Organization Logo

مصر - المكتب

ولاية مصر

Tel:

info@hizb.net

www.hizb.net

Kuzingirwa kwa Gaza ni Ushahidi wa Uasi wa Serikali ya Misri
Press Release

Kuzingirwa kwa Gaza ni Ushahidi wa Uasi wa Serikali ya Misri

July 26, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuzingirwa kwa Gaza ni Ushahidi wa Uasi wa Serikali ya Misri

Gaza imeingia katika awamu ya tano ya njaa (hatua ya njaa mbaya) kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, na wakati Waislamu kila mahali wanajaribu kuunga mkono ndugu zao kwa michango na kuzindua misafara ya kuvunja mzingiro juu yao, nchi jirani zinatazama bila hatua, haswa Misri, ambayo ina mipaka na Gaza, lakini ilidai haina la kufanya katika suala hilo, na ilitosheka na jukumu la mpatanishi, je, Misri kweli haiwezi kuwasaidia watu wa Gaza?!

Tangu mwanzo wa uchokozi wa Wayahudi dhidi ya Gaza, serikali ya Misri ilidai kwamba inatoa kila kitu inachoweza kusaidia watu wetu huko Gaza na ilikana kuwa na jukumu lolote katika kufunga vivuko na kuzingira Gaza, lakini ushahidi unaonyesha ukweli wa uongo wake, na kwamba hali ya sasa haingetokea bila ushirikiano wake na Wayahudi hata kabla ya vita vyao dhidi ya Gaza. Pamoja na mwanzo wa uchokozi, umma ulianza kuiomba Misri kuingilia kati ili kuzuia taasisi ya Kiyahudi kuwashambulia watu wetu huko Gaza na makombora, lakini kila mtu alishangaa kwamba iliwaruhusu hata kuwashambulia Wamisri wenyewe katika kivuko cha Rafah na eneo la Al-Ajra kusini mwa Rafah na maeneo mbalimbali huko Sinai, na askari walishuhudia makombora ya Wayahudi yakivuna ndugu zao huko Gaza au wenzao kwenye mipaka bila hatua kutoka kwa serikali yao; ili vita hivi vifunguliwe na matukio ya kukata tamaa na kujisalimisha.

Serikali ya Misri haikutosheka kupoteza damu ya Waislamu, lakini iliruhusu taasisi ya Kiyahudi kuchukua kivuko cha Rafah, ikipuuza masharti ya mkataba wa amani ambayo ilitumia mara nyingi kuhalalisha kushindwa kwake kuwasaidia watu wetu huko Palestina, na hii si matokeo ya udhaifu wa jeshi la Misri lakini ni usaliti, na ushahidi wa hilo ni kwamba serikali haikuchukua msimamo wowote, haikulaani Wayahudi kwa kukalia kivuko, na haikuingilia kati kuwazuia kwa nguvu au angalau kutumia njia yoyote ya kuwashinikiza, na ilitosheka kujikanusha tuhuma za kufunga kivuko na ilidai kwamba jambo lote liko mikononi mwa taasisi ya Kiyahudi, na kana kwamba ni kukiri haki ya taasisi hii vamizi kudhibiti kivuko!

Hakika, haiwezekani kuzungumzia mada hii bila kutaja mfereji wa Suez, ambao unachukuliwa kuwa moja ya njia muhimu zaidi za kuishinikiza taasisi ya Kiyahudi na Amerika, na pia ni hakika kwamba Misri ilitumia vibaya iwezekanavyo, ambapo video zilisambaa zikionyesha meli za kivita zikiwa na bendera za Amerika na taasisi ya Kiyahudi, na ilidai kwamba haina uwezo wa kuzizuia kupita kwenye mfereji kutokana na sheria za kimataifa, ili kuthibitisha kwa kila mtu kwamba sheria hizi hazionekani isipokuwa kutumikia maslahi ya Magharibi kafiri mkoloni!

Sisi huko Misri tunashuhudia matukio mabaya zaidi ya usaliti na kukata tamaa kutoka kwa mfumo ulioundwa na ukoloni kuwa mbadala wa mfumo wa Kiislamu. Na tunaiangalia ikishiriki katika kuwaua ndugu zetu huko Gaza kwa kuwazingira na kuzuia misaada kuingia kwao na kuzuia juhudi zozote za kuvunja mzingiro juu yao katika kutekeleza maagizo ya Wayahudi, hivyo inamkamata yeyote anayekusanya michango au anajaribu kufika kwenye kivuko ili kuvunja mzingiro, hivyo unaona tukio la ajabu zaidi; wanaharakati wasio Waislamu wanawaomba kwa machozi askari Waislamu kuwaruhusu kuingia ili kuwasaidia watu wetu huko Gaza, hivyo tumefika kiwango gani?!

Enyi askari wa Misri Kinana: Sisi watu wa Misri karibu tufe kwa hasira tunapoona ndugu zetu huko Gaza wakiuawa, na tunajua kwamba mna zana na vifaa vinavyowawezesha kuisaidia Gaza na kuikomboa yeye na Palestina yote, hivyo fanyeni haraka kwa heshima hii kubwa, na Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyi na yeye ndiye msaidizi wenu na hatawapunguzia matendo yenu.

﴿Mwenyezi Mungu akikuunusuruni, basi hakuna wa kukushindeni. Na akikutupilieni, ni nani huyo atakayekunusuruni baada yake? Na Waislamu wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Misri

Official Statement

مصر - المكتب

ولاية مصر

مصر - المكتب

Media Contact

مصر - المكتب

Phone:

Email: info@hizb.net

مصر - المكتب

Tel: | info@hizb.net

www.hizb.net

Reference: PR-01984405-93e8-7c9f-8443-c19d75e22541