
20/7/2025
Rada: Neno la Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan Katika Mkutano na Waandishi wa Habari Leo huko Port Sudan
Neno la Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Jumamosi 19/7/2025 BK huko Port Sudan
"Hakuna serikali inayotoa matumaini isipokuwa chini ya Uislamu na dola yake ya Khilafah"
Mkuu wa Baraza la Utawala, Abdel Fattah Al-Burhan, alitoa agizo, Jumatatu tarehe 19/05/2025, la kumteua afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kamel Idris, kuwa Waziri Mkuu, kuunda serikali ya wataalamu, kama vile Al-Burhan alivyotoa siku hiyo hiyo agizo la kufuta agizo la awali, linalohusiana na usimamizi wa wanachama wa Baraza la Utawala juu ya wizara za shirikisho, na vitengo vya serikali.
Kupitia ufuatiliaji wa uundaji wa serikali kwa uteuzi wa mawaziri kwa awamu, katika kipindi cha miezi miwili kamili, tunaona kwamba serikali imebadilika ngozi, kutoka serikali ya wataalamu iliyotangazwa na Waziri Mkuu, hadi serikali mseto; mchanganyiko wa wataalamu, na mgao kwa washirika wagomvi, wanaogombea wizara za mapato; fedha, madini, na ustawi (wa kijamii); lango la misaada na misaada ya kigeni, nao hawaoni haya. Kamel Idris alifanya kauli mbiu ya serikali yake kuwa ni matumaini, ambapo alisema katika hotuba yake ya televisheni tarehe 19/06/2025 kwamba kauli mbiu ya serikali yake ni "Matumaini" na ujumbe wake ni "Kufikia usalama, maisha mazuri na ustawi kwa watu." Anataka kufikia malengo haya kwa mfumo huo huo wa utawala wa kidemokrasia wa kilimwengu, ambao umekuwa ukitumika kwetu katika nchi yetu hii, tangu kuingia kwa majeshi ya kafiri mkoloni Kitchener nchini Sudan mwaka 1898 BK hadi tarehe yake, na umeshindwa kufikia chochote kati ya ujumbe wa serikali ya matumaini hapo juu, bali ni mfumo huo huo ambao umetupotezea usalama, na ndani yake heshima zimevunjwa! Kukata tamaa kumeenea, na dari ya maisha imepungua hadi hamu ya mwanadamu imekuwa ni kuendelea kuishi bila tamaa wala motisha, na kinyume chake tunawapata washirika wa Kamel Idris, ambao waliletwa na makubaliano ya Juba, wanatoa madai ya ubaguzi, na wanawadanganya watu wa kawaida, wakichanganya mchanganyiko bayana kati ya kukaa kwao katika viti vya wizara, na kuondoa dhuluma kwa wanaodhulumiwa pembezoni mwa nchi na katikati yake. Kituo cha Al-Sharq kiliripoti kutoka kwa Katibu wa Kisiasa wa Harakati ya Haki na Usawa, Mutasim Ahmed Saleh, akisema: (Picha ya pande za amani kushikamana na haki zao za wizara kulingana na maandishi ya makubaliano kama unyang'anyi wa kisiasa, ni usomaji potofu na wenye upendeleo, unaolenga kuwatisha pande hizi na kudhoofisha mradi wao, ili kuimarisha utawala wa wasomi wa kati, na kunyima nguvu za pembezoni ushirikiano wa haki katika kufanya maamuzi).
Ni lazima kwa pande zote mbili; wataalamu wakiongozwa na Kamel Idris, na harakati za kinachoitwa mapambano ya silaha, ni lazima wao watambue kwamba utawala katika Uislamu si keki ambayo mmiliki wake anafurahia mamlaka na utajiri, na anaomba kuketi kwenye kiti cha mamlaka kwa ahadi za uongo kwa waliotengwa au kwa wengine, ﴿ANAWAHIDI NA KUWATAMANISHA, NA SHETANI HAWAHIDI ILA UGHURI﴾, ahadi hizi za usalama, elimu, afya, na nyinginezo, na ahadi hizo kwa waliodhulumiwa katika pande za dola, ambao wanawaita (watu wa pembezoni), yote hayo ni hoja kwa serikali hii ya matumaini, na uzoefu wa watu wa nchi umeonyesha, kwamba kila anayeketi katika kiti cha utawala na anafikiria kuwa ni faida na keki, basi mawazo yake haya yamemwangusha, kwa sababu kuna tofauti kubwa kati ya anayetaka kusimamia masuala ya watu; kama jukumu na amana, na Siku ya Kiyama aibu na majuto, na kati ya aliyekuja kufurahia keki, na mamlaka na utajiri.
