Rada: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan Yatoa Taarifa Muhimu
June 29, 2025

Rada: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan Yatoa Taarifa Muhimu

الرادار شعار

28/6/2025

Rada: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan Yatoa Taarifa Muhimu

Tofauti kubwa iliyopo baina ya heshima chini ya kivuli cha Uislamu, na unyonge chini ya ukandamizaji wa tawala tegemezi.

Kamati Kuu ya mitihani ya shahada ya Sudan imetoa wito kwa jamii ya kimataifa na mashirika husika kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu, na kuchangia katika kuwawezesha wanafunzi wote wa Sudan, kufanya mitihani, haswa maeneo yaliyoathirika na vita, na hali ngumu za kibinadamu. (Suna, 26/06/2025).

Bado kuna kundi la watu wetu wana matumaini mema kwa Umoja wa Mataifa na mashirika yake, na wanatarajia msaada kutoka kwa wale wanaoitwa jamii ya kimataifa na mashirika ya kimataifa, licha ya historia yake ambayo inathibitisha kuwa haitoi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani siyo vyama vya hisani, bali ina ajenda ambayo inafichuka kila wakati kuhusu uadui wake wa wazi kwa Uislamu na Waislamu.

Mnamo mwaka wa 2016, UNESCO ilifanya mkutano wa kuzuia (itikadi kali za vurugu), na mojawapo ya matokeo yake ilikuwa kwamba "lazima suala la kubadilisha mitaala ya elimu katika Mashariki ya Kati, na maeneo mengine ambayo yanashuhudia ustawi wa mawazo kali, lishughulikiwe".

Neno hili (mawazo kali) linatumiwa na linamaanisha Uislamu pekee, kwa sababu nchi za Magharibi zinazodhibiti ulimwengu leo, zinataka Uislamu wa ukasisi, ambao hauna uhusiano wowote na maisha, kwa upande wa mifumo ya utawala na siasa, mfumo wa kiuchumi, na mfumo wa kijamii, ili wasipate kikwazo katika kutekeleza mipango yao, bali wanaendelea na matendo yao yote ya uhalifu dhidi ya Waislamu; ya mateso na mauaji, na kujitenga kwa Sudan Kusini, na vita vinavyoendelea sasa nchini Sudan, ni matokeo ya kufuata Magharibi ya kibepari, na mashirika yake ya uhalifu.

Jukumu la mashirika haya yanayoitwa ya kibinadamu linazidi kile kilichotangazwa, hadi kujaribu kupotosha maoni ya umma, kwa kusambaza habari potofu kuhusu ukweli wa hali katika maeneo ambayo yanaendesha shughuli zake, ili shughuli zake ziendelee, pamoja na kufanya majukumu ya ujasusi yenye shaka kwa niaba ya nguvu za kimataifa, hata idadi ya wachunguzi walielezea kuwa ni zana za ukoloni mamboleo! Bali ni miongoni mwa zana hatari zaidi za mizozo ya kimataifa.

Na nchini Sudan, ni mara ngapi mashirika haya ya kimataifa yamefichuliwa yakifanya kazi ya ujasusi, na upelelezi kwa maslahi ya nchi za Magharibi, na hiyo haishii tu katika kukusanya taarifa, bali inazidi kueneza sumu za mgawanyiko, na mapigano kati ya makundi ya wakazi, kama ilivyotokea Sudan Kusini, ambapo mashirika haya yamechangia kwa upendeleo wao kwa upande mmoja wa mzozo, katika kuzidisha migogoro hii, wakitumia kinga walizopewa.

Ukombozi wetu uko mikononi mwetu wala si mikononi mwa maadui zetu ambao wanatuwindia; iwe ni wale wanaotuonyesha uadui waziwazi, au wale wanaovaa unafiki kama vazi la marafiki, na vazi la "washirika" (wafadhili).

Kuhusisha masuala ya elimu; ambayo ni muhimu zaidi katika kulea na kutengeneza vizazi kupitia hayo na mashirika haya yenye shaka, ni sawa na kujiua kisiasa, na ni maangamizi makubwa, ambayo athari zake za uharibifu kwa jamii zinaonekana mapema au baadaye.

Elimu inawakilisha nguzo muhimu katika uamsho wa Waislamu, na ili iwe hivyo lazima kuwe na mfumo wa kisiasa uliojengwa juu ya itikadi ya Uislamu mkuu, mfumo ambao unajumuisha maono ya kisiasa tofauti, ya juu, na huru kwa nchi yake, kuondoa wanadamu kutoka katika giza la ukafiri, upotofu na ujinga, hadi kwenye nuru ya Uislamu na uadilifu wake, ambao huleta kwa wanadamu katika nyanja zote za maisha; kiroho, kiakili, kiadili, kisiasa, kiuchumi, na zinginezo, na katika sayansi na teknolojia. Mfumo huu wa kisiasa, kwa kauli moja, ni mfumo wa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ambao unatekeleza Uislamu na mifumo yake kikamilifu, na ambao uliongoza ulimwengu kwa karne kadhaa katika ubora wa taasisi zake za kitaaluma, na uvumbuzi wake wa hali ya juu, na uvumbuzi, pamoja na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya binadamu, basi ni tofauti kubwa iliyopo baina ya heshima chini ya kivuli cha Uislamu, na unyonge chini ya kivuli cha mifumo ya utegemezi.

