Organization Logo

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707

spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Neno la Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan Katika Mkutano na Waandishi wa Habari Siku ya Jumamosi 22 Safar 1447 Hijria, Inayolingana na 2025/08/16 Miladia, yenye kichwa: "Wito kwa Watu wa Sudan.. Iokoeni Darfur Isije Ikaungana na Kusini"
Press Release

Neno la Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan Katika Mkutano na Waandishi wa Habari Siku ya Jumamosi 22 Safar 1447 Hijria, Inayolingana na 2025/08/16 Miladia, yenye kichwa: "Wito kwa Watu wa Sudan.. Iokoeni Darfur Isije Ikaungana na Kusini"

August 16, 2025
Location

Neno la Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan Katika Mkutano na Waandishi wa Habari

Siku ya Jumamosi 22 Safar 1447 Hijria, Inayolingana na 2025/08/16 Miladia, yenye kichwa:

"Wito kwa Watu wa Sudan.. Iokoeni Darfur Isije Ikaungana na Kusini"

Majeshi ya Msaada wa Haraka yalitangaza siku ya Jumamosi 2025/07/26 Miladia, kuunda serikali sambamba na serikali iliyopo Sudan, katika mji mkuu wa Darfur Kusini (Nyala), na hatua hii ya Majeshi ya Msaada wa Haraka, ni hatua ya kimaendeleo katika kutenganisha eneo la Darfur, ambalo wanalidhibiti, isipokuwa sehemu za mji wa Al-Fasher, ambao wameuwekea mzingiro mkali kwa zaidi ya mwaka mmoja, na wanafanya mashambulizi ya mara kwa mara ili kuuangusha, ili eneo lote la Darfur liwe chini ya udhibiti wao.

Enyi watu wa Sudan:

Mfululizo wa Marekani wa kutenganisha Darfur ulianza miaka mingi iliyopita, kama ilivyokuwa ikishikilia faili la Sudan Kusini mpaka ilipeleka kwenye kujitenga na Kaskazini, na sasa inakwenda na matukio yale yale, ambayo ilitenganisha nayo Kusini ili kutenganisha Darfur, ambapo ilianza kivitendo kwa kusaini kile kinachoitwa mkataba wa amani mnamo 2011/07/14 Miladia, na ilipa eneo la Darfur uhuru mpana, na suala la uhuru daima ni mwanzo halisi wa kwenda katika mfululizo wa kupasua, na licha ya kwamba; yaani Marekani, ndiyo iliyoanzisha makubaliano haya, lakini haikuona kuwa makubaliano ya mwisho, kwani msemaji wa wizara yake ya mambo ya nje wakati huo Mark Toner, alitoa kauli baada ya kusainiwa mkataba akisema: (Mkataba huu ni hatua ya kusonga mbele kuelekea suluhisho la kudumu la mzozo wa Darfur).

Na kinachothibitisha kuwa Marekani ndiyo iliyotenganisha Sudan Kusini, na inataka kupasua kilichosalia cha Sudan, ni matamshi ya Omar al-Bashir, katika mahojiano yake na shirika la Sputnik la Urusi, ambayo yalichapishwa mnamo 2017/11/25 Miladia, ambapo alisema: (Masuala yangu ya Darfur na Sudan Kusini yalipata uungwaji mkono kutoka kwa Marekani, na chini ya shinikizo lake Sudan Kusini ilijitenga), na akaongeza: (Sasa tuna habari kwamba jitihada za Marekani ni kuigawanya Sudan katika nchi tano), jambo ambalo linathibitisha kuwa Marekani ndiyo iliyotenganisha Sudan Kusini, na sasa inatafuta kuitenganisha Darfur, ikiwa itafanikiwa - Mungu apishilie mbali - basi itapasua maeneo mengine ya Sudan moja baada ya jingine, na itafanya hivyo ili kuchora mipaka ya nchi tano katika nchi yenu kwa damu yenu na damu ya watoto wenu kama ilivyofanya hapo awali kwa kuitenganisha Kusini kwa damu ya watu wenu milioni 2 na kama inavyofanya sasa ili kuitenganisha Darfur kwa damu ya mamia ya maelfu yenu, basi amkeni enyi watu wa Sudan ili kufeli mpango huo na kung'oa mizizi ya vibaraka na wanafiki na kurekebisha mkondo wa maisha yenu.

Enyi watu wa Sudan:

Muumini haumwi mara mbili kutoka tundu moja, na tumeumwa kutoka tundu la Marekani kwa kuitenganisha Sudan Kusini, je, tutairuhusu kuitenganisha Darfur?! Bukhari na Muslim wameripoti kutoka kwa Abu Hurairah, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Nabii ﷺ, kwamba alisema: «Muumini haumwi mara mbili kutoka tundu moja».

