ili tuweze kuingia ndani zaidi, ni lazima tujue kanuni za dola ya kiraia na nini kinacholingana nayo katika utawala wa Uislamu:
Dola ya kiraia inategemea seti ya kanuni thabiti zinazolenga kufikia uadilifu kwa mtazamo wa ubepari wa Magharibi, kwa wazo la usawa na kulinda haki za watu, na kanuni hizi zinawakilisha nguzo kuu za nchi hizi, ama katika Uislamu, enzi kuu ni ya Sharia kwa hakika, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿HAPANA! NAAPA KWA MOLA WAKO! HAWATAAMINI MPAKA WAKUFANYE WEWE HUKUMU KATIKA YALE WANAYOZUSHIANA, KISHA WASIONE UDHIKU KATIKA NAFSI ZAO KWA ULIYO HUKUMU, NA WAJIWASILISHE KABISA﴾ Na akasema: ﴿HAIFAI MWANAMUME MWENYE KUAMINI WALA MWANAMKE MWENYE KUAMINI, ALLAH NA MTUME WAKE WANAPOAMUA JAMBO, WAWE NA HIYARI KATIKA JAMBO LAO. NA ANAYEMUASI ALLAH NA MTUME WAKE BASI AMEKWISHA POTELEA KWENYE UDHANI ULIO WAZI﴾ Na Mwenyezi Mungu akasema: ﴿JE WANATAFUTA HUKUMU ZA KIJAHILIA? NA NANI BORA ZAIDI KULIKO ALLAH KATIKA HUKUMU KWA WATU WANAO YAKINI?﴾.
Hizi ni maandiko kutoka kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu, thabiti na dalili, hakuna nafasi ya kukana, zote zinaelekea katika msemo mmoja kwa uwazi, ambayo maana yake ni kwamba enzi kuu ni ya sheria na sio ya akili, ni ya Mwenyezi Mungu na sio ya watu.
Na wanaamini katika dola ya mji kulingana na kanuni ya enzi kuu kwa watu kwamba kwa kufanya hivyo wanahakikisha kufikia haki na usawa katika jamii, na wanazuia ukiukwaji wowote au unyonyaji wa madaraka na hivyo utawala wa sheria ndio unaofanya serikali iwe chini ya kanuni za kisheria na inaweka taratibu za kuwajibisha maafisa, ambayo huimarisha uaminifu kati ya watu na serikali, ingawa hali yao ya leo inakinzana na hilo na imezama katika udhibiti wa wafanyabiashara na wanasiasa, na umma kwa ujumla ni wafuasi wanaowatii.
Na inaonekana kwamba kanuni ya "enzi kuu kwa sheria" ilifanya mfumo wa utawala katika Uislamu kuwa wa kipekee katika kufikia maana nzuri ya utawala wa sheria. Maana hii ambayo watetezi wa dola ya kiraia walidhani wameitimiza, wakati kwa kweli walifanya enzi kuu, kinadharia, kuwa ya walio wengi dhidi ya wachache (na kivitendo kwa wachache sana wa mabepari wenye ushawishi). Walio wengi ndio wanaweka sheria na ndio wanaibadilisha, basi vipi sheria itakuwa bwana wao?! Ama Uislamu ulihakikisha kwa kuondoa sheria kutoka kwa matamanio ya mwanadamu, ilihakikisha kwamba mwenye nguvu hamtumikishi dhaifu, wala tajiri hamtumikishi dhaifu, bali wote wanamtii Mwenyezi Mungu.
Hiyo inadhihirika katika mfumo wa utawala, kwani Muumba alianzisha amri na makatazo katika nyanja mbalimbali za maisha na alifanya Mwenyezi Mungu Mtukufu mamlaka ya utekelezaji kwa umma (kateni, pigeni mijeledi,…), wanachagua kutoka miongoni mwao, kwa kufanya ahadi kwa ridhaa na uchaguzi, yule atakayewatekelezea hukumu za kisheria.
Pia, dola ya kiraia inatoa umuhimu mkubwa kwa kulinda haki za binadamu na kuhakikisha uhuru wa mtu binafsi, na haki hizi zinajumuisha uhuru wa imani, uhuru wa maoni, uhuru wa kibinafsi na uhuru wa mali.
Na ukweli ni kwamba fikra hizi kwa maana yake halisi, hazina umaarufu wowote miongoni mwa Waislamu na kwamba sababu ya kuibuka kwake kama maneno katika uwanja wa Waislamu ni ukosefu wa ufahamu wa ukweli wake na uelewa wa uhalisia wake kama mtazamo tofauti na Uislamu kwa ujumla na kwa undani mbali na matangazo ya kupotosha, kwa hivyo fikra hizi ziliibuka, na zilichukua nafasi ya mbele katika mapinduzi kama kauli mbiu zinazoonyesha kukataa dhuluma na vizuizi vya uhuru ambavyo vilifanywa dhidi ya watoto wa Waislamu na watawala vibaraka wa Magharibi makafiri na wasaidizi wao, lakini Mwislamu yeyote anajua kwamba amefungwa na sheria ya Mungu na amri na makatazo yake.
Waislamu wana mradi wa utawala ambao Mungu ameuteremsha na Mtume wake ﷺ ameanzisha, katika dola ya Madina, mfumo wa utawala ambao Uislamu unatekelezwa na haki na usawa hutawala, kwa hivyo tunarudi kama tulivyokuwa Waislamu kwa Mola wa walimwengu, tukishikilia mienge ya uongofu badala ya kuiga mabepari walioshindwa.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Ghada Abdul Jabbar (Ummu Awab) - Wilaya ya Sudan
Chanzo: Rada
