
14/7/2025
Rada: Hizb ut-Tahrir Yatoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari Kwamba Uhalifu wa (Tisa Ndefu) Hautaangamizwa Isipokuwa kwa Kutumia Hukumu za Kisharia Chini ya Dola ya Khilafa
Mwandishi wa habari wa tovuti ya Kush News, Habiba Al-Amin, alishambuliwa vikali na watu wanaohusishwa na genge la "Tisa Ndefu", katika eneo la Transit katika mji wa Port Sudan, alipokuwa akirejea kutoka kwenye taarifa za vyombo vya habari, akiandamana na idadi ya wenzake. Hili ni tukio moja tu kati ya matukio mengi ya uporaji, wizi na mauaji, ndani ya miji ambayo inapaswa kuwa salama, kama ilivyo huko Omdurman na Khartoum, na sasa katika mji mkuu wa utawala, Port Sudan, miji hii iko chini ya udhibiti wa serikali, na vyombo vyake vya usalama.
Lakini wahalifu wanashambulia kwa ujasiri wote, kana kwamba wana uhakika kwamba mkono wa serikali hautawafikia, na hata ukiwafikia, wana uhakika, kwa sababu ya udhaifu wa adhabu ya kuzuia, licha ya ukubwa wa uhalifu uliofanywa.
Hakuna mtu anayetofautiana kwamba kuenea kwa uhalifu hawezi kuzuiwa isipokuwa kwa kuanzisha hukumu za Kisharia, kwa sababu kanuni ya Kisharia ni kwamba (Mipaka ni ya kuzuia na ya kufidia); ni kuzuia kufanya uhalifu, na msamaha kwa wale ambao hukumu inatumika kwao, kulipia adhabu ya Akhera.
Kutoka kwa Abdullah bin Omar, alisema: "Nabii ﷺ alikata mkono kwa ngao yenye thamani ya dirhamu tatu" Imesimuliwa na Ibn Majah, na neno ni lake, na imesimuliwa na Bukhari na Muslim. Na katika riwaya: "Kwamba Nabii ﷺ alikata mkono wa mtu aliyeiba ngao kutoka kwenye safu ya wanawake, thamani yake ilikuwa dirhamu tatu" Sahih Abu Dawood, al-Nasa'i na wengineo.
Ama wale wanaowatisha watu salama, na kufanya mauaji, unyang'anyi, uporaji na wizi, kwa nguvu ya silaha kama ilivyo kwa (Tisa Ndefu), aya tukufu zimewajia kuwazima na kuwazuia, Mwenyezi Mungu alisema: ﴿Hakika malipo ya wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya bidii katika ardhi kufanya uharibifu ni kuuliwa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa kupingana au kufukuzwa katika ardhi. Hiyo ni fedheha kwao katika dunia, na katika Akhera watapata adhabu kubwa﴾, lau serikali ingechukua hatua na kutumia adhabu moja tu ya mipaka ya Mungu, wahalifu wote wangetatizika, lakini inaonekana kuwa ni heshima ambayo haistahili, kwa hivyo tunaona inajizungusha ikidhani kwamba kumteua waziri wa mambo ya ndani, au kupeleka polisi katikati ya nchi, au kuandaa kampeni za kuzuia, itafanya tofauti, lakini hali inazidi kuwa mbaya.
Hukumu za Kisharia hazitumiki isipokuwa chini ya dola ya Kiislamu; Khilafa Rashidah juu ya mfumo wa unabii, yenyewe ndiyo inayowazuia wahalifu, na kuwazuia. Ama mifumo ya kidemokrasia huzaa wahalifu, na hata kutengeneza uhalifu, na kulea rushwa, kwa sababu ya udhaifu wa adhabu zao, wanafikiri wao ni wenye huruma zaidi kwa watu kuliko Muumba wao, na hakuna dhambi baada ya ukafiri.
Je, watu wa nguvu na ulinzi katika nchi yetu wataitikia wito wa Mwingi wa Rehema, na kuipa Hizb ut-Tahrir ushindi, ili kufunga ahadi halali kwa Khalifa Rashid, anayeanzisha haki, kueneza usalama, na kuwazuia wahalifu; wakubwa wao kabla ya wadogo wao, kwa mujibu wa kauli yake ﷺ: «Hakika Imamu ni ngao ambayo inapiganiwa nyuma yake na kuogopwa»?!
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye lile linalo kuhuisha﴾.
Jumatatu, 19 Muharram Al-Haram 1447 AH, 14/07/2025 AD
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika jimbo la Sudan
Chanzo: Rada