Hakuna nchi yoyote inaruhusu maeneo yake kupasuliwa, kwa sababu katika umoja kuna nguvu na katika utengano kuna udhaifu na unyonge, vipi ikiwa Uislamu umefanya suala la umoja wa umma, na umoja wa taasisi yake kuwa suala la hatima, hatua ya uhai au mauti inachukuliwa kwalo? Kutoka kwa Arfaja alisema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema: «Yeyote anayekujieni na jambo lenu lote liko juu ya mtu mmoja, anataka kuipasua fimbo yenu, au kutenganisha kundi lenu, basi muuweni».

Enyi Waislamu:

Vipi mnanyamaza kimya juu ya kupasuliwa nchi yenu na hamuendi, na hamfanyi umoja wa nchi yenu kuwa suala la hatima kama alivyowaamuru Nabii wenu ﷺ?! Mnamtii nani? Je, mnamtii Marekani kafiri mkoloni, au mpenzi wenu mteule rehema na amani zimshukie?! Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Na alichokuleteeni Mtume chukueni, na alichokukatazeni achilieni mbali. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu﴾, na anasema Subhaanahu: ﴿Na mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume, na tahadharini. Na mkigeuka basi jueni kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe wazi﴾.

Enyi wanahabari:

Kazi yenu ni kubwa katika kuwafahamisha watu kuhusu hatari za kupasuliwa, basi fanyeni kalamu zenu, na taasisi zenu za habari kuwa mimbari ya ufahamu, mnafunua mipango ya makafiri wakoloni na wasaidizi wao ambao wanawasaidia katika kutekeleza njama zao dhidi ya nchi yetu na umoja wake, kwani nyinyi ni waaminifu katika kusema ukweli, na kusimama dhidi ya ubatili, Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Sema: Umekuja ukweli, na ubatili hauanzi wala haurudi﴾.

Enyi wanasiasa:

Jukumu la kulinda umoja wa nchi, ni jukumu lenu la kwanza, kwa kuzingatia kwamba nyinyi ni viongozi, na machifu, na vichwa vya watu, kwa hiyo kusimama kwenu dhidi ya miradi ya kupasua na kutawanya, ndiyo kinga, basi msiwe wasaidizi wa kafiri mkoloni, naye anatekeleza kupitia kwenu njama zake, Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Wala msiwategemee walio dhulumu, isije ikakuguseni moto. Wala hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala hamtanusuriwa.﴾.

Enyi Maulamaa, enyi warithi wa Manabii:

Jukumu lenu katika kuwaongoza viongozi na watawala, kwa haki na usahihi ni kubwa, basi msiwe wapandwa nao, mnatoa fatwa kwa kile wanachotamani, wala msikae kimya juu ya kusema ukweli bila kujali matokeo, Nabii ﷺ anasema: «Yeyote anayeficha elimu, Mwenyezi Mungu atamziba siku ya Kiyama kwa hatamu ya moto», na mnajua kuwa kulegeza umoja wa umma na taasisi yake ni dhambi kubwa.

Enyi Maafisa na Askari:

Enyi mliyoapa kulinda umoja wa nchi yenu, vipi mnaruhusu kupasuliwa kwake huku mnaangalia?! Kwani Mwenyezi Mungu atawauliza kuhusu ahadi yenu mliyoikata, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ﴿Na timizeni ahadi. Hakika ahadi itaulizwa﴾, basi msiruhusu kuitenganisha Darfur, na kabla ya hapo mlilegalega katika Sudan Kusini, basi ondoeni dhambi kutoka kwa shingo zenu, na simameni imara kwa mpango wa Marekani na muihamasishe jeshi ili kufeli mpango wa kupasua nchi yenu.

Na mjue kuwa misiba hii mikubwa, na njama za makafiri wakoloni zinazoendelea, hazitakuwa na tiba isipokuwa kwa kurudi kwenye Uislamu mtukufu kama itikadi na mifumo ya maisha, na hilo halitakuwa isipokuwa kwa kusimamisha dola ya Uislamu; Khilafah, na hilo linatimia tu kwa kuipa nusra Hizb ut-Tahrir, ili iisimamishe kwa uongofu juu ya manhaj ya Utume, inakatisha kwayo mizizi ya makafiri na kuunganisha nchi za Waislamu.

Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye lile linalo kuishieni.﴾.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir

Katika Wilaya ya Sudan

Official Statement

السودان - مكتب - ناطق

ولاية السودان

السودان - مكتب - ناطق

Media Contact

السودان - مكتب - ناطق

Phone: 0912240143- 0912377707

Email: spokman_sd@dbzmail.com

السودان - مكتب - ناطق

الخرطوم شرق- عمارة الوقف الطابق الأرضي -شارع 21 اكتوبر- غرب شارع المك نمر

Tel: 0912240143- 0912377707 | spokman_sd@dbzmail.com

www.hizb-ut-tahrir.info

Reference: PR-0198b217-5ba0-70e2-8182-f4fd4d58d046