
17-10-2025
Rada: Watu wa Sudan watampata lini msaidizi wa haki wa kuwaokoa?
Imeandikwa na/Ghada Abdul Jabbar (Um Awaab)
Tovuti ya Sudan Tribune ilitangaza kuuliwa kwa raia wasiopungua 60 na kujeruhiwa kwa wengine wengi katika shambulio lililofanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka siku za Ijumaa na Jumamosi kwenye kituo cha kuwahifadhi wakimbizi katika mji wa El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, kulingana na mashuhuda na vyanzo vya matibabu.
Kikosi cha Msaada wa Haraka kimekuwa kikishambulia kwa mizinga na ndege zisizo na rubani malengo ya raia kwa siku kadhaa, na kusababisha uharibifu wa masoko, vyanzo vya maji na vifaa vya afya huko El Fasher, na pia mara kwa mara kushambulia maeneo ya mikusanyiko ya wakimbizi, ikifanya ukiukwaji mkubwa ikiwa ni pamoja na mauaji, kukamatwa na uhamishaji wa lazima.
Msemaji wa wakimbizi wa kambi ya Zamzam, Muhammad Khamis Douda, aliiambia Sudan Tribune kwamba "ndege isiyo na rubani iliyorushwa na Kikosi cha Msaada wa Haraka ilishambulia shule ya Dar Al-Arqam leo Jumamosi, na kusababisha vifo vya raia 37, baadhi yao walifariki kwa kuchomwa moto ndani ya madarasa." Douda alieleza kuwa kituo hicho hicho kilishambuliwa na mizinga siku ya Ijumaa jioni, kikilenga malazi ya chini ya ardhi ambayo wakimbizi walikuwa wakijikinga nayo, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 30.
Maoni:
Kikosi cha Msaada wa Haraka, ambacho kimeshindwa kuuteka mji wa El Fasher, kimekuwa kikiwalenga raia na kile kilichosalia cha miundombinu, hospitali, misikiti na malazi, ili kuwalazimisha raia waliosalia kuondoka katika mji huo muhimu na wa kimkakati, na kwa hivyo kinafanya uhalifu mbaya zaidi dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa mauaji ya halaiki, kwa kusikia na kuona mfumo wa kimataifa, lakini Magharibi makafiri chini ya uongozi wa Amerika, ambayo ilianzisha vita hivi, hawasongi kidole katika ushirikiano na kuficha uhalifu huo ambao unafanya uso uone haya, kwa sababu makundi yenye silaha nchini Sudan yanatumikia mradi wa Amerika wa kuitenga Darfur na mipaka ya damu na kuta za fuvu za watu wake wasio na hatia.
Wako wapi watiifu kutoka kwa wanajeshi? Je, haijafika wakati wao kuchukua hatua na kusimamisha michezo hii ya upuuzi ya Amerika na vibaraka wake ambayo imeharibu mazao na vizazi na kuandikwa mbele ya Mungu kama wasaidizi wa haki?
Ni kuanzishwa kwa Uislamu katika hatamu ya utawala kwa kuanzisha Ukhalifa kwa njia ya Utume tu ndiko kutakomesha uingiliaji wa kafiri mkoloni katika patakatifu petu na kung'oa ushawishi wake kutoka nchini mwetu, na bila ya hivyo, huu ndio umaskini unaoendelea! Mtume ﷺ anasema: "Hakika Imamu ni ngao, anapiganwa kutoka nyuma yake na watu wanajikinga naye."
Chanzo: Rada
