Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uongo wa Suluhisho la Mataifa Mawili kwa Palestina
"Muumini haumwi kutoka shimo moja mara mbili"
Wito kwa Umma wa Kiislamu
Janga linaloendelea huko Gaza, na katika ardhi yote iliyobarikiwa ya Palestina, ni kioo kinachoakisi heshima, hadhi na kujitolea kwa umma, na pia inaakisi majeraha makubwa ambayo umma umepata tangu ulipopoteza ngao yake ya kinga; Ukhalifa.
Ni kioo kinachofichua unafiki wa wazi na viwango viwili vya nguvu za kikoloni, na kinafichua uadui wao mkubwa kwa Uislamu. Sheria ya kimataifa na taasisi zake zimeonyesha ukweli wao kama hazina uwezo na hazina thamani, na zinatii kikamilifu ajenda za nguvu hizo.
Pia, Gaza imefichua waziwazi usaliti wa watawala wa Kiislamu ulimwenguni kote, badala ya kuutetea Palestina, wamejipanga na mabwana zao wakoloni, wakiwafunga jela wanajeshi wa Kiislamu, wakikandamiza madai ya watu ya kufungua mipaka, na kulinda chombo cha Kiyahudi huku kikiendeleza uhalifu wake wa mauaji na njaa.
Hata hivyo, watu wa Gaza wamevumilia katika hali ngumu zaidi, na wamekataa kujisalimisha. Na umma haukukaa kimya, lakini ulidhihirisha maneno ya Mtume ﷺ: "Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuoneana huruma na kushirikiana ni kama mwili mmoja, kiungo kimoja kinapouma, mwili wote unaitikia kwa kukesha na homa". Imesimuliwa na Bukhari na Muslim
Mtego wa kikoloni unaoitwa Suluhisho la Mataifa Mawili
Katika wakati huu muhimu, nguvu zile zile za kikoloni ambazo zilipanda chombo cha Kiyahudi zinarejea kuuza kile wanachokiita "suluhisho" kwa kuanzisha taifa la Palestina kando yake, kwani Ufaransa, Uingereza, Australia na zingine hivi karibuni zilitangaza kuunga mkono mpango huu.
Lakini hizi ni nchi zile zile ambazo zilianzisha chombo cha Kiyahudi, zikakipatia silaha, zikakifadhili na kukilinda tangu kuanzishwa kwake, na bado zinaendelea kukipatia ulinzi wa kidiplomasia, na kukipatia silaha na pesa zinazowezesha uhalifu wake. Kwa hivyo umma lazima uwe macho na usishindwe na mtego wa kukata tamaa na uchovu ambao unawasukuma kukubali suluhisho la kikoloni ambalo linawapa faraja ya muda, huku chombo vamizi kikiendelea kushikilia ardhi iliyobarikiwa. Na Mtume ﷺ alituonya akisema: "Muumini haumwi kutoka shimo moja mara mbili" Imesimuliwa na Bukhari
Kuamini kwamba wito wao wa suluhisho la mataifa mawili unatokana na wasiwasi kwa Wapalestina ni ujinga hatari. Nia zao ni za kisiasa tu, lengo lao ni kufyonza hasira ya umma inayoongezeka dhidi ya ushiriki wao katika uhalifu wa kivita, na kudumisha maslahi yao ya kimkakati katika eneo hilo. Hii ndiyo siasa ya kilimwengu katika hali yake mbaya zaidi: chafu, iliyooza, na isiyo ya kibinadamu.
Kwa nini Suluhisho la Mataifa Mawili sio Suluhisho?
Mpango wa mataifa mawili haukomboi Palestina, lakini unathibitisha uvamizi. Inatoa uhalali kwa chombo cha Kiyahudi, na inahakikisha uwepo wake, badala ya mamlaka ya Palestina isiyo na uwezo bila uhuru wa kweli; ambayo ni, inazalisha tena hali iliyopo.
Chini ya mpango huu, Wayahudi wataendelea kudhibiti mipaka, rasilimali na harakati za watu, na wataendelea kupokea msaada wa kijeshi na kifedha kutoka kwa nguvu za kikoloni, huku nchi za Kiarabu zikichukua jukumu la walinzi wa usalama wake. Mpango huu pia unatoa fursa kwa nguvu za kikoloni na nchi za Kiarabu kunawa mikono yao iliyojaa damu na uhalifu.
Nyuma ya hali halisi hii ya kijiografia, mradi huu unatumikia lengo lingine hatari, ambalo ni kuimarisha utamaduni wa uhalisia na kushindwa ndani ya umma, na kuwafunza vizazi vinavyofuata kukubali makubaliano ya sehemu, ambayo inawahimiza maadui wa Uislamu kudai zaidi, na kuzuia umma kutoka kwa njia pekee ya ukombozi.
Maono wazi ya Kiislamu
Mwenyezi Mungu ﷻ anasema: ﴿Enyi mlioamini msiwafanye maadui zangu na maadui zenu kuwa vipenzi mnawapelekea mapenzi na hali yao wamekanusha yale yaliyokujieni katika Haki wanamtoa Mtume na nyinyi﴾.
Pamoja na kuendelea kuwa macho kwa umma, lazima tusimame imara na tusidhoofike au kufanya suluhu au kufuata hatua za uhalisia ambazo zinaongeza muda wa mateso, hata kama nia ni ya kweli ya kuwapunguzia watu.
Mwenyezi Mungu ﷻ anasema: ﴿Wala msichanganye Haki na batili wala msifiche Haki na nyinyi mnajua﴾, na akasema Subhaanahu: ﴿Wala msilegee wala msihuzunike na nyinyi ndio mtakuwa juu ikiwa nyinyi ni waumini﴾.
Suluhisho la mataifa mawili ni batili, halileti ukombozi wala heshima, lakini linathibitisha unyenyekevu chini ya mfumo wa kikoloni uliowekwa, na umma lazima ukatae kabisa.
Wajibu wetu hauishii tu kupinga dhuluma ya chombo cha Kiyahudi, lakini pia unajumuisha kufanya kazi kwa ukombozi kamili wa Palestina. Na hii inahitaji zaidi ya maandamano au mazungumzo; inahitaji kuhamasisha majeshi ya Waislamu na kuanzisha Ukhalifa kwa misingi ya Utume.
Ukhalifa sio mfano wa kinadharia, lakini ni mfumo uliothibitishwa ambao Waislamu, Wakristo na Wayahudi waliishi chini yake kwa usalama, haki na amani. Na ndio mfumo pekee unaoweza kukomesha uvamizi, kuunganisha umma, na kuondoa uwepo wa kikoloni kutoka nchi zetu.
Suluhisho la mataifa mawili ni mtego unaolenga kutuliza umma na kuhakikisha uhai wa mradi wa Kizayuni. Na jibu letu lazima liwe wazi na la uamuzi: kukataa suluhisho hili batili, na kuzingatia njia pekee ambayo inahakikisha ukombozi; kuanzisha Ukhalifa, na kutumia rasilimali za umma kukomboa Palestina nzima.
Na historia itaandika ikiwa tumesimama imara kwenye ukweli au ikiwa tumekubali makubaliano. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ﷻ aujalie umma busara, umoja na ushindi.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Amerika