
5/8/2025
Kushi News: Zuieni Mpango wa Kutenganisha Darfur, Hotuba ya Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan katika Soko la Port Sudan
Pamoja na kuongezeka kwa matukio ya kusikitisha nchini Sudan, kuzingirwa kamili kwa mji wa Al-Fashir kaskazini mwa Darfur, na mateso ya wakazi wa Kadugli na Al-Dilling, na miji mingi ya Sudan, kutokana na vita hivi vilivyolaaniwa, pamoja na hayo yote, nguvu za kisiasa, harakati za silaha, na baadhi ya viongozi wa jeshi wanashiriki katika kuitayarisha Darfur kujitenga, kwa ajili hiyo, Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan, iliandaa hotuba ya kisiasa katika Soko Kuu katika mji wa Port Sudan, leo Jumatatu, 10 Safar 1447 Hijria, sawa na 04/08/2025 Miladia, yenye kichwa: (Zuieni Mpango wa Kutenganisha Darfur). Alihutubia Ustadh / Muhammad Jami Abu Ayman, msaidizi wa msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan, umati wa waliohudhuria mbele ya Hoteli ya Al-Haramain katika Soko Kuu katika mji wa Port Sudan.
Msemaji alianza hotuba yake na aya tukufu: (Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: mlipokuwa maadui, naye akaziunganisha nyoyo zenu, na kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto, naye akakuokoeni nalo. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyokubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka), na akasema kuwa Uislamu ulikataza Waislamu wasifarakane na kugawanyika katika mataifa madogo, na akawakumbusha njama za makafiri zinazofumwa za kuipasua nchi za Waislamu kwa ujumla na Sudan haswa, na kwamba vyombo vyao vya ndani ni kutoka kwa watoto wa Waislamu, ambao wanachinjana katika vita vichafu, na kile kilichotokea cha kutenganishwa kwa Kusini mwa Sudan kwa faida ya kichwa cha uovu Amerika, na kile kilichoandamana nacho cha majanga wanayoyakabili watu wa Kusini na Kaskazini, ilikuwa mwanzo wa kwenda katika kuigawanya Sudan.
Kisha akaonya juu ya njama iliyopangwa leo, na nia mbaya za kuitenga Darfur, na Kordofan Kusini, na Blue Nile na zinginezo.. na akabeba jukumu kwa kila mtu anayefanya kitendo ambacho kinaweza kusababisha kuigawanya nchi, na akaelezea uchafu wa wito wa kikabila, kikanda, na kikabila, ambao unachochea mizozo kati ya wana wa umma mmoja, akitoa hoja kwa hadithi ya Mtume Muhammad,rehema na amani zimshukie, akisema: (Yeyote anayekujieni hali mko pamoja kwa mtu mmoja, akataka kuivunja fimbo yenu, au kuwafarakanisha jamaa yenu, basi muuweni), na dalili zinginezo ambazo zinahifadhi umoja wa umma, na kuzuia kufarakana kwa Waislamu.
Kisha akasisitiza kufanya kazi ya kuzima njama hizi, na kujitahidi kufanya kazi na wafanyakazi, kuishi katika kivuli cha Dola ya Khilafah Rashidah ambayo itakata mkono wa kila mshiriki katika njama dhidi ya nchi za Waislamu.
Hotuba ilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa waliohudhuria, na walishirikiana nayo kwa furaha.
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Kushi News

