Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji Yanayofanywa na Polisi: Akili ya Kibepari ya Kikatili na Kutoadhibiwa
(Imetafsiriwa)
Maafisa watatu wa polisi nchini Kenya wameshtakiwa kwa mauaji ya mwanablogu mwenye umri wa miaka 31, ambaye alifariki akiwa kizuizini polisi mapema mwezi huu. Kifo cha Albert Ogwang kimezua hasira nchini Kenya, ambapo maandamano yameandaliwa kutaka haki.
Hizb ut-Tahrir/Kenya inataka kuangazia yafuatayo:
Vyombo vya usalama chini ya mfumo wowote wa kilimwengu wa kiliberali, kama vile Kenya, ni mwendelezo wa mfumo wa kikoloni uliotumiwa na Waingereza kuwatawala watu na kukandamiza upinzani. Katika miaka ya 1950, Wakenya walipoanza kusisitiza haki yao ya kujitawala, polisi na vyombo vingine vya usalama vya Uingereza viliwakamata makumi ya maelfu yao na zaidi ya elfu moja walinyongwa. Inaonekana kwamba vikosi vya polisi vinawaona watu wa kawaida kama tishio linalowezekana kwa utawala unaotawala, mbinu ambayo ilitengenezwa hapo awali ili kulazimisha utawala wa kikoloni, na sio kuwalinda.
Kimsingi, mifumo ya kilimwengu ya kiliberali hutukuza maslahi na faida kuliko maisha na mali ya binadamu, na kufanya ufisadi, kutoadhibiwa, na unyakuzi wa serikali kuwa kanuni ya kisiasa. Kwa kuzingatia hili, mauaji yanayofanywa na vyombo vya serikali bila kuadhibiwa ndiyo njia pekee ya kuzuia sauti yoyote ya upinzani au juhudi za kufichua ufisadi mkubwa. Ikumbukwe kwamba ukatili na mateso yanayofanywa na vyombo vya serikali ni mwenendo wa kimataifa na sio tu kwa Kenya.
Tunasisitiza kwamba maisha ya wanadamu, au tuseme roho zote, ni takatifu na zinastahili ulinzi kamili kutoka kwa serikali bila hofu au upendeleo. Katika Uislamu, kulinda maisha ya binadamu ni muhimu sana, na kunachukuliwa kuwa amana takatifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Uislamu unasisitiza utakatifu wa nafsi, unakataza kuinyakua bila haki, na unaamuru kuhifadhiwa na kuheshimiwa kwa wanadamu wote.
Tunasisitiza kwamba chini ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume itakayosimamishwa karibuni kwa idhini ya Mungu, vikosi vya polisi vitawajibika kwa kudumisha utulivu wa umma, kutekeleza sheria na kuchunguza uhalifu. Mateso yamekatazwa kabisa, na afisa yeyote wa polisi atakayepatikana na hatia ya kufanya shambulio la kimwili au mateso dhidi ya mtu yeyote, awe Muislamu au asiye Muislamu, atawajibishwa. Kwa hivyo vikosi vya polisi vitajitolea kikamilifu kudumisha sheria na utulivu na hivyo kulinda maisha na mali ya raia.
Shabaan Muallim
Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut-Tahrir
Kenya