Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nyinyi Ndio Mnaowaangusha Waislamu kwa Njaa Enyi Masoud Pezeshkian!
Iran imetangaza kufilisika kwa benki yake kubwa zaidi ya kibinafsi, ambayo ni benki ya (Ayandeh), na benki hii ina matawi 270 nchini Iran, baada ya madeni yake kuongezeka hadi zaidi ya dola bilioni tano, na cha kushangaza ni ukosoaji wa Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, kuhusu kushindwa kwa utawala akisema: "Tuna mafuta na gesi lakini tuna njaa"!
Je, inawezekana kauli hii itoke kwa rais wa nchi ambayo inamiliki utajiri mwingi, wa mafuta, gesi, kemikali, madini na kilimo, na kwa jiografia yake, idadi ya watu na utajiri wake inaweza kuwa miongoni mwa nchi kubwa duniani, na watu wake wanaweza kuwa miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani, kwa hivyo ikiwa rais, ambaye ana mamlaka ya kuamuru na kukataza, anasema maneno haya, watu wa kawaida watasema nini?!
Hakika mfumo wa utawala nchini Iran - kama ilivyo kwa mifumo mingine katika nchi za Waislamu - ndio unaoangusha umma kwa njaa, ndio unaowezesha nchi kubwa kumiliki uwezo na utajiri wake, ndio ulioondoa mfumo wa Uislamu kutoka kwenye utawala, na umeridhia kutawala kwa mifumo ya kikafiri, na ndio ulioidhinisha mfumo wa riba nchini Iran.
Tatizo kubwa nchini Iran na nchi zote za Waislamu sio kushindwa kwa utawala, lakini ni katika mfumo wa utawala unaotekelezwa, kwa hivyo watawala wajinga wanawalazimisha Waislamu mfumo wa kibepari na ubaya wake wote, na mbaya zaidi kati yao ni mfumo wa riba, ambao ni tangazo la vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ambao unaangamiza mali, na kusababisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mhusika mkuu wa kushindwa huko kwa utawala ambako rais wa Iran anazungumzia ni rais mwenyewe, kwa nini watu wa Iran wana njaa - Enyi Masoud Pezeshkian - na mna mafuta, gesi na utajiri mwingine na madini? Je, si ni matokeo ya sera zenu za kijinga? Je, si kwa sababu ya ukengeufu wenu kutoka kwenye utawala kwa Uislamu?
Na mfano wa hayo unasemwa katika haki ya nchi zingine za Waislamu, ambamo watawala wapumbavu wanapoteza utajiri mkubwa wa umma, na kuwawezesha makafiri wakoloni kumiliki, na wananyima umma utajiri huo, kisha mmoja wao anakuja kuhalalisha sababu ya njaa kwamba ni kushindwa kwa utawala!
Enyi Waislamu: Umeonekana kwa kila mwenye macho na busara upumbavu wa watawala hawa ambao wanasimamia mambo yenu, na hawafai kuwasimamia, umefika wakati wa kuwazuia, kwa hivyo huu ndio hukumu ya mpumbavu; kumzuia kutumia pesa na kumfunga, na mumpatie bay'ah khalifa mmoja awahukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na aondoe mfumo wa riba katika nchi zenu ili Mola wenu Mtukufu na Mtume wake ﷺ awaridhie, na arejeshe utajiri wenu ulioibiwa, na arejeshe heshima na utukufu wenu, na hii hapa Hizb ut Tahrir kiongozi ambaye watu wake hawasemi uongo inawaalika kufanya kazi naye ili kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume.
Ofisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir