Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waacheni Watu Wafanye Uamuzi Wao, Enyi Watawala Wazembe!
Hatukushangazwa, kama ambavyo Umma wa Kiislamu haukushangazwa, na kukaribisha kwa wasaliti watawala wa Waislamu mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kupoteza Gaza, kwani wametuzoesha ulegevu, bali kula njama na makafiri wakoloni kuhusu masuala yetu, na Trump alikuwa amekutana na idadi yao huko New York pembezoni mwa mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jumanne 2025/9/23, hivyo walimsifu, na wakasema wanategemea kwake kumaliza vita dhidi ya Gaza, na mara tu Trump alipotangaza mpango wake wa kikoloni, walikimbilia kuukaribisha, vipi sivyo na mmoja wao hathubutu kufanya kinyume na hivyo; kwa sababu wamepoteza uanaume na ushujaa wao.
Enyi Waislamu: Mmekwisha jua bila ya kuacha shaka kwamba Trump ndiye mfuasi mkuu wa chombo haramu cha Kiyahudi katika uhalifu wake mbaya huko Gaza na Ukingo wa Magharibi, anamwandalia kila anachohitaji cha silaha, pesa na habari, na anamwandalia ulinzi wa kimtandao na kisiasa katika majukwaa ya kimataifa, na mmesikia matamshi yake mengi katika kufunika uhalifu wake, na tamko lake kuhusu eneo lake, na matamshi yake kuhusu Gaza na nia yake ya kuanzisha miradi ya kiuchumi humo, na mwenendo wake katika makubaliano ya Abraham ambayo amewalazimisha watawala wenu, na mmesikia kauli yake alipotangaza mpango wake wa kikoloni pamoja na mhalifu Netanyahu: "Ikiwa Hamas haitakubali mpango huo, atamwandalia Netanyahu uungwaji mkono kamili"; kana kwamba hajawahi kufanya hivyo hapo awali na bado anaendelea! Mmeyajua hayo yote, je, mhalifu kama huyu anaaminika kuhusu masuala yenu?! Na je, mnatumai kutoka kwake kwamba atazingatia maslahi yenu?!
Enyi Waislamu, na enyi majeshi katika nchi za Waislamu:
Hakika mnahitajia mtawala ambaye anaiga Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ katika misimamo na sera zake, na afanye kama walivyofanya Masahaba watukufu radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na wale waliowafuata kwa ihsani, mtawala anayesimama misimamo ya Abu Bakr na Omar na Harun al-Rashid na al-Mu'tasim na Salah al-Din na Baibars na Qutuz na Abdul Hamid, mnahitajia mtawala ambaye akisema neno linavuma katika pande zote za ardhi, na maadui wanatetemeka kwa hofu, neno linalofuatiwa na kitendo kinachowasahaulisha maadui wasiwasi wa shetani, ili Trump na mfano wake wa wahalifu wasifanye yale wanayowafanyia leo, bali wanafanya mahesabu elfu moja kwa Khalifa wenu, mnahitajia Khilafah ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ ameibashiria; Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume ambayo Hizb ut-Tahrir inafanya kazi ya kuisimamisha, kiongozi ambaye watu wake hawadanganyi, basi njooni kufanya kazi pamoja naye na kumsaidia, ili mpate utukufu wa dunia na ushindi Akhera, na la sivyo watawala wenu wazembe watawaangamiza, na watawapeleka kwa maadui zenu.
﴿Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, Yeye atakunusuruni na atafanya imara nyayo zenu.﴾
Ofisi Kuu ya Habari
kwa Hizb ut-Tahrir