Ijumaa ٠٢ Muharram 1447 Hijria

2025/06/27 Miladia

Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan

Chanzo: Rada

More from null

Habari za Abu Wadaha: Msimamo na hotuba ya kukwamisha njama ya kutenganisha Darfur na Port Sudan

أبو وضاحة شعار

14-11-2025

Habari za Abu Wadaha: Msimamo na hotuba ya kukwamisha njama ya kutenganisha Darfur na Port Sudan

Katika muktadha wa kampeni inayoendeshwa na Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan kukwamisha njama ya Marekani ya kutenganisha Darfur, vijana wa Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan waliandaa msimamo baada ya sala ya Ijumaa, 23 Jumada al-Ula 1447 Hijria, sawia na 2025/11/14 Miladia, mbele ya Msikiti wa Bashikh, katika mji wa Port Sudan, kitongoji cha Deim Medina.


Mwalimu Muhammad Jami' Abu Ayman - msaidizi wa msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan alitoa hotuba kwa umati wa waliohudhuria, akitoa wito wa kufanya kazi ili kukwamisha mpango unaoendelea wa kutenganisha Darfur, akisema: Kwamisheni mpango wa Marekani wa kutenganisha Darfur kama walivyotenganisha Kusini, ili kulinda umoja wa umma, na Uislamu umeharamisha kuutenganisha umma huu na kuuvunja, na umeifanya umoja wa umma na dola kuwa suala la hatima, ambalo hatua moja inachukuliwa dhidi yake, uhai au mauti, na pale suala hili lilipoanguka kutoka hadhi yake, makafiri waliweza, wakiongozwa na Marekani, na kwa msaada wa baadhi ya watoto wa Waislamu, kuuvunja nchi yetu, na kutenganisha Sudan Kusini ..Na baadhi yetu walinyamaza kimya juu ya dhambi hii kubwa, na walijishughulisha na upungufu na udhaifu, hivyo uhalifu huo ulipita! Na leo Marekani inarudi tena, kutekeleza mpango huo huo, na kwa mazingira hayo hayo, kuikata Darfur kutoka mwilini mwa Sudan, kwa kile walichokiita mpango wa mipaka ya damu. Wakitegemea wanamgambo wanaokalia Darfur nzima na wameanzisha dola yao bandia kwa kutangaza serikali sambamba katika mji wa Nyala; Je, mtairuhusu Marekani kufanya hivyo katika nchi yenu?!


Kisha alielekeza ujumbe kwa wanazuoni, na kwa watu wa Sudan, na kwa maafisa waaminifu katika vikosi vya jeshi kuchukua hatua ya kukomboa Darfur nzima na kuzuia kujitenga na kwamba fursa bado ipo ya kuzima mpango wa adui, na kukwamisha uovu huu, na kwamba tiba ya msingi ni kuanzisha Khilafah Rashidah kwa njia ya unabii, kwani ni hiyo pekee itakayo uhifadhi umma, na itatetea umoja wake, na itasimamisha sheria ya Mola wake.


Kisha alihitimisha hotuba yake akisema: Sisi ndugu zenu katika Hizb ut-Tahrir tumechagua kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tumsaidie Mungu, na tumuamini, na tutimize bishara ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ basi njooni pamoja nasi kwani Mwenyezi Mungu ni msaidizi wetu bila shaka. Amesema Mwenyezi Mungu: {Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, naye atakunusuruni na atafanya imara nyayo zenu}.


Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan

Chanzo: Habari za Abu Wadaha

Rada: Babnusa Inaelekea Kufuata Mkondo wa Al-Fashir

الرادار شعار

13-11-2025

Rada: Babnusa Inaelekea Kufuata Mkondo wa Al-Fashir

Imeandikwa na Mhandisi/Hasbu Allah Al-Nur

Vikosi vya msaada wa haraka vilishambulia mji wa Babnusa siku ya Jumapili iliyopita, na kurudia shambulio lao asubuhi ya Jumanne.

Al-Fashir ilianguka kwa njia ya kusikitisha, na ilikuwa janga lililotikisa taifa la Sudan na kuumiza mioyo ya watu wake, ambapo damu safi ilimwagika, watoto walifiwa na baba, wanawake wakawa wajane, na mama zao waliomboleza.


Pamoja na majanga hayo yote, mazungumzo yanayoendelea Washington hayakuathirika hata kidogo, bali kinyume chake, mshauri wa Rais wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati, Musaad Bulus, aliliambia kituo cha Al Jazeera Mubasher tarehe 27/10/2025 kwamba kuanguka kwa Al-Fashir kunaimarisha mgawanyiko wa Sudan na kusaidia maendeleo ya mazungumzo!


Katika wakati huo muhimu, Wasudan wengi walitambua kwamba kinachotokea ni sura mpya tu ya mpango wa zamani ambao wazalendo wamekuwa wakionya dhidi yake, mpango wa kuitenga Darfur, ambao unataka kulazimishwa kwa njia ya vita, njaa na uharibifu.


