
8-11-2025
Rada: Kuanguka kwa Al-Fashir kunaharakisha mpango wa Marekani wa kuitenga Darfur
*Imeandikwa na Ustadh/Abdullah Hussein (Abu Muhammad Al-Fatih)*
Asubuhi ya Jumapili tarehe 26/10/2025, Vikosi vya Msaada wa Haraka vilitangaza udhibiti wao wa Al-Fashir, baada ya kuzingirwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, ambayo inamaanisha kuenea kwa ushawishi wao juu ya majimbo yote matano ya Darfur, na kugawanya nchi kati ya mashariki inayodhibitiwa na jeshi la Sudan, na magharibi chini ya udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka. Hivyo, inakuwa wazi kwamba udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka juu ya Al-Fashir ni zaidi ya ushindi katika vita dhidi ya jiji, lakini ni udhibiti juu ya eneo lote kwa njia ya kushangaza.
Maendeleo haya katika eneo la tukio la kuanguka kwa Al-Fashir baada ya kujiondoa kwa jeshi la Sudan, yaliambatana na mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Marekani kati ya wajumbe wa pande mbili, serikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka huko Washington kwa lengo la kusitisha mapigano. Ni wazi kwamba Marekani ndiyo iliyoamuru uongozi wa pande hizo mbili, kutekeleza kuingia kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka huko Al-Fashir, na kujiondoa kwa jeshi kutoka huko, ili kuharakisha mpango wa Marekani wa kuitenga Darfur, kama sehemu ya mpango wa kuigawanya Sudan katika mataifa madogo!
Katika karatasi ya Marekani iliyojadiliwa katika mkutano wa Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush, na washauri wake mwanzoni mwa muhula wake wa pili mwaka 2005 kujadili karatasi ya kazi kuhusu Mashariki ya Kati, karatasi hiyo inazungumzia Sudan, na kuhusu matukio matatu ya baadaye, ambayo hayakatai uwezekano wa kuigawanya Sudan katika mataifa matatu kama ifuatavyo:
* Misri ina uhusiano na moja yao kaskazini.
* Na Marekani ina uhusiano wa kimkakati na nyingine kusini.
* Na taasisi ya Kiyahudi ina uhusiano na taifa ambalo linaweza kuzaliwa magharibi mwa Sudan (Darfur)
Mkakati na diplomasia iliyopendekezwa ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati ilikuwa kwamba mawazo yanaandaliwa na kutayarishwa, kisha marais na viongozi wa nchi za Mashariki ya Kati wanaitwa Ikulu ya White House, ili kuyakubali na si kuyachunguza au kuyarekebisha, na kinachotakiwa ni makubaliano, na viongozi wa nchi katika eneo hilo, juu ya njia au njia bora ambayo mawazo haya ya kisiasa, au mipango ya kidiplomasia inaweza kutekelezwa kupitia mashauriano ya awali katika mfumo wa nchi mbili kisha katika mfumo wa pamoja. Hii ndiyo sera ya Marekani kuelekea nchi za Waislamu kwa ujumla na Sudan haswa; kuweka mipango ya kuigawanya mipaka ya damu na kufanya kazi ya kuitekeleza kupitia watawala na mazingira ya kisiasa na uuzaji wa vyombo vya habari kwake.
Kwa hiyo, amri za Marekani zilikuwa wazi kutumia kila linalowezekana kwa udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka juu ya Al-Fashir na kuuangusha, na kwa hiyo vikosi hivi vilifanya mauaji ya watu wasio na hatia na kumwaga damu nyingi katika ardhi ya Al-Fashir na miji mingine ya Sudan huku uongozi wa jeshi ukishindwa kutimiza wajibu wake katika kulinda Al-Fashir na watu wake na kuiacha itekwe na Vikosi vya Msaada wa Haraka wahalifu kwa picha mbaya zaidi zinazoweza kusimuliwa, na kila kinachotoka kwa matamko na mazungumzo na majuto juu ya mauaji ya Al-Fashir kutoka kwa Marekani na zana za kikanda na za ndani ni kujificha ukweli na njama iliyokubaliwa.
Kinachotakiwa kutoka kwa watu wa Sudan kwa ujumla ni ufahamu juu ya ukweli na ukatili wa Marekani na zana zake za kikanda na za ndani ambazo zinaimba amani na kwa kweli zinaleta uharibifu na mauaji kwa nchi za Waislamu katika utekelezaji wa mpango wa mipaka ya damu.
Na ufahamu pia juu ya mradi wa ukombozi kutoka kwa mipango ya Marekani na Magharibi ya kikoloni ya kuzimu; mradi wa Khilafa ambao unategemea umoja wa dola na umoja wa umma, na kujiunga na kazi na Hizb ut-Tahrir kiongozi ambaye watu wake hawadanganyi ambaye anafanya kazi hii usiku na mchana na kupaza sauti yake kwa sauti ya juu kupitia majukwaa mbalimbali, bali anafanya kampeni kubwa kwa zaidi ya miezi miwili akionya dhidi ya kuanguka kwa Al-Fashir na lengo la Marekani limetimia.
Vijana wa Hizb na uongozi wake hawataacha na wala hawata choka katika kuendeleza kazi yao kwa ajili ya Allah mpaka ahadi ya Allah Mtukufu itimie na bishara ya mpendwa wetu Muhammad ﷺ itimie; ﴿Allah amewaahidi wale ambao wameamini miongoni mwenu na wametenda matendo mema kwamba atawafanya makhulifa katika ardhi kama alivyowafanya makhulifa wale waliokuwa kabla yao, na atawawezesha Dini yao ambayo amewaridhia, na atawabadilishia baada ya hofu yao amani. Wananiabudu Mimi wala hawanishirikishi na chochote. Na watakao kufuru baada ya haya, basi hao ndio wapotofu.﴾, na Imam Ahmad amesimulia katika Musnad kutoka kwa Hudhaifa, akisema: Mtume wa Allah ﷺ alisema: «Utume utakuwa miongoni mwenu kwa muda ambao Allah anataka uwe, kisha atauinua atakapopenda kuuinua, kisha kutakuwa na Khilafa juu ya njia ya Utume, itakuwepo kwa muda ambao Allah anataka kuwepo, kisha ataiinua atakapopenda kuiinua, kisha kutakuwa na ufalme wa kuuma, utakuwepo kwa muda ambao Allah anataka kuwepo, kisha atauinua atakapopenda kuuinu, kisha kutakuwa na ufalme wa kidhalimu, utakuwepo kwa muda ambao Allah anataka kuwepo, kisha atauinua atakapopenda kuuinu, kisha kutakuwa na Khilafa juu ya njia ya Utume».
Chanzo: Rada
