
5/8/2025
Rada: Hizb ut-Tahrir Wilaya ya Sudan Yatoa Taarifa Muhimu kwa Vyombo vya Habari
Bismillahir Rahmanir Rahim
*Taarifa kwa Vyombo vya Habari*
*Uhusiano na nchi za kigeni ni wa serikali pekee, kwa sababu yenyewe ndiyo ina haki ya kusimamia masuala ya umma kivitendo*
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti habari kwamba ujumbe kutoka muungano wa vyama na harakati za mashariki mwa Sudan, ukiongozwa na Shiba Darar, na kuandamana na ujumbe kutoka kwa wazee, ulikutana na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki siku ya Jumamosi 2/8/2025 katika ofisi yake ya "Badi Hallou" ambapo ujumbe ulijadili naye hali ya sasa nchini Sudan kwa ujumla, huku wakizingatia changamoto zinazoikabili mkoa wa mashariki mwa Sudan. Ujumbe huo pia ulisisitiza umuhimu wa uratibu na nchi jirani ili kuunga mkono utulivu wa nchi na kukabiliana na migogoro ya kisiasa na kiusalama.
Je, udhaifu na dharau ya serikali ya Sudan imefikia kiasi hiki, au inajaribu kuwafanya watu wakubali picha hizi potofu, kwa haja iliyo ndani yake; picha hizi ambazo zinajumuisha mafunzo ya wanamgambo wenye uaminifu wa kikanda au kikabila nchini Eritrea?!
Ghasia hizi zinazodhaminiwa na serikali ya Sudan, kisiasa na kijeshi, na ikiwa ni pamoja na kukuza matamshi ya kibaguzi katika duru za kisiasa, yote hayo yanatumikia mpango wa Amerika wa kuigawa Sudan katika majimbo kadhaa; Darfur, kisha mashariki mwa Sudan!!
Serikali ya Sudan inapaswa kuacha upumbavu huu na kuacha kucheza na moto, ambao utaharibu umoja wa sehemu iliyobaki ya nchi na kuiacha kama kumbukumbu, na hilo ni usaliti mkubwa. Simamisheni vitendo hivi vya kisiasa ambavyo vinalenga umoja wa nchi, simamisheni mfululizo wa utengenezaji wa wanamgambo wa ndani au wanaohusishwa na mafunzo na nchi za kigeni.
Kuhusu suala la raia wa dola ya Kiislamu; haki zao na wajibu wao, na uhusiano wao na nchi za kigeni, ni suala la kisheria, na Uislamu mkuu una maelezo wazi ndani yake; kwani hairuhusiwi raia kufanya kazi ya mtawala, si ndani wala nje, isipokuwa kwa uteuzi halali, kama vile Khalifa wa Waislamu, kwa sababu yeye ndiye anayehusika na kusimamia masuala ndani na nje, kwa kauli yake ﷺ: «…Kwa hakika imamu aliye juu ya watu ni mchungaji naye ataulizwa juu ya kundi lake», au kwa yule ambaye Khalifa amemteua, miongoni mwa wasaidizi, magavana na wengineo.
Dola ya Khilafah Rashida itakaposimamishwa hivi karibuni kwa idhini ya Mungu, wakati huo hakuna mtu atakayeruhusiwa kukutana na wakuu wa nchi za kigeni, au kuwa na uhusiano na nchi ya kigeni. Ilikuja katika rasimu ya katiba ya dola ya Khilafah ambayo Hizb ut-Tahrir iliwasilisha kwa umma, kifungu (182): (Hairuhusiwi kwa mtu yeyote, chama, kundi, au jumuiya kuwa na uhusiano na nchi yoyote ya kigeni kabisa, na uhusiano na nchi ni wa serikali pekee, kwa sababu yenyewe ndiyo ina haki ya kusimamia masuala ya umma kivitendo, na umma na makundi lazima iawajibishe serikali kwa uhusiano huu wa nje).
Enyi watu wa Sudan, je, tunachowalingania kwacho ni bora au ukweli huu mbaya mnaoishi ndani yake?!
Je, haijafika wakati kwenu kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir; mwanzilishi ambaye hawadanganyi, kuanzisha Khilafah Rashida ya pili kwa misingi ya Utume? Ni yenyewe pekee ndiyo inayolinda taasisi ya dola, na kuifanya iwe na heshima, ili isiruhusu nchi nyingine yoyote kuingilia mambo yake, au kufungua njia za mawasiliano na raia wake, kwani yote hayo ni uhalifu mkubwa na hatari kwa taasisi yake.
﴿Enyi mlio amini! Itikieni wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye jambo lenu lenye uhai. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika mtakusanywa kwake﴾.
Jumatatu 10 Safar 1447 AH
04/08/2025 AD
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Rada
