Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mpango wa Trump ni sumu kali, na uvamizi wa Kimarekani wa kimataifa wa Gaza, na uhalifu mkubwa unaofanywa na watawala wa Waislamu
Kujisalimisha na kuondoa silaha, kurejesha mateka na mabaki ya maiti, na uvamizi unaoongozwa na Amerika na kuongozwa na Trump kwa jina la Baraza la Amani, na kuteuliwa kwa mchukia Uislamu Tony Blair, na kutekelezwa na tawala za eneo hilo, hizo ndizo sifa za mpango mpya wa Trump ambao alitangaza na kuwashukuru viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu na washirika wake huko Uropa kwa kuuitikia, na alitangaza kuwa viongozi wa eneo hilo wanashiriki kikamilifu katika mpango wa amani.
Gaza ambayo iliudhalilisha utawala wa Kiyahudi katika vumbi na kufichua kwamba ni utawala dhaifu ambao hauhitaji chochote kuuangamiza isipokuwa uamuzi, na ili utawala mhalifu urejeshe hadhi yake, uliweka nguvu zake zote juu ya vichwa vya watu wa Gaza na Amerika na Magharibi yote iliuunga mkono kwa silaha zote za maangamizi, na watawala wa Waislamu walimsaidia kwa kila kitu walichoweza kutoka kwa njia za usambazaji na kuzingirwa na mengineyo ili kurejesha hadhi hiyo ya uwongo, hivyo Gaza iliharibiwa kabisa au karibu, na watu wake walizingirwa kuzingirwa ambayo haijawahi kuonekana, hata hivyo, utawala mhalifu ulifeli kufikia ushindi wake uliokusudiwa katika eneo lililozingirwa ambalo lina mabaki ya maisha, ili kamba ya Trump ije kuwaokoa Wayahudi, na kuwasaidia watawala wa Waislamu kwa mpango wa kuimarisha mshiko wao juu ya Gaza, wakiwataka wapiganaji kukubali, na haya yote ili Trump afanikishe kwa ajili ya utawala uliopotoka kile ambacho hakukifanikiwa kwa miaka miwili, akifanya chombo cha utekelezaji kuwa ni tawala za madhara katika nchi yetu, baada ya kuitelekeza Gaza na watu wake kwa miaka miwili kamili, na matokeo yake ni kuikabidhi Gaza kwa Trump bila juhudi zozote, bali kwa pesa za umma na askari wake!
Hakika Trump anapanga kwa ajili ya Gaza kana kwamba ni mali yake, kisha watawala vibaraka wanafurahi kuikabidhi kwake kana kwamba wamewaokoa watu wake, na wamefuma na bwana wao nyuzi za kuiwasilisha, na kuifanya kuwa mradi wa uvamizi wa kimataifa, uvamizi kwa jina la ujenzi juu ya mito ya damu na milima ya fuvu na mifupa!!
Kisha kujisalimisha kwa Gaza baada ya hapo itakuwa utangulizi wa kurejesha uhusiano wa kawaida na mikataba ya Ibrahimu ili utawala mhalifu uingie katika eneo hilo kana kwamba unazawadiwa kwa uhalifu wake.
Hakika kukubali mpango wa Trump ni uhalifu ambao watawala wanabeba mzigo wake, lakini pia ni mzigo ambao umma wa Kiislamu hautasalimika nao isipokuwa wabadilike na kukataa uhalifu wao.
Kisha ni mzigo ambao majeshi ya umma hayatasalimika nao ambayo yamechelewa kutimiza wajibu wao, na lau majeshi hayo yangechukua msukumo kutoka kwa ushujaa wa Gaza na kurekebisha kile walichochelewa nacho cha ukombozi wa Baitul Muqaddas na viunga vyake, na lau wangeitikia wito wa kuomba msaada kutoka Gaza na maeneo yaliyoizunguka, Trump asingepata nafasi ya mpango wake wala asingethubutu kuota mbegu ya udongo huko Gaza Hashim.
Hata hivyo, fursa haijapita bado ingawa imechelewa, kwani Gaza pamoja na wanaume, wanawake, wazee na vijana wake, na misikiti na minara yake inatoa wito kwa majeshi kusonga mbele, ili kwa kusonga mbele kwake iukomboe Baitul Muqaddas, na kuwazuia watawala kurejesha uhusiano wa kawaida juu ya fuvu na mifupa ya Gaza na kurejesha Msikiti wa Al-Aqsa na ardhi iliyobarikiwa kama ilivyokuwa, tukufu na imara, bali na kuifanya Baitul Muqaddas kuwa kitovu cha Uislamu.
Na tunahitimisha kwa wito wa Mwenyezi Mungu kwa waumini: ﴿Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu atakayewafanya marafiki, basi huyo ni miongoni mwao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. Utawaona wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi wanavyo hima kukimbilia kwao, wanasema: Tunakhofia yasitupate mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi, au jambo jingine litokalo kwake, basi watajuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao﴾.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa Palestina