Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaliko wa Adui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waislamu Unastahili Ghadhabu na Hasira za Mwenyezi Mungu
Mche Mwenyezi Mungu Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia!
(Imetafsiriwa)
Hizb ut-Tahrir / Malaysia inalaani vikali mwaliko uliotumwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato' Seri Anwar Ibrahim, kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye mikono yake bado imelowa damu ya Waislamu huko Gaza, kwenda Malaysia kuhudhuria Mkutano wa Arobaini na Saba wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia (ASEAN) huko Kuala Lumpur. Mwaliko huu sio tu ishara ya aibu ya kidiplomasia ambayo haina msingi wowote wa kimaadili; bali ni dharau kubwa kwa heshima ya taifa hili, na usaliti unaoumiza hisia za kila Muislamu ambaye bado anabeba heshima karibu na moyo wake, hasa watu wa Palestina.
Inawezekanaje kwa mtu anayedai kuwatetea watu wa Palestina kumwalika muuaji wao na mharibifu wa ardhi yao, katika nchi za Waislamu?! Heshima yetu iko wapi wakati adui wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na adui wa Mtume Wake ﷺ na adui yetu anapokelewa katika nchi yetu kwa heshima na sherehe?! Ni chembe gani ya thamani anayo adui wa Uislamu kama huyu ya kumwandalia zulia jekundu?! Ni nani kati ya maadui wa Mwenyezi Mungu leo, anayeweza kuwa wa kudharauliwa zaidi na Mwenyezi Mungu? Nani anahusika na mauaji ya Waislamu zaidi ya 67,000 na uharibifu wa Gaza?! Trump huyu sio tu kafiri jeuri; damu ya Waislamu wasio na hatia imemwagika kwenye udongo wa Gaza kwa amri yake, na anajivunia sana hilo. Ametambua Quds, kibla cha kwanza cha Waislamu, kama mji mkuu wa chombo cha Kiyahudi ghasibu. Na kwa kusaini kwake, alitunga kile kinachoitwa "Mpango wa Karne," ambao ni mpango ambao umekataa haki za watu wa Palestina na kwa kweli unalenga kufuta Palestina kutoka kwenye ramani ya dunia. Na sasa tena anatangaza kile kinachoitwa "mpango wa amani" kwenye ardhi ambayo hana haki yoyote ya kisheria ndani yake kabisa. Je, mtu kama huyu anastahili kualikwa na kuheshimiwa katika nchi ambayo watu wake wanashuhudia kwamba hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu?!
Waziri Mkuu wa Malaysia anataka kuficha aibu hii kwa vazi la urais wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia (ASEAN). Tunauliza kwa uaminifu: Je, ni wajibu kwa urais wa Jumuiya ya ASEAN kutoa mwaliko kama huu? Kinyume chake, kukataa mwaliko wa Trump mhalifu kungeonyesha athari ya heshima na ujasiri. Vyovyote vile visingizio, havifichi ukweli kwamba kitendo hiki kinatokana na kujisalimisha kwa Amerika na kuiogopa. Wakati unyenyekevu na heshima ya kweli ni kwa Mwenyezi Mungu pekee, sio kwa maadui Zake.
Jambo la aibu zaidi ni kudai kwamba kwa kuwepo Trump, ujumbe kuhusu Palestina unaweza kuwasilishwa kwake moja kwa moja! Ni dhana ya kejeli sana: Je, mbwa mwitu anayekula kundi atasikiliza ushauri wa kuwahurumia kondoo?! Jambo la upuuzi kama nini! Tunawezaje kuomba suluhisho kutoka kwa yule aliyeharibu Gaza?! Tunawezaje kuinua sauti zetu, au hata kukubali suluhisho la tatizo letu, kutoka kwa adui yetu mwenyewe? Fahamu ewe Waziri Mkuu wa Malaysia kwamba suluhisho la suala la Palestina halitatoka kwa Donald Trump. Suluhisho liko mikononi mwako, wewe na watawala wote wa Waislamu; kwa kukusanya majeshi yenu ili kung'oa chombo cha Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake. Lakini kwa bahati mbaya hufanyi hivyo, badala yake unawasalimisha shingo za Wapalestina kwa Trump na Wayahudi ili wawachinje!
Kwa hakika, kumwalika Trump katika nchi hii haimaanishi tu kuchochea ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, bali pia kuhatarisha mamlaka ya nchi yenyewe. Mara tu atakapowasili, hatutakuwa na udhibiti kamili juu ya vipengele vya mfumo wa usalama wa taifa: polisi, jeshi, mamlaka za uhamiaji na taasisi nzima ya usalama itasambazwa tena ili kuhakikisha ulinzi wa mtu anayehusika na mauaji ya Waislamu zaidi ya 67,000, ili kuzuia chembe yoyote ya vumbi kumgusa. Na hii ni dharau kubwa, muuaji wa watoto wachanga, watoto, wanawake na wazee anachukuliwa kwa njia ambayo inazidi hata kumchukulia mfalme! Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿Enyi mlio amini! Msiwafanye maadui zangu na maadui zenu kuwa marafiki.﴾
Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia: Fahamu kwamba kwa kumwalika Trump katika nchi yako, na kumketisha katika baraza lako na kupiga picha naye, hautapata kwa hilo chembe ya heshima, kwani heshima yote ni ya Mwenyezi Mungu. Wajue wale wanaotafuta kuboresha sifa zao mbele ya maadui wa Mwenyezi Mungu kwamba wanachukuliwa kuwa wanyonge machoni pa waumini wa kweli, na kwamba aibu yao mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kubwa zaidi. ﴿Je, wanatafuta heshima kwao? Hakika heshima yote ni ya Mwenyezi Mungu.﴾
Zaidi ya hayo, hakuna tofauti ya kivitendo kati ya kumwalika Trump na kumwalika Netanyahu katika nchi hii, kwani wote wawili ni kafiri mharamia, adui wa Uislamu, wa Mwenyezi Mungu, wa Mtume Wake na wa Waislamu. Na wote wawili ni wahalifu wachafu, lakini Trump anahisi kuwa yuko juu kwa sababu watawala wa Waislamu wamechagua kumtukuza; jinsi walivyo duni!
Hizb ut-Tahrir inafanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashidah ya Pili kwa njia ya Utume, ambayo itaifunza Amerika na chombo cha Kiyahudi maana halisi ya urafiki na uadui. Wakati huo, maadui wa Mwenyezi Mungu wataishi dharau duniani, kabla ya kuonja dharau ya Akhera mikononi mwa Mwenyezi Mungu.
Abdul Hakeem Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Nchini Malaysia