Organization Logo

المكتب الإعلامي المركزي

المركزي

Tel: 0096171724043

Fax: 009611307594

media@hizb-ut-tahrir.info

www.hizb-ut-tahrir.info

Enyi Waislamu: Shikeni Hatamu za Uongozi, Wala Msifanye Masuala Yenu Yawe Mikononi mwa Maadui Zenu
Press Release

Enyi Waislamu: Shikeni Hatamu za Uongozi, Wala Msifanye Masuala Yenu Yawe Mikononi mwa Maadui Zenu

October 11, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Waislamu: Shikeni Hatamu za Uongozi, Wala Msifanye Masuala Yenu Yawe Mikononi mwa Maadui Zenu

Mazungumzo ya awamu ya kwanza katika mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kusitisha vita dhidi ya Gaza yameanza Sharm el-Sheikh nchini Misri, yakihudhuriwa na wajumbe wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner, Waziri Mkuu wa Qatar, na wakuu wa ujasusi wa Uturuki na Misri.

Ilikuwa wazi kutokana na mpango huo ni kutimiza maslahi ya kibinafsi kwa Rais wa Marekani, kuwasilisha mafanikio yake katika kusitisha vita dhidi ya Gaza kama sehemu ya wasifu wake wa kupata Tuzo ya Nobel ya Amani, na kutimiza maslahi ya kisiasa na kiuchumi kwa Marekani; kwani inafanya usimamizi wa sekta hiyo kuwa chini ya kamati ya kimataifa inayoongozwa naye, na nyuma yake Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, akijua kuwa Amerika na Uingereza ndio maadui wakubwa wa Uislamu na Waislamu, na walinzi wa chombo cha Kiyahudi! Ilikuwa pia wazi kutokana na mpango wa Trump kuzingatia maslahi ya chombo cha Kiyahudi, kukiwezesha katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na kuzuia hatari yoyote inayoitishia.

Kabla ya kuwasilisha mpango wake, Trump aliongoza mkutano uliowajumuisha Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia na Pakistan, pembezoni mwa mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jumanne, 2025/9/23, akielezea kama "mkutano muhimu zaidi". Kisha akawasilisha, au kuwalazimisha, "mpango wa pointi 21" ambao muhimu zaidi ulikuwa: (Kuachiliwa kwa mateka wote wa Kiyahudi na Hamas, usitishaji wa mapigano wa kudumu, na uondoaji wa taratibu wa jeshi la Kiyahudi), na Trump alikuwa mkweli katika kusudi lake la kuwakusanya ili kukomboa mateka wa Kiyahudi, alihutubia akisema: (Utawala wake unataka kurejesha mateka 20 na maiti 38 kutoka Gaza ...), kisha akasisitiza hatua kwa hatua katika uondoaji, ambalo ni neno lililojaa mtego wa kukomesha uondoaji, na kisha chombo cha Kiyahudi kinabaki kudhibiti uendelevu wa usitishaji wa mapigano! Haishangazi kusikia kukaribishwa kwa watawala wa Kiislamu wa Rowaibidah kwa mpango wa Trump, na haishangazi kuona kila mmoja wao akisubiri zamu yake ya uhaini katika mpango huu, na baadhi yao wameanza jukumu lao katika mazungumzo ya awamu ya kwanza, kwa hivyo tuliona Waziri Mkuu wa Qatar akishiriki ndani yake, na pia wakuu wa ujasusi wa Uturuki na Misri, na wengine wanasubiri zamu yao, ni ubaya ulioje wanaoutenda!

Enyi Waislamu: Hakika watawala wenu walio dhaifu wamewauza kwa bei duni zaidi, na wameacha masuala yenu kwa maadui zenu, ili kuhifadhi viti vyao vilivyopotoka, vinavyoelekea kuanguka, na ukimya wenu juu yao unawafanya waendelee na upotovu na uhaini wao, hawaoni haya kwa Mwenyezi Mungu wala Mtume wake wala kwenu, wamefanya njama dhidi ya Palestina na wakaiwezesha Wayahudi kuitawala, na wamenyamazia mauaji ya makumi ya maelfu na uharibifu wa nyumba juu ya vichwa vya wakazi wake huko Gaza, na walishuhudia kuhamishwa kwa watu wake kutoka nyumba zao, na wakati huo walikuwa wanatoa wito wa amani, na suluhisho la mataifa mawili - mradi wa Amerika - ambao unatimiza maslahi ya chombo cha Kiyahudi.

Umefika wakati wa kuweka kikomo kwa uhaini wa watawala hawa wa Rowaibidah, na kuwatupa kama kokwa, na kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir, kiongozi ambaye watu wake hawasemi uongo, ili kusimamisha Khilafah Rashidah ya Pili kwa njia ya Utume, ili utukufu wako na heshima yako zirejee kwako, na mshike hatamu ya uongozi, na muwe nyinyi ndio watendaji wenye ushawishi katika kuunga mkono masuala yenu, na msiruhusu maadui zenu kuchukua madaraka ya mambo yenu.

﴿Ikiwa Mwenyezi Mungu atawasaidia, basi hakuna atakayewashinda, na ikiwa atawaacha, basi ni nani atakayewasaidia baada yake? Na kwa Mwenyezi Mungu ndio wanapaswa kumtegemea waumini

Ofisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut-Tahrir

Official Statement

المكتب الإعلامي المركزي

المركزي

المكتب الإعلامي المركزي

Media Contact

المكتب الإعلامي المركزي

Phone: 0096171724043

Fax: 009611307594

Email: media@hizb-ut-tahrir.info

المكتب الإعلامي المركزي

Tel: 0096171724043 | media@hizb-ut-tahrir.info

Fax: 009611307594

www.hizb-ut-tahrir.info

Reference: PR-0199c428-b450-7eec-91f3-f3e604fa0bf9