
24/6/2025
Rada: Muhammad Jami' (Abu Ayman) Anaandika.. Kwa vita Sudan na utekelezaji wa mpango wa mmomonyoko polepole
Katika ripoti ya Sudan Tribune ya Jumatano 2025/6/18 kwa kichwa: "Vita vya Jangwa na Mipaka vinazusha Sudan na kuchochea hofu ya uingiliaji wa kigeni", ilisomeka: "Udhibiti wa Kikosi cha Msaada wa Haraka wa eneo la Jebel Uweinat na pembetatu ya mpaka wa kimkakati kati ya Sudan, Misri na Libya, uliwakilisha mwelekeo tofauti katika suala la kuweka msingi na kupata vifaa."
Vita nchini Sudan kati ya jeshi na Kikosi cha Msaada wa Haraka vimemaliza mwezi wake wa tatu wa mwaka wake wa tatu bila kukata uamuzi kwa upande wowote, badala yake, ni wazi kwamba pande hizo mbili zinashindana katika kumiliki maeneo mapya na kujiondoa kutoka kwa mengine kwa njia ya kutiliwa shaka na ya kushangaza, kama ilivyo katika hali ya kujiondoa kwa Kikosi cha Msaada wa Haraka kutoka Khartoum na kisha kumiliki mji wa Al-Nuhud na idadi ya miji ya Kordofan Magharibi, na kujiondoa kwa jeshi kutoka humo na kutoka idadi ya miji na majimbo, la mwisho likiwa pembetatu ya mpaka wa kimkakati kati ya Sudan, Misri na Libya.
Lakini kuna swali ambalo limeendelea kuwa akilini mwa watu wa Sudan: Kwa nini viongozi wa jeshi hawataki kukata uamuzi katika vita hivi?! Na uhusiano wa hiyo ni nini na vita vya kizazi cha nne au cha tano?!
Imekuwa wazi kwa kila mfuatiliaji kwamba vita hivi vina ajenda maalum ambayo inaonyeshwa na uondoaji wa kutiliwa shaka na kutofungua hatamu ambayo wanajeshi wameiomba mara kwa mara, lakini haikupata masikio ya kusikia kutoka kwa viongozi wanaohusishwa na Amerika haswa.
Hiyo ni kwa sababu vita vinalenga mpango mchafu wa Amerika wa kupiga ushawishi wa Uingereza unaowakilishwa na vikosi vya kiraia vinavyoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Abdullah Hamdok, na kisha mradi wa kugawanya Sudan unaoendelea huko Darfur kwa kasi, Mungu na aharibu mpango wao na kukatisha tamaa matumaini yao. Na yote yanayotokea yanaelezea kuongezwa muda wa vita licha ya ukosefu wa sababu za kushawishi za kuzuka kwake, au kuendelea kwake kwa njia na mitindo mbalimbali. Lakini Profesa Max Manwaring, mtaalam wa mkakati wa kijeshi katika Taasisi ya Mafunzo ya Chuo cha Vita vya Amerika, alielezea hilo katika mhadhara ulioenea kwenye YouTube ambao maafisa wakuu kutoka NATO na jeshi la Wayahudi walialikwa mwaka wa 2018 BK.
Ambapo mhadhara huo unafichua kile kinachoendelea nchini Sudan kutokana na mgogoro kati ya raia na wanajeshi, na kutokana na mapigano kati ya jeshi na Kikosi cha Msaada wa Haraka.
Profesa Max alianzisha mhadhara wake kwa kusema kwamba "njia ya vita vya jadi imepitwa na wakati, na mpya ni kizazi cha nne cha vita"!!
Na alisema haswa: "Lengo sio kuvunja taasisi ya kijeshi ya taifa lolote, au kuharibu uwezo wake wa kijeshi, lakini lengo ni uchovu na mmomonyoko polepole, lakini kwa uthabiti. Kwa hivyo lengo letu ni kulazimisha adui kujisalimisha kwa mapenzi yetu"! Na anaongeza: "Lengo ni kuyumbisha utulivu", "Na kuyumbisha huku kunatekelezwa na raia kutoka nchi adui kuunda taifa lililoshindwa .. Hapa tunaweza kudhibiti .. Na mchakato huu unatekelezwa kwa hatua .. polepole na kimya kimya na kwa kutumia raia wa nchi ya adui, kwa hivyo adui yako ataamka akiwa amekufa ..."!
Na kinachovutia zaidi katika mhadhara huu ni msemo: "Uchovu, na mmomonyoko polepole". Na mmomonyoko polepole unamaanisha kueneza uharibifu na machafuko katika miji, na kuwageuza watu kuwa makundi yanayotangatanga, na kulemaza uwezo wa nchi adui wa kukidhi mahitaji ya msingi .. ambapo anasema "Katika aina hii ya vita unaweza kuona watoto waliokufa au wazee, kwa hivyo usisumbuke"!
Na anasema: "Mkakati wa uchovu unamaanisha kuhamisha vita kutoka mstari mmoja hadi mwingine, na kutoka ardhi moja hadi nyingine, na kumaliza uwezo wote wa nchi adui katika hatua tofauti, na kufanya "nchi adui" ipigane kwenye mistari mingi iliyozingirwa na fisi wa ndani kutoka pande zote, na kupanga joto la mstari mmoja na kupunguza mstari mwingine, ambayo ni, kuendelea kusimamia mzozo na sio kuutatua" mwisho wa nukuu.
Na hili ndilo linalotokea sasa katika vita vya Sudan; kuna fisi, mbweha na nyoka wanaoendesha vita na hawataki vita hivi viishe hadi watimize ajenda yao ya Amerika; kwani hiyo inatekelezwa na mawakala wa Amerika kutoka kwa viongozi wa vikosi vya jeshi katika jeshi na Kikosi cha Msaada wa Haraka.
Na kutokwa na damu hii kwa nchi hakutaacha isipokuwa watu wa Sudan watatambua mpango huu mbaya wa uhalifu na kuwazuia mawakala hawa na kukata ushawishi wa Amerika na nchi zingine za kikoloni, na hiyo haitakuwa isipokuwa kwa kuanzisha dola ya Khilafa iliyoongoka kwa misingi ya unabii. Na hii ni wajibu wa viongozi waaminifu katika jeshi nchini Sudan; kupiga kwa nguvu za chuma mawakala na kuwapa ushindi waaminifu kutoka kwa watu wa umma ili kuanzisha dola ya Khilafa iliyoongoka kwa misingi ya unabii, kwani ndani yake kuna njia ya kutoka na ukombozi. Kutoka kwa Al-Arbad bin Sariya kutoka kwa Nabii ﷺ alisema: «Kwa hakika yeyote kati yenu atakayeishi ataona tofauti nyingi, kwa hivyo lazima ufuate Sunnah yangu na Sunnah ya Makhalifa Walioongoka, shikamaneni nayo kwa magego» Imesimuliwa na Abu Dawood, na Ahmad.
Na ni lazima ujue kwamba kuanzisha Khilafa ni wajibu, na anayekawia kuianzisha ni mwenye dhambi. Kutoka kwa Abdullah bin Omar, Mwenyezi Mungu awaridhie, kutoka kwa Nabii ﷺ alisema: «Na yeyote anayekufa na hana ahadi ya utiifu shingoni mwake, amekufa kifo cha ujinga» Imesimuliwa na Muslim.
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Jami' (Abu Ayman)
Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Jimbo la Sudan
Chanzo: Rada
