
20/6/2052
Rada: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan Yatoa *Taarifa kwa Vyombo vya Habari* Muhimu
*Mamlaka za kiusalama* katika mji wa Al Qadarif zinawakamata vijana wa Hizb ut-Tahrir kwa ajili ya kunusuru chombo cha Kiyahudi*!
Kufuatia vijana wa Hizb ut-Tahrir katika mji wa Al Qadarif kutoa hotuba ya hadhara katika soko la Al Qadarif, karibu na Hospitali ya Meno, jana Alhamisi, 23 Dhul-Hijjah 1446 Hijria, sawia na 19/6/2025 Miladia, ambayo ndani yake Ustadh Awad Muhajir, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, alizungumzia uhalisia wa vita na chombo cha Kiyahudi, na furaha ya Waislamu kulipiga chombo hicho, na kiu ya watu ya ushindi dhidi ya chombo hicho kinachokalia ardhi takatifu, Masra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, akisisitiza ulazima wa kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ambayo itakomboa Palestina, na nchi zingine za Waislamu zinazokaliwa. Ambapo waliohudhuria waliitikia vyema hotuba hiyo, na kulikuwa na michango bora kutoka kwa waliohudhuria…
Mara tu hotuba ilipoisha, na kabla ya umati kutawanyika, magari matatu ya vyombo vya usalama yalifika, na kuwakamata vijana watatu wa Hizb ut-Tahrir, ambao ni ndugu: Al-Mahi Abidin, Maisara Yahya, na Muhammad Yahya, pamoja na mtu wa nne kutoka kwa waliohudhuria, na waliwapiga, na kuwafunga macho. Kisha wakawapeleka mahali kusikojulikana, na kuchukua nao kifaa cha sauti kilichotumika katika hotuba, huku waliohudhuria wakishangazwa na kitendo hicho cha ajabu, na waliokamatwa hawajaachiliwa hadi kuandikwa kwa taarifa hii!!
Kutokana na kitendo hiki cha kinyama, sisi katika Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan tunasisitiza yafuatayo:
Kwanza: Tunalichukulia serikali kuwajibika kwa usalama wa ndugu waliokamatwa, na tunawaonya, na vibaraka wao, dhidi ya matokeo ya vitendo kama hivyo ambavyo havifanani na Uislamu na Waislamu, na vinaingia katika mrengo wa kusimama na Mayahudi ndugu wa nyani na nguruwe na wanaowaunga mkono miongoni mwa makafiri wakoloni, na kutoka kwa watawala wa nchi za dhiki katika nchi za Waislamu, ambao wanadhani kila ukelele ni dhidi yao, Mwenyezi Mungu awaangamize vipi wanageuzwa!
Pili: Kitendo hiki cha ajabu na cha kutiliwa shaka, kutoka kwa wale ambao walipaswa kuwanusuru ndugu zao huko Palestina, kinathibitisha kwamba tawala hizi, pamoja na mfumo wa utawala nchini Sudan, ni maadui wa Umma, na kazi yao ni kulinda chombo cha Kiyahudi kilichoharibika, na kutekeleza njama za makafiri wakoloni katika nchi yetu. Na vita visivyo na maana vinavyoendelea nchini Sudan ni mojawapo ya matokeo ya kufuata utekelezaji wa mipango ya Amerika; mlezi wa chombo cha Kiyahudi, na adui wa Uislamu na Waislamu.
Tatu: Khilafah ambayo inawatisha Mayahudi, na watawala wa Magharibi makafiri wakoloni, pamoja na vibaraka wao kutoka kwa watawala wa tawala ndogo za dhiki katika nchi za Waislamu, tunasema kwamba Khilafah hii inakuja bila shaka, na huu ndio wakati wake, na huu ndio zama zake kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na msaada wake, na hapo itawalipa wote waliofanya uhalifu dhidi ya Umma huu.
Mwisho, tunauambia mfumo tawala nchini Sudan, na vyombo vyake vya usalama ambavyo vilifanya kitendo hiki kibaya, tunawaambia waachilie mara moja wabebaji wa ulinganiaji wa haki, na mcheni Mwenyezi Mungu na mjue kuwa Mwenyezi Mungu hatengenezi kazi ya waharibifu, basi msiwe chombo cha kupiga vita Uislamu na wabebaji wa ulinganiaji wake, itawafika udhalili katika dunia, na adhabu kali katika Akhera.
﴿WALE WANAO PENDELEA MAISHA YA DUNIA KULIKO AKHERA, NA WANAZUIYA NJIA YA MWENYEZI MUNGU, NA WANATAFUTA IWE POTOFU. HAO WAMO KATIKA UDHANI WA MBALI﴾
Ijumaa 24 Dhul-Hijjah 1446 Hijria
20/06/2025 Miladia
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Rada
