Habari kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan
Yaandaa Mkutano wa Kisiasa Khartoum
Katika kampeni yake ya kukwamisha mpango wa kuigawanya Sudan kwa kuitenganisha Darfur, vijana wa Hizb ut-Tahrir katika wilaya ya Sudan, waliandaa mkutano wa kisiasa huko Khartoum, katika eneo la soko la Al-Dukhinat Al-Awamra, asubuhi ya Jumamosi tarehe 4 Oktoba 2025 BK.
Sheikh Abdul Fattah Ahmed, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, alizungumza akianza na aya na hadithi zinazozungumzia umoja wa Umma wa Kiislamu, na umoja wa dola ya Kiislamu, ambapo Uislamu umesisitiza kuuliwa kwa yule anayetaka kuuvunja mti wa umoja wa Umma, na kuligawanya kundi lake, na kuliharibu umoja wake. Alisema: Wakati adui kafiri anapopanga njama dhidi ya umoja wa Umma na dola yake, na anajitahidi kuuvunja, basi ni lazima Waislamu walifanye suala hili kuwa suala la hatima, na wachukue hatua ya uhai au mauti kulihusu.
Na sisi katika Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Sudan, kutokana na jukumu letu kwa Umma, tunawaelezea mpango hatari, ambao Amerika inaufanya sasa wa kuikata Darfur kutoka Sudan, kama ilivyoukata kusini hapo awali.
Na Sheikh Ahmed alieleza uharamu wa mpango huu, na akawahimiza watu wa nchi kusimama kwa nguvu, kuukabili, na wana uwezo wa kufanya hivyo, ili Darfur isiende kama ilivyoenda kusini, na akawahimiza wenye ikhlasi miongoni mwa wenye nguvu na ulinzi, kuhifadhi umoja wa nchi, na kwamba Mungu atawauliza kuhusu hilo. Na akawaalika watu wa nchi kuweka mikono yao pamoja na Hizb ut-Tahrir, kusimamisha Khilafah Rashidah ambayo itakata mkono wa Amerika na Magharibi kafiri, kuchezea masuala ya Umma.
Umati ulikatisha hotuba ya Sheikh kwa takbira na tahalili, wakisema kwamba Khilafah ndio suluhisho. Kama vile mmoja wa waliohudhuria alisema, kwamba kitendo hiki ndicho kinachohitajika, na watu wanapaswa kukizunguka.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan