Organization Logo

تركيا مكتب

ولاية تركيا

Tel:

bilgi@hizb-turkiye.org :

http://www.hizb-turkiye.com

Ziara ya Marekani Moja kwa Moja: Udhuru, Kuomba, Uhalali, Makubaliano, na Majukumu Mapya!
Press Release

Ziara ya Marekani Moja kwa Moja: Udhuru, Kuomba, Uhalali, Makubaliano, na Majukumu Mapya!

September 30, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Ziara ya Marekani Moja kwa Moja: Udhuru, Kuomba, Uhalali, Makubaliano, na Majukumu Mapya!

(Imetafsiriwa)

Ziara ya Rais wa Uturuki Erdogan nchini Marekani kushiriki katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilikuwa tukio la aibu, si kwake tu, bali pia kwa viongozi wote wa nchi. Rais wa Marekani mwenye kiburi, Donald Trump, alitoa hotuba mbele ya Baraza Kuu akitangaza kwamba Marekani ndiyo "taifa kubwa na lenye nguvu zaidi duniani" kisiasa, kijeshi na kiuchumi, na kwamba katika miezi minane ya utawala wake, ameiwekea dunia ushuru wa ziada wa dola trilioni 17, na kwamba Marekani iko katika hali bora huku nchi zingine "zinaelekea kuzimu," na kwamba maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayana maana, na pia alidai kuwa amemaliza vita saba ndani ya miezi saba. Na kwamba tarehe 7 Oktoba 2023 ilikuwa "ukatili wa magaidi wa Hamas," akizingatia kuwa suluhu ni kuachiliwa mara moja kwa mateka, na akaongeza kuwa dini inayoathiriwa zaidi na mateso duniani ni Ukristo. Katika hotuba yake, Trump aliwatusi nchi zote kuanzia Amerika ya Kusini hadi nchi za Kiislamu, na kutoka Ulaya hadi Urusi, akionyesha kiburi cha Amerika kwa sauti ya juu, huku wawakilishi wa nchi wakipokea matamshi haya ndani ya ukumbi kwa makofi!

Kisha ilifika zamu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ambaye alizungumza waziwazi kuhusu Uturuki, akisema kwamba viongozi wanaokwenda kukutana na Trump wanaomba Marekani ili kutatua suala la Gaza, na kwamba wanazungumza wanavyotaka nje ya Ikulu ya White House, lakini mwishowe wanakimbilia huko, akiongeza kuwa Erdogan pia atakuja Ikulu ya White House, na kwamba viongozi wote wanaomba kupata dakika tano za kukutana na kusalimiana na Trump. Balozi wa Marekani nchini Uturuki, Tom Barak, alisema kwamba Trump amechoshwa na Erdogan, lakini atampa uhalali anaouhitaji, akisema kwamba suala si S-400 au ndege za F-16, bali "uhalali" kwanza.

Mkutano kati ya Trump na Erdogan ulifanyika katika mazingira haya ya kudhalilisha. Vyombo vya habari vilikuwa vimezungumzia kabla ya ziara juu ya mkutano wa siri kati ya mtoto wa Trump na Erdogan huko Istanbul, ambapo kulikubaliwa kununua ndege 300 za Boeing badala ya kupanga tarehe ya mkutano. Wakati viongozi wengine walikuwa wanaomba dakika tano, mkutano kati ya Trump na Erdogan uliendelea kwa saa mbili kamili. Katika mkutano huu, Trump hakusema neno lolote katika taarifa zake kuhusu taasisi ya Kiyahudi na Gaza, au kumkumbusha kuhusu suala la Padre Branson, au kuashiria uchaguzi uliofanyika kwa udanganyifu. Badala yake, mkutano huo ulijadili masuala magumu sana na ya gharama kubwa, ikiwa ni pamoja na: Syria, Ukraine, mauzo ya ndege za F-16 na F-35 na risasi za kijeshi, vikwazo vilivyowekwa kwa nchi adui chini ya Sheria ya Kukabiliana na Maadui wa Marekani, ununuzi wa Uturuki wa gesi asilia iliyoyeyushwa yenye thamani ya dola bilioni 45 kutoka upande mwingine wa dunia kwa miaka 20 licha ya eneo lake la kijiografia lililo tajiri kwa gesi, nishati ya nyuklia, na suala la benki ya Halk, na shule ya watawa huko Heybeliada. Lakini maelezo ya mikutano hii hayajafichuliwa bado, huku Trump akisema: "Mtatishwa mtakapojua tulichozungumzia na Erdogan." Ilikuwa ya kushangaza kwamba Trump alimpokea Erdogan kibinafsi mlangoni, akamvutia kiti, akamwagia sifa, akafanya naye mkutano mrefu, kisha akamuaga huku akielezea mkutano huo kuwa "mzuri sana," katika tukio linaloonyesha ukubwa wa makubaliano aliyoyatoa na jukumu alilolilazimisha.

Haipendezi kamwe muungano wa nchi ambayo watu wake ni Waislamu na Marekani, ambayo inachukuliwa kuwa adui wa wazi wa Uislamu na Waislamu, na mshirika katika matukio yote mabaya yanayoshuhudiwa katika nchi za Kiislamu, na mshiriki katika mauaji ya kimbari ya Gaza, na msaidizi kamili wa taasisi ya Kiyahudi. Pia, kumtendea Rais wa Marekani mwenye kiburi, Trump, ambaye anawatusi na kuwanyonya watu duniani, kama "rafiki," na kutoa makubaliano haya yote kwa ajili ya mkutano, ni jambo lisilokubalika kabisa. Zaidi ya hayo, ufafanuzi wa idara ya mawasiliano kwa taarifa za Erdogan kwenye kituo cha Fox News, badala ya kumjibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rubio, ni jambo la aibu sana. Udhalilishaji huu ambao ulifanyika kwa ajili ya mkutano na Trump ni rehani kwa mustakabali wetu na nchi yetu, na ni usaliti kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwa Gaza mchana kweupe.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Uturuki

Official Statement

تركيا مكتب

ولاية تركيا

تركيا مكتب

Media Contact

تركيا مكتب

Phone:

Email: bilgi@hizb-turkiye.org :

تركيا مكتب

Tel: | bilgi@hizb-turkiye.org :

http://www.hizb-turkiye.com

Reference: PR-01998fa2-2400-76f6-bef7-6abe5af994eb