
10-10-25025
Rada: Lini tutaacha kuingiliwa na Magharibi makafiri na mashirika yake ya kikoloni katika maisha yetu, na kuelekeza nyuso zetu kwa Mungu Mmoja, Mwenye hukumu?
Imeandikwa na: Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Chini ya udhamini wa shirika la Ufaransa la Promediation, vyama vya Sudan viliandaa warsha huko Port Sudan, kama ilivyo katika tovuti ya Sudan Tribune mnamo 5/10/2025 BK: (Msemaji wa kambi ya Demokrasia, Muhammad Zakaria, alisema kuwa warsha hiyo "inajadili jinsi ya kufanya mazungumzo ya Sudan na Sudan, pande zake, mahali pa mkutano, jukumu la upatanishi, na masuala ya ufadhili." Alieleza kuwa warsha hiyo itafuatiwa na hatua zingine kwa lengo la kufikia makubaliano kati ya idadi kubwa zaidi ya nguvu za kisiasa nchini, ili kufikia utulivu na kuepuka migogoro na mitafaruku hasi).
Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan, tunatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu ukweli huu:
Kwanza: Uislamu umekata kauli kuhusu suala la chanzo cha tiba ya matatizo ya maisha kwa njia ya uhakika, hivyo amejaalia mamlaka ya sheria pekee, hivyo haijuzu kwa Mwislamu kuchukua tiba ya tatizo lolote la maisha isipokuwa kutoka katika sheria, bali amejaalia jambo hilo kuwa ni sawa na imani, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿LA, NAAPA KWA MOLA WAKO, HAWATAAMINI HATA WAKUFANYE WEWE HUKUMU KATIKA YALE WANAYOTAFUTANA, KISHA WASIPATE VIGUGUMIZI KATIKA NAFSI ZAO KWA ULIYO HUKUMU, NA WAJISALIMISHE KABISA﴾; kwa hivyo chanzo cha tiba kimefungwa katika Uislamu, na si matamanio ya wanasiasa wanaokimbilia viti vya utawala.
Pili: Uislamu umewataka Waislamu wanapotofautiana katika jambo lolote, walirejeshe kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake ﷺ, si kwa nchi za kikoloni, wala mashirika yake ya uhalifu, kwani kurejesha jambo hilo katika Uislamu ni miongoni mwa mambo thabiti ya imani, Mwenyezi Mungu amesema: ﴿NA IKIWA MNATOFUTIANA KATIKA JAMBO LOLOTE, LIRUDISHENI KWA MWENYEZI MUNGU NA MTUME, IWAPO MNA MWAMINI MWENYEZI MUNGU NA SIKU YA MWISHO. HILO NI BORA NA ZURI ZAIDI MWISHO WAKE﴾.
Tatu: Kutegemea nchi za kikoloni za kikafiri zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, kama vile Ufaransa, Marekani, Uingereza na Urusi, na kutegemea uingiliaji wa mashirika yake ya uhalifu, kama vile Promediation, Taasisi ya Amani ya Marekani, Chatham House, na mengineyo, ni kujiua kisiasa na usaliti kwa umma, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ﴿Enyi mlio amini! Msiwafanye watu wa nje kuwa wasiri wenu, hawataacha kukufanyieni uovu, wanapenda mnateseke. Uadui umekwisha dhihirika vinywani mwao, na yale wanayo yaficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainisheni aya, ikiwa nyinyi ni wenye akili﴾.
Nne: Sheria ya Kiislamu imefanya uhusiano na nchi za kigeni, na mashirika yake kuwa ni wa dola pekee, na imemzuia mtu yeyote au kikundi chochote kuwa na uhusiano na nchi ya kigeni, au na shirika lolote la kigeni kabisa, kwani kuna hatari kubwa kwa umoja wa nchi na umma.
Tano: Uislamu una utajiri wa hukumu na matibabu kwa matatizo yote ya maisha, kwani siasa katika Uislamu ni kuhudumia maslahi ya watu, ndani na nje, na dola huitekeleza kivitendo, na ni kazi tukufu zaidi, bali ni kazi ya Mitume, kama alivyoeleza Mtume ﷺ aliposema: «WANAI WAISRAELI WALIONGOZWA NA MANABII, KILA NABII ALIPOKUFA ALIFUATWA NA NABII, NA HAKUNA NABII BAADA YANGU, NA WATAKUWEPO MAKHALIFA NA WATAKUWA WENGI,» WALISEMA: UNATUAMRISHA NINI? ALISEMA: «TIMIZENI AHADI YA WA KWANZA, NA WA KWANZA, NA WAWENDELEENI HAKI ZAO, KWANI MUNGU ATAWAULIZA KUHUSU YALE ALIYOWAKABIDHI» Ameitoa Muslim.
Hitimisho: Leo umma unahitaji mfumo wa Uislamu; Ukhalifa ulioongoka juu ya njia ya Utume, ambao unasimamisha dini, unatekeleza sheria, unaondoa ushawishi wa Magharibi makafiri wakoloni kutoka nchini kwetu, na unawafuata watu wa shaka miongoni mwa wanaowasiliana na balozi za Magharibi na mashirika yake, na unaufanya uhai kuwa wa Mungu mmoja, Mwenye hukumu. Na kwa ajili ya hili, na wafanye kazi wenye kufanya kazi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ﴿ENYI MLIO AMINI! MUITIKIENI MWENYEZI MUNGU NA MTUME ANAPOKUITENI KWENYE YALE YANAYOKUHUSHENI﴾.
* Msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Rada
