Organization Logo

الدنمارك مكتب

الدنمارك

Tel:

info@hizb-ut-tahrir.dk

http://www.hizb-ut-tahrir.dk/

Kuunga mkono mauaji ya kimbari ni uhalifu, si wito wa ukombozi!
Press Release

Kuunga mkono mauaji ya kimbari ni uhalifu, si wito wa ukombozi!

October 19, 2025
Location

Taarifa kwa vyombo vya habari

Kuunga mkono mauaji ya kimbari ni uhalifu, si wito wa ukombozi!

(Imetafsiriwa)

Leo Ijumaa, Oktoba 17, 2025, Mahakama ya Kitaifa imeniachilia huru baada ya kutiwa hatiani katika mahakama ya jiji kwa kosa la kutoa wito wa ukombozi wa Palestina.

Hotuba yangu katika maandamano ya Mei 2021 mbele ya ubalozi wa Misri, ambapo niliita majeshi ya Waislamu kuokoa wanaume, wanawake na watoto wanaoonewa huko Gaza, ilikuwa ni uhalifu kulingana na hukumu ya mahakama ya jiji la Copenhagen iliyotolewa Juni 2024!

Ilibainika katika mahakama ya jiji na mahakama kuu kwamba hotuba hiyo haikulenga Wayahudi, lakini ilitoa wito wa kuondoa chombo cha Kizayuni kinachokalia ardhi kwa nguvu kupitia mapambano ya silaha.

Hukumu ya mahakama ya jiji ilitoa hukumu ya moja kwa moja kwa kutoa wito wa ukombozi wa Palestina, ambapo madai ya kizamani ya ofisi ya mwendesha mashtaka kuhusu kupinga Usemiti yalianguka haraka.

Hukumu hii ilibatilishwa leo kwa kuwa haieleweki na haina msingi wa kisheria. Hata hivyo, ilikuwa sehemu ya mkondo wa kisiasa wa hukumu za haraka dhidi ya wapinzani wa uvamizi wa Kiyahudi wa Palestina.

Ni aibu kwa mfumo wa mahakama wa Denmark kwamba kesi hii ilifika katika mahakama kuu kabla ya kukataliwa, na kwamba mahakama imepotoshwa kwa kiwango hiki kikubwa ili kulinda chombo kinachofanya mauaji ya kimbari na kutoa msaada usio na masharti kutoka kwa serikali ya Denmark.

Jaji wa mahakama kuu alikataa kukubali shinikizo kubwa lililowekwa na serikali, ambalo lilishawishi polisi na ofisi ya mwendesha mashtaka kufungulia mashtaka mtu yeyote anayetoa wito wa ukombozi wa Palestina.

Licha ya kuachiliwa kwangu huru sasa, msururu mrefu wa hukumu za kisiasa zilizotolewa dhidi ya watu waliotoa wito au kuunga mkono upinzani wa silaha dhidi ya chombo cha Kiyahudi hauwezi kupuuzwa. Katika kesi moja, mambo yalifika hadi kufikia kunyang'anywa uraia!

Kuwaadhibu watu na kuwafungulia mashtaka kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa dhidi ya uvamizi wa kijeshi ambao unafanya mauaji ya kimbari kwa kutumia vipengele vya silaha vya Denmark ni majaribio ya uonevu yasiyokubalika. Lakini njia hii imefika mwisho. Iwe kuna kesi za kisiasa au la, wito wa ukombozi wa kweli wa Palestina hauwezi kusimamishwa. Leo imekuwa wazi zaidi kuliko hapo awali kwamba saratani ya Kizayuni inayowakilishwa na uvamizi wa kijeshi, ugaidi wa kimfumo, mauaji ya halaiki, mateso, wizi wa ardhi na utakaso wa kikabila, lazima iondolewe kwa hatua za kijeshi, ambayo ni maono ambayo yanapata nguvu duniani kote kama suluhisho la kweli pekee.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir/Denmark tunatoa wito kwa kila mtu aliye na chembe ya haya kuendeleza upinzani dhidi ya uungaji mkono wa Denmark kwa koloni la walowezi, chombo cha Kiyahudi, na mipango yake inayoendelea ya kuangamiza watu wa Palestina.

Tunatoa wito kwa ndugu na dada zetu Waislamu kufanya kazi kwa dhamira na uvumilivu zaidi ili kukomesha kabisa uvamizi na kukomboa Palestina kupitia majeshi ya nchi za Kiislamu.

Kutoa wito wa ukombozi wa Palestina sio uhalifu, lakini ni wajibu na heshima. Ni serikali ya Denmark ambayo inatenda uhalifu kwa kuunga mkono koloni la walowezi ambalo linafanya mauaji ya kimbari.

Elias Lamrabet

Mwakilishi wa vyombo vya habari wa Hizb ut-Tahrir nchini Denmark

Official Statement

الدنمارك مكتب

الدنمارك

الدنمارك مكتب

Media Contact

الدنمارك مكتب

Phone:

Email: info@hizb-ut-tahrir.dk

الدنمارك مكتب

Tel: | info@hizb-ut-tahrir.dk

http://www.hizb-ut-tahrir.dk/

Reference: PR-0199f223-ede8-7b40-9127-26581a553bec