Habari kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan
Yafanya Mkutano wa Hadhara Mashariki mwa Nile
Vijana wa Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan mashariki mwa Nile leo Jumatano tarehe 25 Rabi' al-Awwal 1447 Hijria, sawa na 17 Septemba 2025 Miladia baada ya sala ya Adhuhuri, katika Msikiti Mkuu katika soko la Sita Al-Wahda, walifanya mkutano wa hadhara ambapo walibeba mabango yanayowataka Waislamu kusimama imara, kuzuia mpango wa kuigawa Sudan kwa kuitenganisha Darfur.
Katika mkutano huo, ilisomwa hotuba iliyowataka Waislamu kutekeleza wajibu wao, kuzuia mpango huo, na mkutano huo ulipata maitikio kutoka kwa umati wa waliohudhuria, ambapo idadi yao ilisimama kusikiliza hotuba.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan