Organization Logo

أستراليا الممثل

أستراليا

29 Haldon St, Lakemba 2195 NSW AUSTRALIA *** PO Box 384 Punchbowl 2196 NSW AUSTRALIA

Tel: +61 438 000 465

media@hizb-australia.org

Australia Yajitolea kwa Ukaliaji wa Mabavu wa Sehemu Iliyosalia ya Palestina
Press Release

Australia Yajitolea kwa Ukaliaji wa Mabavu wa Sehemu Iliyosalia ya Palestina

October 24, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Australia Yajitolea kwa Ukaliaji wa Mabavu wa Sehemu Iliyosalia ya Palestina

Serikali ya Australia imetangaza kuwa itashiriki katika "Kikosi cha Ujenzi Mkuu wa Gaza" kinachoongozwa na Trump, muungano unaoongozwa na Marekani wa nchi za Magharibi na nchi za Kiislamu uliopewa jukumu la kuwapokonya silaha Gaza kwa nguvu na kisha kuikabidhi kwa taasisi haramu.

Tangazo hili linakuja sambamba na tangazo la taasisi haramu kutaka kuunganisha Ukingo wa Magharibi pia, sambamba na juhudi pana za Marekani za kulazimisha udhibiti wa Kiyahudi juu ya Palestina nzima katika jaribio lake la kuunda upya Mashariki ya Kati nzima.

Afisi ya Hizb ut Tahrir/ Australia inataka kusisitiza yafuatayo:


1. Australia ina rekodi ndefu ya kuhudumia maslahi ya kikoloni katika Mashariki ya Kati. Ilikuwa Kitengo cha Wapanda Farasi Wepesi wa Australia ambacho kiliingia Palestina kwa mara ya kwanza wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia kwa niaba ya Waingereza, na kuchangia katika ukaliaji wa majeshi ya Uingereza na kuikabidhi kwa Wayahudi baadaye.


2. Mchango wa Australia katika "Kikosi cha Ujenzi Mkuu wa Gaza" unalenga kulazimisha kujisalimisha kisiasa kwa Gaza baada ya Wayahudi kushindwa kufanya hivyo kijeshi. Pia, Australia ilifanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wake wa asili, na kuwezesha mauaji ya kimbari ya kwanza dhidi ya watu wa Palestina, na ilinyamaza kimya kuhusu mauaji ya kimbari katika miaka miwili iliyopita, na sasa inawasaidia Wayahudi kufuta utambulisho wa Palestina kabisa, kwa hivyo Australia italaaniwa milele kwa kuwezesha utendaji wa uhalifu huu.


3. Uhalifu mkuu katika mkasa huu ni usaliti wa watawala wa Waislamu, daima wamesimama kama mstari wa kwanza wa ulinzi kwa ukaliaji, na wamethibitisha tena usaliti wao kwa kukubali kupeleka majeshi yao kuikabidhi Palestina badala ya kuikomboa. Na Mwislamu yeyote anayeendelea kuhalalisha watawala hawa au kutetea uhalifu wao au kusaidia katika utekelezaji wa usaliti wao, atasalia kuwa mshirika katika uhalifu wao milele.


4. Muungano wa kimataifa wa Kizayuni-Kisalibani ulioundwa kulazimisha Gaza kujisalimisha unatukumbusha waziwazi chuki za kihistoria zilizokita mizizi ambazo nchi hizi zinazoifadhi kwa nchi za Kiislamu. Wanajiona kama uendelezaji wa warithi wa Wasalibani wa kwanza, na hawataacha hadi Umma wa Kiislamu wote utakaposhindwa na Sharia itakaposhindwa kabisa.


5. Imesemwa mara kwa mara katika karne iliyopita, lakini imekuwa chungu zaidi sasa, kwamba isipokuwa Waislamu watarejesha utashi wao wa kisiasa na mamlaka yao waliyoporwa, na kuwafukuza watawala wao wasaliti, na kusimamisha Khilafah Rashidah, tutabaki daima chini ya uhalifu wa Wazayuni-Wasalibani na usaliti wa vibaraka wao wa ndani. Ni wakati wa kunyakua sababu za udhibiti kutoka kwa mikono ya wadhalimu kila mahali.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Australia

Official Statement

أستراليا الممثل

أستراليا

أستراليا الممثل

Media Contact

أستراليا الممثل

Phone: +61 438 000 465

Email: media@hizb-australia.org

أستراليا الممثل

29 Haldon St, Lakemba 2195 NSW AUSTRALIA *** PO Box 384 Punchbowl 2196 NSW AUSTRALIA

Tel: +61 438 000 465 | media@hizb-australia.org

Reference: PR-019a0e35-a0f8-7685-a690-979baa114055