Uzbekistan: Risala ya rambirambi kwa mbeba da'wa
Mirza Ahmadov Miraziz
Kwa masikitiko makubwa tunamtangazia umma wetu wa Kiislamu mwana mwingine miongoni mwa wana wao wacha Mungu waliosimama imara, na hatumsafishi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ndugu yetu Mirza Ahmad Miraziz amefariki siku ya Ijumaa, Oktoba 10, 2025, na swala ya jeneza iliswaliwa jana, Jumamosi. Miraziz alizaliwa Tashkent mwaka 1970. Alikuwa mmoja wa maelfu ya Waislamu waaminifu na jasiri walioitikia wito wa Hizb ut-Tahrir kwa watu wa Uzbekistan kufanya kazi ya kurejesha maisha ya Kiislamu.
Miraziz, kama vijana wengine wengi, alikamatwa na kuhukumiwa kifungo kirefu akiwa katika ujana wake katika utawala wa kidhalimu katili Karimov. Baada ya takriban miaka 20 gerezani, mwaka 2025, akiwa na umri wa miaka 55, aliachiliwa akiwa karibu mfu kutokana na mateso makali ya kimwili na kisaikolojia gerezani.
Huyu kijana muumini, ambaye alitumia takriban nusu ya maisha yake katika magereza yenye unyevunyevu, alibaki mwaminifu kwa ahadi yake aliyojiwekea mbele ya Mwenyezi Mungu, hakupiga magoti mbele ya utawala katili wa Karimov, hakumtambua, na hakukubali chochote isipokuwa dola ya Khilafah ambayo inatekeleza hukumu za Mungu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu ndugu yetu Miraziz na amsamehe, na amjaalie kuwa miongoni mwa waumini ambao alisema kuwahusu: ﴿Miongoni mwa Waumini wapo watu walioshikamana na ahadi waliyoagana na Mwenyezi Mungu. Basi wapo miongoni mwao waliokwisha timiza nadhiri yao, na wapo wanao ngojea, wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo.﴾.
Pia tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia na jamaa za ndugu yetu na tunamuomba Mungu awajalie subira njema na uthabiti. Na hatuwezi ila kusema katika nafasi hii: ﴿Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea﴾.
Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Katika Uzbekistan