
14/6/2025
Rada: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan Yatoa Taarifa Muhimu..
Taarifa kwa vyombo vya habari
Hakuna kitakacho zuia kuongezeka kwa wanamgambo na majeshi sambamba isipokuwa Ukhalifa ulioongoka kwa njia ya Utume
Kongamano la Tamantai limetangaza muungano wa kijeshi unaoitwa Vikosi vya Pamoja vya harakati za Mashariki mwa Sudan, na unajumuisha vikosi vya Kongamano la Beja Uongozi wa Muungano chini ya uongozi wa Muhammad Tahir, vikosi vya Urta ya Mashariki chini ya uongozi wa Kamanda Al-Amin Dawood, na Upinzani wa Watu, na Wanaojitolea chini ya uongozi wa Nazir Turk. Tangazo hili linakuja katika mazingira ya vita ambayo isingekuwepo bila kuwepo kwa jeshi linalofanana na jeshi la dola; Vikosi vya Msaada wa Haraka, vita hivi ambavyo vimeharibu kila kitu, vimeharibu miundombinu, vimewafukuza watu, vimevunja heshima, na kuua maelfu ya raia wasio na hatia kwa damu baridi, baada ya yote haya yaliyotokea, na bado yanatokea, serikali bado inafumbia macho uanzishwaji wa majeshi mapya, bali inatumia baadhi yao, ambayo inahimiza kila mtu kuanzisha wanamgambo na jeshi sambamba na jeshi la dola, na mbaya zaidi ni kwamba majeshi haya yote yanayokinzana yanaendeshwa chini ya itikadi za upofu, ama za kikanda, au za kikabila, na ingawa kuwepo kwake kimaumbile kunamaanisha uharibifu wa nchi, na kupoteza nguvu zake, na kuiandaa kwa mgawanyiko na uvunjaji unaotakikana na Magharibi kafiri mkoloni ambayo ilianza kwa kutenganisha Sudan Kusini, na sasa inajitahidi kwa hatua za haraka kutenganisha Darfur.
Kuzungumzia vikosi vya pamoja katika Mashariki mwa Sudan, ambavyo ni vikosi vya kikanda, kunamaanisha kuiweka Mashariki mwa Sudan kwenye mashine ya kuchanika.
Ama kwa upande wa kisheria, haifai kwa dola kuwa na majeshi mawili, achilia mbali kuweko kwa majeshi yanayotegemea ushabiki wa kikabila, au kikanda, Mtume ﷺ anasema: «Na yeyote anayepigana chini ya bendera ya upofu, anaghadhibika kwa ajili ya ushabiki, au anatoa wito kwa ushabiki, au anashinda ushabiki, kisha akauawa, basi kifo chake ni cha kijahiliya».
Na Hizb ut-Tahrir imebainisha katika rasimu ya katiba ya dola ya Khilafa umoja wa jeshi, ambapo imekuja katika kifungu cha 66 cha rasimu ya katiba ya dola ya Khilafa: (Jeshi lote linafanywa kuwa jeshi moja ambalo linawekwa katika kambi maalum, isipokuwa kwamba baadhi ya kambi hizi lazima ziwekwe katika majimbo mbalimbali na baadhi yake katika maeneo ya kimkakati, na baadhi yake hufanywa kuwa kambi za mzunguko zinazozunguka daima ambazo ni vikosi vya kushambulia, na kambi hizi zimepangwa katika makundi mengi, kila kundi likiitwa jeshi, na kupewa nambari na kusemwa jeshi la kwanza, jeshi la tatu, kwa mfano, au linaitwa jina la jimbo kutoka majimbo au wilaya kutoka wilaya).
Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan, tunathibitisha kwamba uanzishwaji wa harakati za silaha na wanamgambo wa kikabila au kikanda hautumikii chochote isipokuwa mpango wa kafiri mkoloni anayetafuta kuivunja Sudan na kuipasua.
Hivyo tunawaomba wenye akili timamu kutoka Sudan kufanya kazi ya kukata njia kwa mipango ya kafiri mkoloni na vibaraka wake ndani, kwa kufanya kazi kwa bidii na Hizb ut-Tahrir; kiongozi ambaye hasemi uongo kwa watu wake, kuanzisha Khilafa iliyoongoka kwa njia ya Utume, ambayo inaunganisha nchi na kuondoa machafuko haya yote, bali inatafuta kuiunganisha na nchi zingine za Waislamu.
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye jambo linao kuhuisheni﴾
Alhamisi 16 Dhul-Hijja 1446H
2025/6/12M
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Rada
