
21/7/2025
Kushi News: Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan yafanya mkutano wa kisiasa
Kufuatia kuongezeka kwa wizi, uporaji, na kuwatisha watu salama, katika miji mingi ya Sudan, Hizb ut-Tahrir / Wilaya ya Sudan, ilifanya, saa nne za jioni leo Jumatatu, 26 Muharram 1447 Hijria, ambayo inalingana na 21/07/2025 Miladia, mkutano wa kisiasa, mbele ya Hoteli ya Al-Haramain katika Soko Kuu, katika mji wa Port Sudan, ambapo Al-Ustadh Muhammad Jami Abu Ayman, msaidizi wa msemaji rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan, alizungumza.
Al-Ustadh Abu Ayman alianza hotuba yake, akieleza umuhimu wa usalama, na kwamba ni hitaji la msingi ambalo mwanadamu analihitaji katika maisha yake, na kwamba Uislamu umeteremsha sheria na hukumu, ambazo kwa kutekelezwa kwake katika dola, usalama kwa jamii utakuwa umehakikishwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimshukie, alisema: (Yeyote anayeamka akiwa salama katika kundi lake, ana afya mwilini mwake, ana chakula cha siku yake, basi kana kwamba dunia imekusanywa kwake kwa ukamilifu wake).
Kisha akaeleza jinsi Uislamu ulivyojali kupambana na uhalifu wa kila aina, hasa wizi, uporaji, na uvamizi, na mengineyo, kwa mfumo wa adhabu za Kiislamu, na kutoka kwazo ni mipaka ya kisheria, ambayo dola inatekeleza ili iwe mazuwaji na majawiri, na akatumia hadithi: "Kusimamisha haddi katika ardhi ni bora kwa watu wake kuliko mvua ya usiku arobaini", na jinsi ulegevu katika utekelezaji wa mipaka ya Mwenyezi Mungu, umeleta ujasiri kwa wahalifu kufanya ufisadi katika ardhi.
Kama vile Mwenyezi Mungu alivyosema: {Hakika malipo ya wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wanaofanya juhudi za kufanya uharibifu katika ardhi ni kuuliwa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa kupishana au kufukuzwa katika ardhi. Hiyo ni fedheha kwao katika dunia, na katika Akhera watapata adhabu kubwa.} [Al-Maidah: 33], akizungumza kuhusu haddi ya uharibifu na umuhimu wa kuitumia kwa kile kinachoitwa magenge ya tisa ndefu, na lau haddi moja ingetumiwa, wahalifu wangezuiwa mara moja, na sura hizi za uhalifu zingetoweka kutoka katika maisha yetu.
Watu waliohudhuria waliendelea kufuatilia hotuba kwa shauku, hata mmoja wao alibeba bendera kuonyesha msimamo wake na bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimshukie, popote inapoinuliwa, kulingana na msemo wake.
Na mwishoni, mzungumzaji aliwahimiza waliohudhuria kufanya kazi ya kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu katika ardhi, kwa wale wanaotafuta usalama na utulivu, na hii haitapatikana ila Waislamu wakijitahidi kupata dola ya Khilafah ambayo inatekeleza hukumu za Kiislamu na kuibeba kwa ulimwengu kwa da'wah na jihad, akitumia hadithi ya Mtume ﷺ : (Hakika yeyote atakayeishi miongoni mwenu baada yangu ataona tofauti nyingi, basi shikamaneni na sunna yangu na sunna za Makhalifa waongofu waongozaji baada yangu, ziumeni kwa magego). Imetolewa na Abu Dawood, Al-Tirmidhi, Ibn Majah, na Ahmad.
Na himdi zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Kushi News

