Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Dharau ya Marekani kwa Raia Wake Inawaacha Wanawake na Watoto na Njaa
(Imetafsiriwa)
Mpango wa Msaada wa Lishe wa Ziada (SNAP) ni programu ya shirikisho inayosaidia watu binafsi na familia zenye kipato cha chini na watu wenye ulemavu kupata marupurupu ya kielektroniki yanayotumika kununua chakula na vinywaji, isipokuwa vileo, na mimea ya kujipandia chakula chao wenyewe. Ripoti zinaonyesha kuwa Wamarekani milioni 42 wanategemea marupurupu ya (SNAP) kujilisha wao na familia zao. 54% ya watu wazima wanaopokea marupurupu ya chakula ni wanawake, wengi wao wakiwa mama wasio na waume, na 39% yao ni watoto, ambayo inamaanisha kuwa karibu mtoto mmoja kati ya watano anategemea marupurupu haya ili kuhakikisha kuwa hana njaa. Vile vile, kufungwa kwa serikali kuu kulilazimu baadhi ya majimbo kutafuta njia zingine za kufadhili programu za chakula cha mchana cha bure na cha bei iliyopunguzwa katika maeneo yao ya elimu, ili watoto wanaotegemea chakula wakati wa siku ya shule wasilazimike kuishi bila chakula. Kwa sababu hiyo, maghala mengi ya chakula yaliyoenea kote nchini yanachapisha picha za rafu tupu, na yanaomba watu watoe chakula na kadi za zawadi za maduka ya mboga ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya chakula.
Tunaweza kuuliza, ni vipi taifa tajiri zaidi ulimwenguni linaweza kupuuza ukweli kwamba mamilioni ya raia wake walio hatarini zaidi hawatapata chakula cha kutosha? Unaweza kujiuliza Marekani inatumia wapi pesa zake, hata wakati wa kufungwa kwa serikali? Vema, badala ya kuhakikisha kuwa Wamarekani wanapata chakula cha kutosha, wanatuma mabilioni ya dola kwa shirika la Kiyahudi kuwaua Wapalestina. Ni mtawala anayeona ujenzi wa ukumbi wa kifahari ni muhimu kuliko kitu kingine chochote, huku manaibu wengine wakiona uwekezaji wao wa kibinafsi unapewa kipaumbele kuliko ustawi wa watu wanaopaswa kuwawakilisha! Kama unavyoona, Marekani ya kibepari haijawahi kuwa na nia ya kutunza maslahi ya raia wake, lakini ilikuwa na nia tu ya kutoa msaada wa kijeshi na kifedha kwa wale wanaowanyima watoto ulimwenguni kote haki yao ya usalama, chakula, makazi na elimu, ambayo ni mahitaji ya msingi. Kwa hivyo, inawaacha watoto huko Amerika pia wakiteseka na njaa na ukosefu wa usalama, na kukosa elimu na huduma sahihi za afya.
Hata wale wanaoishi katika mataifa tajiri zaidi ulimwenguni, wanahitaji sana mfumo wa kisiasa ambao hauwaachi raia wake na njaa, huku watawala wakitazama akaunti zao za benki za kibinafsi zikiongezeka. Mfumo wa kisiasa ambao kiongozi wake hutembelea nchi, kama Khalifa Omar bin al-Khattab, Mwenyezi Mungu amridhie, ili kuhakikisha kwamba kila mtoto ana uwezo wa kula hata kabla ya kujilisha mwenyewe. Mfumo wa kisiasa unaotegemea yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyateremsha ili kuendesha mambo ya watu. Na hakuna mfumo mwingine wa kisiasa unaoweza kufanikisha mambo haya na zaidi; ni Khilafah.
Sehemu ya Wanawake
Katika Ofisi ya Habari Kuu
ya Hizb ut-Tahrir