
24/6/2025
Rada: Hotuba ya Kisiasa Katika Jiji la Port Sudan:
(Uislamu Umeitatuaje Tatizo la Kupanda kwa Bei)
Rada News Chini ya kichwa hiki, Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan leo Jumatatu tarehe 27 Dhul-Hijja 1446 Hijria, ambayo inalingana na 23/06/2025 Miladia, ilitoa hotuba yake ya kisiasa ya kila wiki, mbele ya Hoteli ya Haramain katika Soko Kuu katika jiji la Port Sudan.
Mzungumzaji, Profesa Muhammad Jami Abu Ayman, alizungumzia tatizo la kupanda kwa bei ambalo watu wa Sudan wanakumbana nalo, na jinsi gani si hivyo tu bali binadamu wote wanakumbana na kupanda kwa bei kutokana na udhibiti wa mifumo ya kibepari ya kidemokrasia iliyopo duniani, na jinsi inavyosababisha kupanda kwa bei kiasi kwamba watu wengi hawawezi kupata bidhaa na huduma. Kisha akaeleza hadithi: (Mwenye kuingilia bei za Waislamu ili awapandishie, ni haki kwa Allah kumketisha kwenye bonde la moto Siku ya Kiyama), na akaorodhesha mambo ambayo yanaweza kusababisha kupanda kwa bei, ambayo tayari yamesababisha kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma, na jinsi Uislamu ulivyoyashughulikia, ambayo ni kama ifuatavyo:
1/ Ukiritimba: Uislamu umekataza ukiritimba, na mzungumzaji alieleza kwa kina athari yake kubwa katika kupandisha bei na kwamba Uislamu umeharamisha kitendo hiki kiovu: (Hakuna anayefanya ukiritimba ila ni mwenye makosa).
2/ Kodi za aina zote mbili, za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, na jinsi mnunuzi anayedhulumiwa ndiye anayezi lipa kodi hizi ambazo nchi zinazotumia mifumo ya kibepari ya kidemokrasia huchukua kutoka kwa bidhaa na huduma, na huchukua bila haki ya kisheria.
3/ Ushuru wa forodha, kwani kila mtu anahisi athari yake katika kupanda kwa bei, na akaeleza kuwa Uislamu umeharamisha, kwani Amani na baraka za Allah zimshukie alisema: "Haingii Peponi mwenye kutoza ushuru haramu" na ushuru haramu ni forodha kama alivyoashiria Abu Ayman kwa hadithi ya Al-Ghamidiyah: (Alikuja Al-Ghamidiyah akasema: Ee Mtume wa Allah, nimezini, na ninataka unitakase. Akamrudisha, na siku ya pili akamjia, akasema: Ee Nabii wa Allah, kwa nini unanirudisha; labda unataka kunirudisha kama ulivyomrudisha Maiz bin Malik? Naapa kwa Allah mimi ni mjamzito. Akasema: Ikiwa sivyo, basi nenda mpaka uzae. Alipozaliwa alimjia na mtoto katika nguo, akasema: Huyu nimemzaa. Akasema: Nenda ukamnyonyeshe, mpaka umwachishe. Alipomwachisha, alimjia na mtoto, akiwa ameshika kipande cha mkate mkononi mwake, akasema: Huyu, Ee Nabii wa Allah, nimemwachisha, na amekula chakula. Akampa mtoto kwa mmoja wa Waislamu, kisha akaamrisha, akachimbiwa shimo mpaka kifuani kwake, na akaamrisha watu wampige mawe, na Khalid bin Al-Walid akakaribia na akampiga jiwe kichwani, damu ikamrukia usoni, akamtukana, Mtume ﷺ akasikia matusi yake, akasema: Acha, ewe Khalid, naapa kwa ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika ametubu toba ambayo lau angetubu mwenye kutoza ushuru haramu, Allah angemghufiria. Kisha akaamrisha, akamsalia, na akazikwa).
4/ Akiba, ambapo mzungumzaji alieleza kuwa akiba inazuia watu na pesa ambazo watu wote wanapaswa kuzitumia, na sio mali ya kikundi kidogo cha matajiri na wamiliki wa mitaji pekee…
Wahudhuriaji waliipongeza hotuba hiyo, baadhi yao walisema Takbir na Tahlil, na mmoja wao alisema: (Huu ni mada bora, na hatukusikia isipokuwa Allah amesema na Mtume amesema… Allah akulipe kheri).
Hatimaye, mzungumzaji aliwakumbusha wahudhuriaji juu ya wajibu wa kufanya kazi ya kuanzisha dola ambayo inatekeleza hukumu za Uislamu katika uchumi na katika mifumo mingine ya maisha, na kwamba Khilafah ndiyo dola iliyoanzishwa na mpendwa Mtume Muhammad ﷺ, na akafafanua kuwa ni Khilafah kwa njia ya Utume baada yake…. Kisha akatoa bishara ya ahadi ya Mola wetu Mlezi akisema: (Allah amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba atawafanya warithi katika ardhi kama alivyowafanya warithi wale waliokuwa kabla yao), na bishara ya Nabii wetu ﷺ akisema: (… Kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume).
Na Alhamdulillah Mola Mlezi wa walimwengu
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Rada