Mzunguko wa kukataa kile kinachoitwa usitishaji wa mapigano wa miezi mitatu umeongezeka, na sauti za kupinga zimeongezeka, hasa baada ya habari kuvuja kuhusu uwezekano wa kuongezwa kwa miezi mingine tisa, ambayo kimsingi inamaanisha kuisomalia Sudan na kufanya mgawanyiko kuwa ukweli usioweza kuepukika kama ilivyo nchini Libya.


Na pale watengeneza vita waliposhindwa kunyamazisha sauti hizi kwa ushawishi, waliamua kuzinyamazisha kwa vitisho. Hivyo, dira ya mashambulizi ilielekezwa Babnusa, kuwa eneo la kurudia tukio la Al-Fashir; mzingiro mkali uliodumu kwa miaka miwili, na kuangusha ndege ya mizigo ili kuhalalisha kusimamishwa kwa usambazaji wa anga, na kulipua miji ya Sudan kwa wakati mmoja; Omdurman, Atbara, Damazin, Al-Abyad, Um Barmbita, Abu Jubaiha na Al-Abbasiya, kama ilivyotokea wakati wa shambulio la Al-Fashir.


Shambulio la Babnusa lilianza siku ya Jumapili, na liliongezeka tena asubuhi ya Jumanne, huku vikosi vya msaada wa haraka vikitumia mbinu na njia zilezile ambazo zilitumia huko Al-Fashir. Hadi wakati wa kuandika mistari hii, hakuna hatua yoyote halisi ya jeshi iliyorekodiwa kuwasaidia watu wa Babnusa, katika marudio ya kusikitisha ambayo karibu yanafanana na eneo la Al-Fashir kabla ya kuanguka kwake.


Ikiwa Babnusa itaanguka - Mungu apishie mbali - na sauti zinazopinga usitishaji wa mapigano hazitapungua, janga hilo litajirudia katika jiji lingine... Na kadhalika, hadi watu wa Sudan walazimishwe kukubali usitishaji wa mapigano wakiwa wanyonge.


Huo ndio mpango wa Amerika kwa Sudan kama unavyoonekana wazi; Kwa hivyo jihadharini, enyi watu wa Sudan, na fikirieni kile mnachofanya, kabla ya sura mpya yenye kichwa cha habari Mgawanyiko na Upotevu kuandikwa kwenye ramani ya nchi yenu.


Watu wa Babnusa wamehamishwa kabisa, ambao wanahesabu watu 177,000, kama ilivyoripotiwa katika kituo cha Al-Hadath tarehe 10/11/2025, na wanazurura bila mwelekeo.


Kupiga kelele, kulia, kupiga mashavu na kurarua mifuko ni tabia za wanawake, lakini hali hiyo inahitaji uanaume na ujasiri wa kukataa uovu, na kuchukua hatua dhidi ya mnyanyasaji, na kuinua neno la haki linalotaka kuachiliwa kwa minyororo ya majeshi ili kuchukua hatua ya kuokoa Babnusa, bali kurejesha Darfur yote.


Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Hakika watu wanapomuona dhalimu na hawamzuilii mkono wake, Mwenyezi Mungu yuko karibu kuwafunika kwa adhabu kutoka kwake.» Na akasema ﷺ: «Hakika watu wanapoona uovu na hawaubadilishi, Mwenyezi Mungu yuko karibu kuwafunika kwa adhabu.»


Na ni aina mbaya zaidi ya dhuluma, na miongoni mwa maovu makubwa, kuwakatisha tamaa watu wetu huko Babnusa kama watu wa Al-Fashir walivyokatishwa tamaa hapo awali.


Marekani ambayo inataka leo kuigawanya Sudan, ni ile ile iliyoigawanya kusini hapo awali, na inataka kuigawanya Iraq, Yemen, Syria na Libya, na kama watu wa Sham wanavyosema "na kamba iko kwenye mtungi", mpaka machafuko yataenea katika taifa lote la Kiislamu, na Mungu anatuita kwenye umoja.


Amesema Mwenyezi Mungu: ﴿NA HAKIKA HII DINI YENU NI DINI MOJA, NA MIMI NI MOLA WENU, BASI MCHENI﴾, na akasema ﷺ: «Akiapishwa Khalifa wawili, basi muueni yule mwingine miongoni mwao.» Na akasema: «Hakika yatakuwa majanga na majanga, na anayetaka kuutenganisha mambo ya umma huu na wao wote, mpigeni kwa upanga yeye yeyote anayekuwa.» Na pia alisema: «Anayekujieni na amri yenu nyote mkiwa juu ya mtu mmoja anayetaka kuigawanya fimbo yenu au kuitenganisha jamaa yenu, basi muueni.»


Je, nimefikisha? Ee Mwenyezi Mungu shuhudia, je, nimefikisha? Ee Mwenyezi Mungu shuhudia, je, nimefikisha? Ee Mwenyezi Mungu shuhudia.

Chanzo: Rada