Ama madai ya pembezoni, ambayo yanatolewa na kila mshirikiana na nje, mwasi dhidi ya mamlaka ya dola, yana maana ya dhuluma zinazowapata raia wa dola katika pande zake, ambazo sababu yake ni mfumo wa Magharibi kafiri mkoloni mwenyewe, ambaye hamuandama kila anayebeba silaha kwa ajili ya kubadilisha mfumo huu dhalimu, bali kwa ajili ya kuchukua mgao ili kuutumia na kuutekeleza, yaani kuendelea kuwadhulumu watu wa pembezoni kwa mikono yao wenyewe si kwa mkono wa Amru!
Hakika mamlaka katika Uislamu; yaani haki ya kuchagua mtawala na kumsimika, ni kwa ajili ya Umma pekee au anayemwakilisha, nayo inatoa haki hii kwa anayejiona kuwa anastahiki jukumu hili la jumla, kwa kuwa na nguvu, mcha Mungu, mpole kwa raia, asiyekera, hizi ni sifa za mtawala katika nafsi yake binafsi, na ama katika uhusiano wake na raia, ni lazima awazungushe kwa nasaha zake, na asiguse mali ya umma, na awatawale kwa Uislamu pekee. Hizi ni saba kamili zikikusanyika katika mtawala maisha yatanawiri, na hali ya watu itakuwa nzuri, basi wapi wataalamu na harakati ziko kutoka kwazo?!
Hakika picha ya Kamel Idris ya serikali yake, kama serikali ya matumaini kwa watu wa Sudan, ambao kiwango cha chini cha matumaini yao ni serikali inayoshughulikia matatizo yao, na inaboresha maisha yao hadi kiwango cha kuishi mwanadamu, kwa kuhakikisha kukidhi mahitaji yao ya msingi kwa mtu binafsi: (chakula, mavazi na makazi), na kuhakikisha kukidhi mahitaji ya msingi ya jamii ambayo ni (usalama, elimu, na matibabu), na kile kinachohitajika kwa ajili ya hayo kutoka katika kutoa maji safi, umeme, na miundombinu; kutoka katika mitandao ya mawasiliano, barabara, madaraja na vinginevyo, na kile kinachohitajika kwa ajili ya hayo yote kutoka katika kusimamisha uporaji wa mali za nchi, na kurudisha pesa za mali za umma kwa wamiliki wake, na nguzo ya hayo yote ni kung'oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka nchini kwetu. Hiki ndicho kinachotoa matumaini kwa watu wa Sudan, na ambacho serikali ya Kamel Idris haiwezi kukifikia.
Kwa nini? Kwa sababu kushughulikia tatizo lolote kunahitaji kujua sababu zake zilizosababisha kutokea kwake, kisha kuchukua tiba inayolenga sababu za tatizo, na kwa kufanya hivyo tiba itakuwa ya kimsingi. Je, Kamel Idris amekuja, akiwa amebeba katika mfuko wake tiba inayotoa matumaini? Au amekuja akiwa amebeba sababu za tatizo, baada ya kuzipamba mikono ya muuza dawa?!
Hakika watu wa Sudan ni Waislamu, na Uislamu Mkuu ndio dini ambayo alikuja nayo Bwana wetu Muhammad ﷺ, wahyi kutoka kwa Muumba Mtukufu, na Uislamu huu ambao unafuatwa na watu wa Sudan ni dini na kwake ndio dola, itikadi na mifumo kamili ya maisha hadi Siku ya Kiyama, Anasema Mtukufu: ﴿LEO NIMEWAKAMILISHIENI DINI YENU NA NIMETIMIZA NEEMA YANGU JUU YENU NA NIMERIDHIKA KUWENI UISLAMU KUWA DINI YENU﴾, Uislamu huu ndio haki, isipokuwa kwamba Magharibi kafiri mkoloni, ambaye ameshinda raundi ya mwisho katika mgogoro kati ya haki na batili, ameiharibu dola ya Waislamu; Khilafah, na amewasimamishia Waislamu nchi za kitaifa za kiutendaji, amewateua watawala vibaraka mafisadi, wanaolindwa na majeshi kutoka katika udongo wao; mamluki katika siasa, fikra, na vyombo vya habari, kazi yao yote ni kupambana na kurejea kwa Uislamu; tiba ya maisha, bali na kutumia mifumo ya bwana wao kafiri kwa Waislamu, nao wanagombana nani anayestahili zaidi kuitumia, wanajeshi au wataalamu au harakati za silaha?!
