Organization Logo

الباكستان مكتب

ولاية باكستان

Twitter: http://twitter.com/HTmediaPAK

Tel:

HTmediaPAK@gmail.com

http://www.hizb-pakistan.com/

Watawala wa Pakistan, Watu wa Trump, Wanawateka Nyara Vijana wa Hizb ut-Tahrir Ili Kuhakikisha Utoaji Kamili wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina
Press Release

Watawala wa Pakistan, Watu wa Trump, Wanawateka Nyara Vijana wa Hizb ut-Tahrir Ili Kuhakikisha Utoaji Kamili wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

October 27, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala wa Pakistan, Watu wa Trump, Wanawateka Nyara Vijana wa Hizb ut-Tahrir

Ili Kuhakikisha Utoaji Kamili wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Kamanda wa uwanja anayependwa na Trump, Asim Munir, alijibu kwa ukatili kampeni kali ya Hizb ut-Tahrir katika jimbo la Pakistan, ambayo inataka uhamasishaji wa haraka wa vikosi vya jeshi vya Pakistani kuikomboa Palestina. Majambazi wa Asim Munir waliwateka nyara wanaharakati watano kutoka Lahore, Karachi na Peshawar, na mahali walipo bado haijulikani. Ukatili wa Asim Munir ulitarajiwa, kwani hawezi kuchukua hatua, au hata kufikiria nje ya miongozo ya Trump katika suala lolote, iwe ni kuhusu Gaza, Kashmir, Afghanistan, au rasilimali kubwa za madini nchini Pakistan. Mwongozo wa sasa wa Trump kuhusu Gaza ni "Amani kupitia Nguvu," yaani, kukandamiza upinzani wowote kwa nguvu ili kulazimisha kutoa ardhi nyingi iliyobarikiwa ya Palestina kwa chombo cha Kiyahudi, kama sehemu ya mpango wa Trump au "Mikataba ya Abraham." Asim Munir alihamasisha dhidi ya Hizb ut-Tahrir, kama walivyofanya mawakala wengine wa ukoloni katika nchi za Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Jordan na Lebanon hivi karibuni.

Enyi Waislamu nchini Pakistan, Ardhi Takatifu: Tunawahakikishia, sisi vijana wa Hizb ut-Tahrir, kwamba hatutaacha kuilingania Uislamu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kwa robo karne nchini Pakistan, tumekabiliana na watawala dhalimu wengi, kutoka Musharraf hadi Asim Munir, na tumekabiliwa na kampeni nyingi za ukandamizaji, kukamatwa, mateso na utekaji nyara. Daima tumekuwa tukivumilia, tukishikamana na njia ya Mtume ﷺ katika mabadiliko, tukifuata uvumilivu wake ﷺ baada ya kuwaambia watu: «SEMENI: HAKUNA MWENYE KUSTAHIKI KUABUDIWA KWA HAKI ISIPOKUWA ALLAH MPATE KUFANIKIWA». Tunaiga uvumilivu wa Ammar bin Yasser, Mwenyezi Mungu amridhie, ambaye alishuhudia kuuawa kwa wazazi wake, na Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akawaambia: «SUBUHINI ENYI FAMILIA YA YAASIR, KWANI AHADI YENU NI PEPONI». Na tunasubiri tukitarajia thawabu, tukisisitiza kwamba baada ya utawala wa dhuluma, ukandamizaji na zama za kulazimishwa, kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume. Ahmad amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: «KISHA UTAKUWA UFALME WA KULAZIMISHWA, NA UTAKUWA KAMA ALLAH ATAKAVYOTAKA UWE, KISHA ATAUONDOA ATAKAPOTAKA KUONDOA, KISHA ITAKUWA KHILAFAH KWA NJIA YA UTUME», huu ni sunna ya Mwenyezi Mungu katika kuwajaribu Waislamu kabla ya kuwaneemesha kwa ushindi. Basi simameni pamoja nasi, na semeni neno la haki mbele ya watawala dhalimu!

Enyi Maafisa katika Vikosi vya Jeshi vya Pakistan: Mnafahamu vyema kwamba Hizb ut-Tahrir haibebi silaha, licha ya dhuluma zote ilizokumbana nazo kwa zaidi ya miongo saba katika nchi za Kiislamu. Kwa hivyo, chama kinafuata kwa usahihi njia ya Mtume ﷺ ambaye alizuia katika Makka kwa da'wah tu na hakufanya kitendo chochote cha kijeshi kabla ya Hijra. Na pale Masahaba wa Bait ya pili ya Aqaba walipomuuliza ruhusa ya kupigana kwa mapanga huko Mina, aliwaambia ﷺ: «HATUJAAMRISHWA HILO BADO».

Na sasa, ingawa sisi vijana wa Hizb ut-Tahrir hatuna silaha, lakini tunawataka nyinyi watu wa silaha na nguvu mtoe nusra ya kijeshi ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ombi letu hili linaendana na njia ya Mtume ﷺ, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alikutana mwenyewe na watu wa nguvu na silaha na akawaomba nusra ili kuiwezesha dini, na akauliza kuhusu uwezo wa kimwili na ulinzi, ambapo alikuwa akiuliza: «JE, KUNA ULINZI KWA WATU WAKO?», alikutana na makabila mengi kama vile Bani Kilab, Bani Hanifa, Bani Amir bin Sa'sa'a na Bani Kinda na Bani Shayban. Na Mtume ﷺ aliendelea na njia hii kwa uvumilivu hadi Mwenyezi Mungu alipomneemesha kwa ushindi, kwa hivyo Ansar walitimiza nusra, na hivyo ukawa Utawala wa Kiislamu huko Madina. Pamoja na dhuluma zote tunazokabiliana nazo, tutaendelea kudai kwamba mtoe nusra ya kijeshi ili kusimamisha hukumu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyateremsha, basi fanyeni haraka katika itikio lenu, ili tusishuhudie dhidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama!

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Katika Jimbo la Pakistan

Official Statement

الباكستان مكتب

ولاية باكستان

الباكستان مكتب

Media Contact

الباكستان مكتب

Phone:

Email: HTmediaPAK@gmail.com

الباكستان مكتب

Twitter: http://twitter.com/HTmediaPAK

Tel: | HTmediaPAK@gmail.com

http://www.hizb-pakistan.com/

Reference: PR-019a2514-f1e8-77d3-a009-a67634800fa5