Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Njia ya kujiondolea hatia ya kuwaangusha watu wa Palestina
ni kufanya kazi usiku na mchana ili kusimamisha Khilafa Rashidah, na kuhamasisha vikosi vya jeshi
(Imetafsiriwa)
Kwa sababu ya kutochukua hatua kwa majeshi ya Waislamu kumnusuru Gaza, baba mwingine aliyedhulumiwa, Abu Omar, ameuawa akiwa anatafuta riziki kwa ajili ya watoto wake. Alipokuwa akisubiri msaada, risasi ya mpiga risasi Myahudi mwoga ilipenya kichwani mwake. Ama rafiki aliyerudisha mwili wake, alikuwa na njaa kwa siku tano, na alirudi kutoka kwenye mlango wa shahada, na huenda akafa shahidi hivi karibuni. Hili si tukio moja tu, bali makumi ya matukio kama haya kila siku yanashuhudiwa na umma wa watu bilioni mbili!
Maswali yenye uchungu hayazuiliwi kwa swali moja; ni mpaka lini mauaji ya watu waliodhulumiwa kutoka kwa wanaume, wanawake na watoto wa Palestina yataendelea? Mashahidi wangapi watapanda mpaka majeshi yachukue hatua? Ni mpaka lini dada zetu wataendelea kulia na kulalamika? Ni mpaka lini Wayahudi wataendelea kuponda roho za Waislamu, mali zao na heshima zao chini ya miguu yao? Ni mpaka lini tutabaki bila kusonga? Ni mpaka lini tutaishia tu kuwaombea waliodhulumiwa na kuwalaani madhalimu?!
Zaidi ya yote, Waislamu waliodhulumiwa huko Palestina watakaposimama Siku ya Kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu na kulalamika, si tu kwa watawala wa Waislamu na majeshi yetu, bali watatulalamikia sisi sote, basi tutajibu nini? Tulikuwa wapi wakati watoto wao walikuwa wanakufa, wakati walikuwa wanalia, kwa nini tulikuwa kimya? Mwenyezi Mungu atakapotuuliza kuhusu uzembe wetu katika kutimiza wajibu wetu wa kisheria, basi tutajibu nini? Je, dunia ilikuwa ya thamani zaidi kwetu kuliko Akhera? Je, mapenzi ya wazazi na watoto ndiyo yaliyotuzuia? Je, kazi zetu na biashara zetu zilituzuia kutekeleza amri yake Subhaanahu wa Ta'ala?
Kuna njia ya kuokoka aibu ya Siku ya Kiyama na majuto ya hesabu, na kujiandaa kwa ajili yake; tunapaswa kuvunja ukimya wetu na kuinua sauti zetu leo. Yeyote anayetaka kuokoka adhabu ya Siku ya Hesabu kali, basi anapaswa kudai kwa nguvu zote majeshi ya Waislamu kuchukua hatua mara moja kuwanusuru ndugu zao waliodhulumiwa huko Gaza, na kuwaondoa watawala na viongozi wa kijeshi ambao ndio kikwazo kikubwa katika njia ya jihadi ya kuwanusuru.
Enyi Waislamu wa Pakistan: Kimya na unyenyekevu mbele ya dhalimu mshambuliaji ni msaada kwake kuua aliyedhulumiwa, basi simameni na kuinua sauti zenu, watikiseni askari na maafisa waaminifu katika vikosi vya jeshi, na wakumbusheni wajibu wao wa kisheria.
Na waambieni kwamba Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta'ala ameamrisha akisema: ﴿Nendeni (vitani) mkiwa wepesi na wazito, na jihadini kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu﴾. Na waambieni kwamba Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta'ala amewalazimisha kuwanusuru Waislamu wa Palestina akisema: ﴿Na wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwanusuru﴾. Waambieni ikiwa hawapigani kutetea wanyonge miongoni mwa Waislamu huko Palestina wataulizwa, Mwenyezi Mungu Ta'ala amesema, ﴿Na mna nini hamkupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na (kuwaokoa) wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto﴾?
Wafikishieni maafisa na askari kwamba mfumo wa sasa umewafunga kwenye kambi, na kwamba kutoa nusra kwa Hizb ut-Tahrir ili kusimamisha Khilafa Rashidah kwa manhaj ya Utume ni faradhi ya kisheria kwao. Khilafa ndiyo inayounganisha umma chini ya bendera moja, na imamu mmoja, na nguvu moja. Na ndiyo inayowalinda watoto wa Abu Omar, na kulipiza kisasi kwa wauaji wake, na itawapa heshima ya kukomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na msikiti wa Mtume ﷺ, na mtastahiki uombezi wake enyi wana wa Muhammad bin al-Qasim. Kutoka kwa Abu Hurairah Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Allah ﷺ amesema: «Saa haitasimama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi na Waislamu watawaua...». Sahihi Muslim
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Pakistan