
6-11-2025
Rada: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan.. Taarifa kwa Vyombo vya Habari Amerika Inayotaka Kuikata Darfur Inazusha Suala la Abyei na Inatishia!
Baada ya Sudan Kusini kujitenga na kaskazini mnamo 2011, eneo la Abyei liliachwa likiwa linazozaniwa na haikuamuliwa uhusiano wake na upande wowote; Kusini na Kaskazini, ambapo ilitarajiwa kuwa kura ya maoni ingefanyika Abyei mnamo 2011, sambamba na kura ya maoni ya Sudan Kusini, kuamua uhusiano wa eneo hilo na Kaskazini au Kusini, lakini kura ya maoni haikufanyika, kwa sababu ya mzozo kati ya nchi hizo mbili kuhusu ni nani anayestahili kupiga kura katika kura ya maoni! Kwani eneo hilo linakaliwa na makabila yanayofuata Kusini, ambalo ni kabila la Dinka Ngok, na lingine linalofuata Kaskazini, ambalo ni kabila la Misseriya, na bila shaka Wadinka hawataridhika kujitenga na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na serikali ya Kaskazini kwa sababu watakuwa mnyororo dhaifu katika serikali ya Sudan, na vile vile Wamisiriya hawata kubali kujitenga na mazingira yao ya kikabila ili kuwa na serikali ya Kusini kwa sababu pia watakuwa mnyororo dhaifu katika serikali.
Kisha vita fupi vilizuka katika eneo hilo mnamo 2012, lakini iliamuliwa kwa kuunda kikosi cha muda cha usalama cha Umoja wa Mataifa cha Abyei (UNISFA), na mnamo Novemba 2020, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano kuhusu utekelezaji wa azimio lake namba 2046 linalohusu masuala ya pande mbili yaliyosalia kati ya Sudan na Sudan Kusini, na hali katika majimbo ya Kordofan Kusini na Nile ya Bluu, bila kutoa uamuzi wazi kuhusu Abyei.
Kisha kulikuwa na mkutano wa mwisho jana Jumatano 5/11/2025, ambapo Balozi wa Marekani Michael Waltz alitishia Sudan kaskazini na kusini, kwamba atapinga kuongezwa muda wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (UNISFA), ambao muda wake utaisha tarehe 15 Novemba ya sasa, ikiwa pande hizo mbili hazitatii majukumu yao kwa makubaliano ya amani, ambayo kwayo Sudan Kusini ilitenganishwa.
Sisi katika Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan, tulikuwa tumeonya kupitia taarifa kwa vyombo vya habari tarehe 21/5/2011, kuhusu hatari ya makubaliano ya Naivasha, na tukasisitiza kwamba eneo la Abyei litakuwa (Kashmir ya Sudan); suala la mpaka lililosalia, na tayari zaidi ya miaka 14 imepita tangu tulisema hili, na suala la Abyei bado liko pale pale, na hii si ajabu kwa nchi za kikoloni, kwani kuna maeneo yanayozozaniwa kati ya nchi za Kiislamu; haswa eneo la Kiarabu, ambalo liligawanywa mnamo 1916, kupitia makubaliano mabaya ya Sykes-Picot, na suala la mzozo juu yake halijaamuliwa, kwa sababu limelikusudiwa kwa lenyewe, na mfano mzuri wa hilo ni suala la mzozo juu ya Halayeb na Shalateen kati ya Misri na Sudan.
Masuala haya ambayo kimsingi yako ndani ya mipaka ya nchi za Waislamu hayatatatuliwa, isipokuwa kwa kuanzisha dola ya Khilafah, ambayo itaunganisha nchi zote za Waislamu, ambapo hakutakuwa na mzozo juu ya mipaka, kwani ardhi ni ardhi ya Kiislamu ya kharajia au ashiria, na hii inahitaji umma kukimbilia kuianzisha iliyoongoka juu ya njia ya Utume, ikikata mkono wa kafiri mkoloni anayecheza na nchi zetu.
Alhamisi 15 Jumada al-Awwal 1447 Hijria
06/11/2025 Miladia
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Rada
