Organization Logo

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

Tel: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

contact@ht-bangladesh.info

Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Bangladesh Waandaa Maandamano na Mikesha Kupinga Uhamishaji wa Waislamu kwa Nguvu na India kwenda Bangladesh Chini ya Tishio la Silaha
Press Release

Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Bangladesh Waandaa Maandamano na Mikesha Kupinga Uhamishaji wa Waislamu kwa Nguvu na India kwenda Bangladesh Chini ya Tishio la Silaha

July 05, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Bangladesh Yaandaa Maandamano na Mikesha

Kupinga Uhamishaji wa Waislamu kwa Nguvu na India kwenda Bangladesh Chini ya Tishio la Silaha

Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Bangladesh leo Ijumaa, Julai 4, 2025, baada ya swala ya Ijumaa, iliandaa maandamano na mikesha katika misikiti kadhaa huko Dhaka na Chittagong, kukataa na kulaani uhamishaji wa Waislamu kwa nguvu na India kwenda Bangladesh chini ya tishio la silaha. Idadi ya vijana wa chama walitoa hotuba wakati wa mikesha hii, ikifuatiwa na maandamano ya umma.

Serikali ya Modi inawatendea Waislamu nchini India kama wanyama, ikiwaelezea kama "wahamiaji haramu", inabomoa nyumba zao, na kuwalazimisha kuondoka nchini kwa nguvu kwenda Bangladesh. Wasemaji wakati wa mikesha walilinganisha tabia hii ya taifa la Kihindu la India (Hindutva) na kile ambacho shirika la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu linafanya dhidi ya Waislamu huko Palestina.

Wasemaji walikosoa wasomi watawala na wa kilimwengu wa sasa, wakisisitiza kwamba wanatafuta kuficha ukweli wa kile kinachotokea, kwa kuhusisha matendo haya ya uchokozi na kuzorota kwa uhusiano kati ya India na Bangladesh baada ya kuanguka kwa dikteta Hasina. Hata hivyo, ukweli unathibitisha kwamba tabia hizi si mpya, lakini ni sehemu ya sera iliyoenea, inayojumuisha mauaji kwenye mipaka, uchokozi wa maji, na mateso ya kimfumo ya Waislamu ndani ya India, kuanzia kubomolewa kwa Msikiti wa kihistoria wa Babri kujenga hekalu, hadi kufuta urithi wa Kiislamu ambao ulienea kwa miaka elfu, hadi kuwataka kuondoa kaburi la Aurangzeb, na kupitisha sheria mpya ya uraia, na kusasisha Daftari la Kitaifa la Wakaazi, na sera nyinginezo, ambazo zinathibitisha kwamba lengo ni kufuta utambulisho wa Waislamu na kuwahamisha, kama shirika la Kiyahudi linavyofanya huko Palestina. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿Hakika utawakuta walio na uadui mkali zaidi kwa walioamini ni Mayahudi na washirikina﴾.

Wasemaji walieleza kuwa tabia hii ya kiburi ya taifa la Kihindu la India dhidi ya Waislamu ina sababu kuu mbili:

Kwanza: Ingawa Waislamu katika eneo hili wanaunganishwa na imani moja na damu moja, ukoloni kafiri wa Uingereza uliwagawanya kwa misingi ya kitaifa (Mhindi, Mbangali, Mpakistani...) ili kuwadhoofisha, kisha ukawalazimisha mifumo ya utawala wa kilimwengu kwa niaba. Leo, tunaona wanasiasa na wasomi wa kilimwengu wakipinga vikali dhuluma za Wahindu nchini Bangladesh, lakini wanajificha kama paka mbele ya uhalifu wa India dhidi ya Waislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Si miongoni mwetu anayeitisha ubaguzi wa kikabila, na si miongoni mwetu anayepigana kwa ubaguzi wa kikabila, na si miongoni mwetu anayekufa kwa ubaguzi wa kikabila» Imesimuliwa na Abu Daud.

Pili: India leo ni wakala wa kikanda tu wa ukoloni kafiri wa Marekani, na ni mwanachama wa muungano wa kijeshi wa "Quad" katika eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki. Kama vile ukoloni wa Marekani unavyotumia shirika la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu Mashariki ya Kati kukandamiza Umma wa Kiislamu, unatumia taifa la Kihindu la India Kusini mwa Asia kwa madhumuni hayo hayo.

Wasemaji walisisitiza kuwa ni wajibu wa Waislamu kisheria kuwasaidia ndugu zao Waislamu popote pale wanapokabiliwa na uchokozi. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿Na wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia﴾ Lakini mifumo hii ya kitaifa ya kilimwengu inayotawala katika nchi za Waislamu haihifadhi Umma, haitumi majeshi kusaidia Waislamu huko Palestina, Kashmir, au Arakan, badala yake inatuma vikosi vyake chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa na kwa maagizo kutoka Marekani kumwaga damu ya Waislamu!

Mwishoni mwa mikesha, wasemaji waliwataka Waislamu kutangaza msimamo wao waziwazi, ambao ni:

Mateso ya Waislamu duniani kote yanasababishwa na kukosekana kwa mlinzi wa kweli wa Umma wa Kiislamu, ambayo ni Khilafah. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «Hakika Imamu ni ngao, anapiganiwa nyuma yake na anaogopwa» Imesimuliwa na Muslim. Kwa hivyo, lazima tuungane kusimamisha Khilafah, bila kujali hawa watawala vibaraka. Na lazima tuuelekeze wito kwa wana wa Umma watiifu katika majeshi, ili watoe nusra kwa chama mtiifu katika Umma huu; Hizb ut-Tahrir, kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume.

Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Bangladesh

Official Statement

بنغلادش مكتب

ولاية بنغلادش

بنغلادش مكتب

Media Contact

بنغلادش مكتب

Phone: 8801798367640

Fax: Skype: htmedia.bd

Email: contact@ht-bangladesh.info

بنغلادش مكتب

Tel: 8801798367640 | contact@ht-bangladesh.info

Fax: Skype: htmedia.bd

Reference: PR-0197d075-ab70-7d66-9f8b-872346955cf0