Sababu ya mgogoro ambao watu wa Sudan wanateseka nao, ni kutumika kwa mifumo ya Magharibi kafiri mkoloni ya kimitazamo; kutoka katika mfumo wa kidemokrasia katika utawala, na mfumo wa kibepari katika uchumi, unaorahisisha uporaji wa mali na kuwatumikisha watu wa nchi. Na hili ndilo ambalo Kamel Idris amekuja kulitutumia, ili afanye upya kamba ya utumwa kwa Magharibi kafiri kuzunguka shingo zetu, je, inatudhuru sisi kumtumia serikali ya wataalamu katika kutekeleza kazi yake, au harakati za silaha, au mamluki kutoka katika ulimwengu wa siasa?!
Hakika matumaini, na katika historia yote ya kibinadamu, hayazaliwi katika ulimwengu wa batili, wala udanganyifu, uongo na upotoshaji, bali matumaini huzaliwa daima pamoja na haki, ukweli na uaminifu, yanabebwa na manabii waliotumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuhitimishwa na Bwana wetu Muhammad ﷺ kwa ujumbe wa Uislamu Mkuu, unaobeba maelezo ya kutosha katika itikadi, na mifumo ya maisha katika utawala, uchumi, jamii, sera ya elimu, na sera ya kigeni, Waislamu wenye mamlaka hufanya, au anayewawakilisha kutoka katika watu wenye nguvu na ulinzi, wanafanya katika mfumo huu bay'ah kwa mtu kutoka kwao kuwa Khalifa wa Waislamu, na wakati huo mfumo wa Khilafah unakuwa umesimama, na matumaini yanazaliwa katika maisha ya heshima chini ya Uislamu, kwa yafuatayo:
Kwanza: Khalifa ataikunja ukurasa wa mwisho wa kuishi kwa Waislamu kwa mifumo ya kimitazamo iliyoagizwa, yeye na wataalamu wake wa kuitumia kutoka Magharibi kafiri, na ataanza kutumia mifumo ya Uislamu, iliyochukuliwa kutoka katika wahyi kwa nguvu ya dalili.
Pili: Khalifa ataanza mara moja kuwateua wasaidizi, watawala na viongozi wengine, au wale anaowatumia, na ataanza mara moja kushughulikia matatizo ya raia, mbali na mgao wowote, kwani mamlaka kisheria ni ya Umma, na si kwa anayebeba silaha na kushirikiana na nje.
Tatu: Khalifa wa Waislamu ataondoa ushawishi wa Magharibi kafiri kutoka nchini kwetu, na atasafisha taasisi za dola kutoka katika vyombo vyake, na atachukua utajiri wa Umma wa kiakili, na utajiri wake wa kimwili, ngazi ambayo anapanda kwayo ili kuwa dola ya kwanza duniani kama ilivyokuwa hapo awali, na kwa muda wa miaka mia sita iliyopita.
Nne: Uislamu unaotumiwa na Khalifa wa Waislamu, utalisafisha mazingira ya kisiasa kutoka kwa vibaraka na vyombo vya Magharibi kafiri mkoloni, na kutoka kwa hotuba ya ubaguzi wa rangi, na madai ya kijahiliya ambayo yanawagawa raia wa dola, na wakati huo wazo la kusimamia masuala ya raia wote kwa uadilifu na ihsani litatosha kutatua madai ya ubaguzi na istilahi nyinginezo ambazo zimezaliwa kutokana na kuishi chini ya mifumo ya Magharibi kafiri.
Tano: Khalifa wa Waislamu atafanya nguvu ya silaha katika dola kuwa nguvu moja, inayoongozwa na Khalifa wa Waislamu, na atasimamisha uundaji usio na maana wa wanamgambo wapya kila asubuhi mpya, bali baya zaidi na kubwa, baadhi yao wanafundishwa katika nchi za nje! Kisha tunatarajia matumaini na maisha mazuri, chini ya vivuli vya nguvu hizi za silaha nyingi!
Huu ni sehemu ndogo ya hukumu za Uislamu, tunapotoa mradi kwa Umma ambao unaweza kutoa matumaini katika maisha mazuri, na siku utakapowekwa mahali pa utumiaji na utekelezaji, maisha yetu yatabadilika kabisa, kisha matumaini yatafuata kitendo kinachotupeleka kwenye kufikia kilele cha utukufu kama tulivyokuwa hapo awali, na hilo kwa Mwenyezi Mungu si gumu.
Anasema Mtukufu: ﴿ENYI MLIOAMINI ITIKIENI WITO WA MWENYEZI MUNGU NA MTUME ANAPOKUITENI KWENYE YANAYOKUHUISHA﴾.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan
Chanzo:Rada
