Organization Logo

المكتب الإعلامي المركزي

المركزي

Tel: 0096171724043

Fax: 009611307594

media@hizb-ut-tahrir.info

www.hizb-ut-tahrir.info

Enyi Waislamu: Je, bado mna matumaini kwa watawala wenu wajinga?!
Press Release

Enyi Waislamu: Je, bado mna matumaini kwa watawala wenu wajinga?!

August 07, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Waislamu: Je, bado mna matumaini kwa watawala wenu wajinga?!

Bado shirika la Kiyahudi linaendelea na uhalifu wake dhidi ya watu wa Gaza, na kusababisha makumi ya mashahidi kuongezeka kila siku, na pia linaendelea kuweka mzingiro Gaza, na watu wake wanakufa kwa njaa, na wamekuwa bila chakula, kinywaji, dawa, au makazi, licha ya majaribio fulani ya kupeleka msaada kwao kwa aibu! Lakini mamia ya maelfu hawapati hata tonge la kujikimu au kutuliza njaa za watoto wao, hivyo wanakuwa wanakufa kwa njaa mikononi mwao na mbele ya macho ya dunia nzima bila msaidizi au mlinzi.

Tumeshuhudia watu wengi duniani wakichukua hatua wakidai kumalizwa kwa vita dhidi ya Gaza na kuondolewa kwa mzingiro kwa watu wake, na kuwapatia chakula na kinywaji, na hilo halikutoa chochote isipokuwa aibu zaidi kwa serikali zao, na baadhi yao walidai kwa aibu kuondolewa kwa mzingiro kwa watu wa Gaza, kama vile mtu yeyote wa kawaida asiye na uwezo, kana kwamba wao si wamiliki wa uamuzi wa kisiasa!

Ama nchi za Waislamu, usiulize hali yake, hasa nchi zilizo karibu na Palestina, kwani watawala wake wasaliti wajinga wanazuia kitu chochote kuingia Gaza, licha ya shauku ya watu wa nchi hizo kupigania njia ya Mungu na kuwasaidia ndugu zao huko Gaza.

Ama majeshi ya nchi hizo, badala ya kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kupigana na shirika la Kiyahudi, na kuondoa mateso kwa watu wa Gaza, baadhi yao wanasimama kwenye mipaka, kuwazuia Waislamu kuvuka, na kuwasaidia watu wa Gaza! Kana kwamba wanangojea amri kutoka kwa wale wajinga ambao wamechukua jukumu la kulinda shirika la Kiyahudi!

Swali ambalo linajitokeza kila wakati, na mbele ya mateso ya watu wa Gaza: Je, bado Waislamu au majeshi yao wana chembe ya matumaini kwa watawala hawa wajinga?! Je, wanangojea harakati za Al-Mu'tasim zitokee ndani yao?! Jibu liko katika kauli Yake Mwenyezi Mungu: ﴿Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyomo ndani ya watu mpaka wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao﴾, na msingi wa kubadilisha yaliyomo ndani ya nafsi ni mifumo inayotumika kwao, nayo ni mifumo ya wasaliti, inayowazuia na dini ya Mungu, na kukata uhusiano wa undugu wa Kiislamu kati yao, na kuamsha ndani yao hisia za utaifa ambazo Mungu ameziharamisha, na kufanya kile kinachotokea Gaza cha mauaji, uharibifu, mzingiro, na njaa kana kwamba hakitokei katika nchi za Waislamu; na kana kwamba hakitokei kwa ndugu zao Waislamu!

Enyi Waislamu, na enyi majeshi katika nchi za Waislamu:

Umekwishafika wakati wa kufunga nia yenu na kufanya uamuzi wenu wenyewe mbali na watawala wale wajinga, ambao wamewekwa na kafiri mkoloni juu ya shingo zenu, hawazingatii kwenu uaminifu wala ahadi, na hawajali kutunza mambo yenu, wala kuhifadhi maslahi yenu, wala kuwasaidia ninyi na kuwasaidia ndugu zenu huko Gaza na kwingineko, na imewalazimu kuwavua, na kumtii khalifa anayewahukumu kwa Kitabu cha Mungu na Sunna za Mtume wake, na anayeahamisha majeshi kuwasaidia Waislamu, na kuwarudishia heshima na utukufu wenu, na hamna mbele yenu isipokuwa Hizb ut-Tahrir, kiongozi ambaye watu wake hawadanganyi, mwenye mradi wa kuamsha kwenu kwa misingi ya Uislamu, basi msaidieni Mungu ili akusaidieni na athibitishe nyayo zenu.

Ofisi ya Habari Kuu

kwa Hizb ut-Tahrir

Official Statement

المكتب الإعلامي المركزي

المركزي

المكتب الإعلامي المركزي

Media Contact

المكتب الإعلامي المركزي

Phone: 0096171724043

Fax: 009611307594

Email: media@hizb-ut-tahrir.info

المكتب الإعلامي المركزي

Tel: 0096171724043 | media@hizb-ut-tahrir.info

Fax: 009611307594

www.hizb-ut-tahrir.info

Reference: PR-0198811d-3218-7ac4-8d08-5a72190f9832