Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaliko wa Kuhudhuria Kipindi cha Saluni ya Kisiasa
Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan inazindua hafla ya mara kwa mara yenye kichwa: (Saluni ya Kisiasa), mwaliko ambao unaelekezwa kwa wanahabari, wanasiasa, na wote wanaopenda masuala ya umma, kuhudhuria na kushiriki.
Kipindi cha kwanza mwezi huu cha Saluni ya Kisiasa kitamshirikisha Bwana Hatem Jaafar, mwanasheria, mwanachama wa baraza la Hizb ut Tahrir katika Jimbo la Sudan, chenye kichwa: (Sera ya Trump na Athari zake kwa Uamsho wa Umma wa Kiislamu).
Saluni itaendeshwa na Bwana Muhammad Jami (Abu Ayman), msaidizi wa msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Jimbo la Sudan.
Wakati: Jumamosi 25 Dhu al-Hijjah 1446 AH, sawia na 2025/06/21 BK, saa moja baada ya adhuhuri InshaAllah.
Mahali: Ofisi ya Hizb ut Tahrir / Jimbo la Sudan huko Port Sudan - Kitongoji cha Al-Azma.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Katika Jimbo la Sudan