Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan Mbele ya Msikiti Mkuu katika Mji wa Port Sudan
Wito kwa Watu wa Sudan.. Msiruhusu Amerika kuipasua nchi yenu na kuichuna ngozi Darfur
Anasema Mtukufu: ﴿NA HII DINI YENU NI DINI MOJA, NAMI NDIYE MOLA WENU BASI MCHENI﴾, na anasema ﷺ, kama alivyosimulia Muslim: «YEYOTE ANAYETAKA KUIFANYA KIKUNDI HII UMMA HALI YAKUWA WAMOJA, BASI MPIGENI KWA UPANGA YEYOTE YULE».
Enyi Waislamu: Hakika mataifa katika maisha yao yana masuala ya hatari, yaani masuala ambayo yanachukuliwa hatua moja nayo nayo ni kuishi katika kivuli chake au kufa kwa ajili yake, na itikadi ya Kiislamu imetubainishia sisi Waislamu masuala yetu ya hatari; yaani yale ambayo yanachukuliwa hatua ya maisha au kifo, na miongoni mwa masuala haya ya hatari ni suala la umoja wa dola na umoja wa umma, na tulipopunguza suala hili hadhi yake hapo awali, Amerika iliweza kwa msaada wa baadhi ya wana wetu kuipasua nchi yetu, na kuitenganisha kusini mwa Sudan, na sasa inarejea kukamilisha ilichoanza hapo awali, ili kuchora kwa mipaka ya damu dola mpya katika kilichosalia cha nchi yetu; kwa kuichuna ngozi Darfur, ambapo matukio yanaenda kasi kuhudumia mpango wa Amerika kwa msaada wa vyombo vyake ndani na nje.
Hakika Amerika ambayo ilitenganisha kusini mwa Sudan; chini ya madai ya amani bandia, na kwa mikono ya watawala na waasi, na kwa baraka za wanasiasa na baadhi ya wanahabari na kimya cha wanachuoni, inajitahidi leo kwa mtindo huo huo, kuichuna ngozi Darfur kutoka Sudan; kwa kuandaa jukwaa huko Darfur; ambalo linadhibitiwa na vikosi vya msaada wa haraka isipokuwa Al-Fashir, ambayo inajitahidi kuiangusha, na imeanzisha dola kwa kutangaza serikali sambamba katika mji wa Nyala; mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini, je, mtaiacha ifanye hivyo katika nchi yenu?! Na Mungu atakuulizeni baada ya kuwataka mfe bila ya kafiri mkoloni kutimiza lengo lake.
Enyi watu wa Sudan: Simameni kuhujumu mpango, na kung'oa mizizi ya vibaraka na wanafiki, na kurekebisha mwelekeo wa maisha yenu, kwani muumini haumwi mara mbili kutoka tundu moja, na tumeumwa kutoka tundu la Amerika kwa kuitenganisha kusini mwa Sudan, je, tutairuhusu kutenganisha Darfur?! Al-Bukhari na Muslim wamesimulia kutoka kwa Abu Hurairah, Radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume ﷺ, kwamba alisema: «Muumini haumwi mara mbili kutoka tundu moja».
Basi simameni enyi Waislamu kumtii Mwenyezi Mungu, kwa kulifanya suala la umoja wa taasisi ya dola kuwa suala la hatari, ambalo linachukuliwa hatua ya maisha au kifo, kutoka kwa Arfaja alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema: «YOYOTE ANAYEKUJIA HALI YAKUWA JITIHADA ZENU NI ZA PAMOJA JUU YA MTU MMOJA, AKITAKA KUVUNJA GOGO LAKO, AU KUITAWANYA JAMAA YENU, BASI MUUWE».
Je, tutamtii mpenzi wetu Muhammad ﷺ, au tutamtii Amerika kafiri mkoloni?! Hakuna shaka kwamba tunamtii Mtume ﷺ tukijibu amri ya Mola wetu Mwenyezi aliyesema: ﴿NA MTIINI ALLAH NA MTIINI MTUME NA TAHADHARINI MKIPUUZA BASI JUENI KUWA JUU YA MTUME WETU NI UFIKISHAJI WA WAZI﴾. Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: ﴿NA ALICHOKULETEENI MTUME CHUKUENI NA ALILOKUKATAZENI ACHENI NA MCHENI ALLAH HAKIKA ALLAH NI MKALI WA KUADHIBU﴾.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Sudan